SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Muziki wa Afrika Kusini uko "influenced" sana na historia zao za mapambano dhidi ya ubaguzi. Style zao za uimbaji na uchezaji zinatoka moja kwa moja katika viwanja vya mapambano ya kudai usawa na kupinga ubaguzi wa rangi.
Style yao mpya ya muziki wa Amapiano imemix mitindo hiyo ya zamani ya muziki wa mapambano lakini wameongeza pia influence ya uhuru wa kijinsia yaani "free sexual expression". Ndiyo maana dance move nyingi za Amapiano zimekaa "kike kike" ingawa zinachezwa na watu wa jinsia zote.
Zamani katika muziki ya aina nyingi ilikuwa rahisi kutofautisha dance za kike na zile za kiume ila Amapiano imekuja kubadili hilo. Kwa kiasi kikubwa hili limechangiwa na kwamba Afrika Kusini ni moja ya nchi za kwanza kukubali masuala ya jinsia mbadala na ushoga. Huu ndiyo msingi wa Amapiano.
Kinachonishangaza ni kwamba Watanzania tumeukubali huu muziki wa Afrika Kusini na hadi tunatamba nao huko duniani kama vile ni muziki wetu ila nabaki najiuliza, hivi sisi hatuna muziki wetu uliokuwa influenced na mapambano ya kudai uhuru, haki na usawa nchi hii?
Kama tumeamua kukumbatia muziki wa Afrika Kusini, mbona style kama hii kwenye picha sioni kina Jux, Diamond, Marioo, Harmonize, Nandy na Zuchu wakiipiga?