Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"alipokamatwa" tarehe 30/05/2024. Mtoto huyu hakukamatwa alitekwa na wakora.View attachment 3020022
Taarifa za kifo cha huyu mtoto zimeumiza mioyo yetu,mtoto wa miaka miwili kufanyiwa ukatili huu si jambo la kulifumbia macho na ilipaswa tupaze sauti tangu alipokamatwa tarehe 30/05/2024.
Uhai wa Asimwe umedhulumiwa na watu wabaya kwa sababu zao wanazozijua wenyewe lakini kama Taifa tumeshindwa kumlinda mtoto mdogo kwa hapa inabidi tujitafakari.
Ingependeza kama kungetolewa onyo kali kutoka ngazi za juu ili kukomesha mauaji haya ambayo yalipotea kwa muda isaidie kuzuia kasi yake isije ikarudi kama zamani.
Mwisho kabisa watanzania tubadilike na kuachana na hizi dhana wa kuamini mambo ya wasgizani na tumuogope Mungu ambae ndie muumba wa vyote.
Pumzika Asimwe
Kiroboto Lucas Mwashambwa njoo hapa umtetee mama.Rais hakuonekana kuumizwa hata kidogo na huyu mtoto ndo maana hamjasikia kauli yoyote kutoka kwake.
Angekuwa kaumizwa angeitisha press conference ya ghafla na kisha kufunga mipaka yote kwa muda,na kisha kumpa IGP na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa siku 14 wawe wamewapata wauaji wakiwa hai au wamekufa,na ikibidi kuomba msaada Scotland Yard na FBI,huwa nasema siye hatuna Serikali tuna genge la wahuni tu walioshika Bunduki.
Aisee unaweza kuhisi labda sisi tuna planet yetu yani kila uchao ni vituko fikirishi kiasi cha kujiuliza hivi tuna serikali?kila kona ni mapambio lakini huwez kusikia makemeo kutoka ngazi za juu kwenye mambo yanayodisturb jamii inaumiza sana kwa kweliSerikali na Bunge zipo bize na Mpina
Umenena vema mzee na ni ishu inayowezekana kabisa lakini huwezi kusikia mpango kazi kama huo cha msingi wakikamatwa wauwawe mbona vibaka tunawaua daily kitaa huku?Ilitakiwa siku mtoto anapotea Jeshi, polisi, usalama na kila chombo cha dola waingie Kagera. Baa zifungwe, wauza bangi, waganga wa kienyeji, watiliwa mashaka wote ndani. Kila kijiji kila nyumba oparesheni. Hata asipopatikana lakini siku nyingine mtu akimuona albino awe kama ameona msafara wa Rais. Kila raia anakuwa mlinzi. Kanda ya ziwa wamezidi ujinga.
Ina mana wauaji walikuwa wanaskilizia kwanza.....walipoona kimya kumepoa nadhan ndo wakatekeleza unyama wao.....dah! so painful.100 % correct na kwa kufanya hivyo huyo mtoto angeweza kupatikana akiwa hai maana katoroshwa tangu 30/05/2024 kakutwa amefariki 17/06/2024
Huyu mtoto ni peponi moja kwa mojaMwenyezi Mungu, ailaze mahala pema, peponi roho ya mtoto mzuri Asimwe.
Hawa watu wenye imani potofu hawa, walaanike. Unaanzaje kuuwa Malaika asiye na kosa lolote?
Tuanze kampeni ya kuwalinda Albino, Serikali muamke sasa, kuwalinda na kuwapa Elimu, jamii inayoishi nao wasishiriki, watoe taarifa mtu akigusia hilo.
ArushaHizi ni mambo za kiboya sana na zipo huko kanda ya ziwa
Inafaa sasa alibino waamishwe huko waamishiwe mikoa salama kama Arusha ambapo alibino wanaishi kwa amani
Nasikitika kukujurisha kwamba haitakua vile unatamani.Kiasi nimeumia juu ya huyu mtoto siwezi kueleza. Washukiwa wa huu unyama wakikamatwa polisi wafanye press tuwaone na kesi yao hadi hukumu viendeshwe kwa uwazi na liwe funzo.
Kwanza tunatakiwa kuwaona katika press wakiwa hoi kwa kipigo, unyama walioufanya hawana haki yoyote ya kiubinadamu.
Nikumbushe lini albino aliuwawa au kukatwa viungo huko ArushaArusha
Njombe
Moshi
Iringa
Geita
Hii mikoa inaongoza kwa mauwaji ya watu, hiyo salama sijui inatoka wapi. Ni bora ukasema Dar, tanga na pwani yote kwa ujumla
Mkuu jiulize why kikikaribia kipindi cha uchaguzi haya mauaji yanatokea sana!!!yaani ningekua RAIS mm, ningekamata waganga wote na kupiga risasi hadharani!!View attachment 3020022
Taarifa za kifo cha huyu mtoto zimeumiza mioyo yetu,mtoto wa miaka miwili kufanyiwa ukatili huu si jambo la kulifumbia macho na ilipaswa tupaze sauti tangu alipokamatwa tarehe 30/05/2024.
Uhai wa Asimwe umedhulumiwa na watu wabaya kwa sababu zao wanazozijua wenyewe lakini kama Taifa tumeshindwa kumlinda mtoto mdogo kwa hapa inabidi tujitafakari.
Ingependeza kama kungetolewa onyo kali kutoka ngazi za juu ili kukomesha mauaji haya ambayo yalipotea kwa muda isaidie kuzuia kasi yake isije ikarudi kama zamani.
Mwisho kabisa watanzania tubadilike na kuachana na hizi dhana wa kuamini mambo ya gizani na tumuogope Mungu ambae ndie muumba wa vyote.
Pumzika Asimwe
Nikumbushe lini albino aliuwawa au kukatwa viungo huko Arusha
Arusha ni sehemu albino wanaishi kwa amani na furaha wanatembea kwa uhuru bila hofu ya kutekwa na kuuwawa.
Tanzania si salama kwa Watanzania wote CCM ikiendelea kuwepo.Tanzania si salama kwa Albino hasa kanda ya ziwa