Watu wanatafuta kila namna ya kukosoa. Ujinga mtupu. Kwa nature ya watu tulionao na unafiki ulivyo mkubwa viongozi wa taifa hili wanatakiwa wawe wanafanya maamuzi magumu linapokuwa ni swala lenye manufaa kwa Taifa.
Kuna watu wao ni kukosoa kila kitu. Mradi wa mwalimu nyerere ni fundisho tosha kwa wa Tz kuhusu aina ya viongozi tunaowataka. Hata kama Magufuli hayupo hai lazima tushukuru uthubutu wake katika hili. Mzee alikuwa anaona mbali sana. Pia Raisi Samia lazima tumpongeze kwa kazi kubwa aliyo ifanya . Kwa hali aliyoipokea nchi angeweza kuachana na mradi huu ili kufurahisha mioyo ya waliokuwa wanampinga Magufuli. Lakini ameweza kuishi kwenye Maono ya Magufuli na kupambana mpaka mradi umekamilika.
Wapingaji kila kitu husasan wanaoandamana saiv wawe na chembe ya aibu. Kama ni waungwana Watoke hadharani waombe msamaha kwa watanzania kwa kutumika vibaya kwa kutolitakia mema Taifa.
Raisi Samia na viongozi wengine Msikubali kabisa kutolewa kwenye reli kunapokuwa na jambo la msingi na lenye manufaa kwa Taifa. Kuna wanasiasa wanaotumika. Wananchi tunajua cha kuwafanya 2025