Kama kuna Medali ambayo Taifa tunastahili basi ni Medali ya vipaji vya kuamini miujiza ya kuvuna tusichokipanda.
Kama tunavyofanya kwenye tozo, badala Mamlaka kuandaa kwanza Wananchi wenye uwezo wa kulipa 'tozo' wao wanaanza na tozo kwanza wakiahidi uwezo wa kulipa utakuja huko mbeleni.
Na ndio vivyo hivyo tunachokifanya hata kwenye maeneo mengine...nina imani bila ya shaka hata Waziri wa Michezo hawezi kubughuhiwa kwa maswali kwa kilichotokea kwani naye atahoji mbona inafanyika hivyo maeneo yote?.
Kama taifa tunaamini tukiendelea tu kushiriki Olympic zote basi kuna siku tutabahatisha Medali, na mpaka sasa tumeshakata miaka 41 tukitoka kapa, labda bado 100 mingine.
View attachment 1884913