fukunyuku1234
JF-Expert Member
- Mar 12, 2024
- 243
- 494
Taarifa za kifo cha huyu mtoto zimeumiza mioyo yetu, mtoto wa miaka miwili kufanyiwa ukatili huu si jambo la kulifumbia macho na ilipaswa tupaze sauti tangu alipokamatwa tarehe 30/05/2024.
Uhai wa Asimwe umedhulumiwa na watu wabaya kwa sababu zao wanazozijua wenyewe lakini kama Taifa tumeshindwa kumlinda mtoto mdogo kwa hapa inabidi tujitafakari.
Ingependeza kama kungetolewa onyo kali kutoka ngazi za juu ili kukomesha mauaji haya ambayo yalipotea kwa muda isaidie kuzuia kasi yake isije ikarudi kama zamani.
Mwisho kabisa watanzania tubadilike na kuachana na hizi dhana wa kuamini mambo ya gizani na tumuogope Mungu ambae ndie muumba wa vyote.
Pumzika Asimwe
Pia soma:
- Kagera: Kisa cha Mtoto mwenye Ualibino kudaiwa kuibiwa, RPC Makungu asema tayari wameanza uchunguzi
- Kufuta mauaji ya albino, ni kutokomeza kabisa Waganga wapiga ramli
- Update: Mwili wa Mtoto Albino (Asimwe) wakutwa hauna baadhi ya viungo