Mlishaonywa kua huo ujenzi wa reli ya kisasa ulikufa na bwana yule, yule bwana angekuwepo asingeruhusu haya, alikuwa na nia ya kuufanya huo mradi uipe heshima hii nchi japo Pesa za ujenzi inaonekana ilikuwa mtitii sana,
Tuseme ukweli hii nchi iko mikononi mwa wafanyabiashara kwa mgongo wa wawekezaji, na hawa ndio watakaouteka huo mradi na hata huo mradi wa bwawa la umeme watauteka tu, kubali kataa, hao wafanyabiashara ndio hawa hawa wauzaji na wasambazaji wa vifaa vya magari, mafuta na umeme, pia ni wafanyabiashara wa usafirishaji abiria na mizigo kwa njia za mabasi na malori, na hao hao ndio wanufaikaji wa biashara nyingi nchini.
Ujenzi wa reli ya treni pia ni tishio kwa wauzaji wa vipuri vya mabasi na malori, maana malori yao na mabasi yakipunguza routes mnadhani watauzaje spea?
Ukweli mchungu huo mradi lazima ucheleweshwe na hata ukitimia lzma ufanyiwe hujuma za kuupunguza kasi ama thamani kwa waTanzania ili wauchukie, ni kama hivyo mnavyoletewa matreni ya vita vya pili vya dunia, ili muyachukie na mubaki na safari luxuries za mabasi, karibia90% ya wasafiri wa Dar-Dodoma, dar-moro wangeachana na mabasi, maana treni ingetatua kero ya muda wa safari, usalama, na nauli ya safari, na tungesikia vilio vikubwa vya matajiri wa mabasi wakiilalamikia serikali[emoji23][emoji23].
Kwa nchi masikini na isiyo na dira ya maendeleo ni ngumu kutoroka kwenye mitego ya hawa washenzi wanyonyaji wanaojificha kwenye mwamvuli wa wawekezaji.
Wawekezaji bora ni wale wanaoipa thamani miradi ya wazawa.
Sir100 na genge lake la c+c+m hawana huruma na maisha ya waTanzania.