Tumeumia, lakini chonde chonde tusiandamane...

Hatimaye uchaguzi mkuu wa 2020 umekamilika na kutuletea matokeo ya kushangaza. Sio siri kuwa uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki wala haukuwa wa wazi. Ushahidi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya demokrasia ulikuwa mwingi na kila mahali. Hakika, watu wengi wameumizwa kwa yaliyofanyika.

Baada ya kutangazwa matokeo, viongozi wa vyama vya upinzani, hususan Chadema na ACT, walijitokeza hadharani kutangaza kutoyatambua matokeo. Hili ni jambo sahihi kwani hamna namna unaweza kuukubali uchafuzi ule uliobatizwa jina la uchaguzi.

Shida ipo katika hatua zilizotangazwa za kupambana na udhalimu na ujambazi uliofanyika dhidi ya demokrasia.

Vyama vya upinzani vimetangaza maandamano yaisyo na ukomo yatakayoanza kesho Jumatatu Novemba 2.

Tujiulize maswali mawili: Kwanza: je maandamano ni muhimu? Pili: Je maandamano yanawezekana na yataleta tija inayotegemewa katika muktadha wa Tanzania?

Nikianza na swali la kwanza, hakika maandamano ni muhimu, tena ni muhimu sana. Maandamao ni moja ya njia muhimu za kujieleza katika siasa za kidemokrasia, haki ambayo inatajwa hata kwenye katiba ya nchi (rejea uhuru wa kujieleza na kutoa maoni).

Kwa hiyo, katika hali ya kawaida, ilikuwa ni muhimu kuandamana kuelezea kutoridhishwa na uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika.

Hata hivyo, kuhusu swali la pili, kwamba, je maandamano yanawezekana na je yataleta tija? Jibu, bila shaka, ni hapana. Nina hoja tatu za msingi za kuamini maandamano hayataleta tija.

Hoja ya kwanza ni ukatili wa vyombo vya dola utakaopelekea watu wengi kuumizwa, iwapo watajitokeza. Uzoefu wa Zanzibar na maandamano yaliyowahi kuitishwa huko nyuma dhidi ya utawala wa awamu ya tano, yakiwemo yale ya UKUTA na yale ya Mange Kimambi, unaonesha kuwa hii ni serikali ya kikatili isiyojali kabisa utu na haki za binadamu.

Katika utawala wa serikali ya awamu hii, uhai wa binadamu hauna thamani hata kidogo. Watakuua na hawatajali. Kwa nini viongozi wa upinzani muwapeleke watu kwenye kifo hali mnaelewa kiwango cha ukatili wa serikali hii?

Tuseme, watu wameandamana na baadhi kadhaa wamekamatwa na kuwekwa ndani. Je, vyama hivi vilivyoitisha maandamano vina uwezo wa kwenda kuwatoa ndani kwa kuwawekea dhamana au itakuwa kila mtu na lwake? Naelewa kiuhakika kabisa kuwa wengi kati ya watakaojitokeza (kama kweli watajitokeza) ni vijana wadogo, maskini ambao huenda familia zao hazina mbele wala nyuma na zinawategemea katika kutafuta riziki. Je mmewafikiria hao wategemezi?

Ukweli ni kuwa, kuna idadi kubwa ya Watanzania wasioridhishwa na ukandamizaji wa demokrasia., lakini changamoto za kimaisha wanazokabiliana nazo ni kubwa mno kuwafanya wajali. Hivyo, ni wazi kuwa, watakaojitokeza kwa maandamano ni watu wachache sana, jambo ambalo litarahisha kazi ya vyombo vya dola ya kuwashughulikia.

Na baada ya kushughulikiwa kikatili, naamini vijana hao hawatarudia tena kuandamana. Jambo hili likitokea litaipa serikali dhalimu ya CCM ushindi wa kisaikolojia. Watasema na kutangaza duniani kote, ‘Aagh ni wakorofi wachache tu waliokuwa wakileta ukorofi.’

Ndugu viongozi wa upinzani kutoka vyama vya ACT na Chadema, jaribuni kuwalelewa watu mnaowaongoza, na tafadhalini msiwapitishe katika njia wasiyoimudu kwani wafuasi huenda wakaamua kuacha hata kuunga mkono mapambano ya kidemokrasia. Kuwafanya watu waandamane hivi sasa ni sawa na kukamua jipu lisiloiva.

Nini kifanyike? Mambo mawili ni muhimu sana. Kwanza, vyama viendelee kupaza sauti za kupinga uchafuzi wa demokrasia uliofanyika kwa kutumia vyombo mbalimbali ili kunyanyua uelewa miongoni mwa wananchi na hivyo kupata uungwaji mkono. Hoja isiwe chama kipi ni mahiri zaidi katika kuleta maendeleo bali ulinzi wa demokrasia yetu.

Pili, viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine wajaribu kushawishi jamii ya kimataifa kwanza kutotambua uchaguzi na matokeo yake na kisha kuibana serikali ya Magufuli irudie uchaguzi baada ya kufanya mabadiliko ya kisheria yanayokandamiza demokrasia.

Kwa kumalizia, ni vyema kwa vyama vya upinzani kujitathmini. Baada ya kufanyiwa dhulma walizofanyiwa, Je nini wanaweza kufanya ili vyama hivi viendelee kuheshimika na kukubalika mbele za wananchi?
Madikiteita huwa hawasikilizi maneno, ila mabomu. Definitely kufa ni lazima ili wengine wapone. Wakifa kama laki moja au zaidi dunia itaingilia kati na Tanzania ya haki itaundwa. Usiogope kura, kwani utaishi milele? Kwa hali ya sasa una tofauti gani na maiti?
 
Msitegemee huyo dictator uchwara atarudisha mtandao na huku mnataka kuandamana, tunzeni VPN Zenu vizuri. Na 2025 Anagombea tena tusipomfunga brake now.
 
Acha ni kafe tu hakuna shida ila sitakufa peke yangu
 
Wewe kaa nyumbani sisi tutaandamana!
 
Nchi nzima idadi ya polisi na wanajeshi sidhani kama inafika laki moja, Chadema peke yake ina wanachama wanazidi milioni 7, Utawazuaiaje?

Wanajeshi wanaweza kuzuia maeneo maalum katika nyakati maalum. Hawana uwezo wa kuzuia watu wa nchi nzima!

Na display yoyote ya nguvu kupita kiasi kwa raia itakuwa ni muendelezo wa kukusanya ushahidi wa kuwafikisha watu ICC

Pia raia wakishakuwa wengi wanao uwezo wa kuzuia au kuchelewesha polisi wasiwaharibie mipango yao, kwa mfano maaskari huwa wanategemea usafiri wa magari yao, nimeona kwenye nchi nyingine raia wanawachelewesha kwa kuziba hizo barabara kwa mawe mazito, au kuchoma matairi.

Kiufupi ni hekima kuwaacha wananchi waandamane, hasa wakishakuwa wengi la sivyo ni uwendawazimu kutumia bunduki dhidi ya maelfu ya raia, maana at the end of day, kuua raia wanaodai haki zao za kiraia siyo heshima kwa jeshi makini. Jeshi haliwezi kujisifu uhodari kwa kuua raia wa nchi husika ili kulinda genge la watu wachache wanaotaka madaraka kwa kuiba chaguzi!
 
Naisubiri
Serikali na tume ya uchaguzi imeziba Sana masikio TUNASEMA FUTEN UCHAGUZI HAMSIKII SASA NASEMA NA NAUNGA MKO MAANDAMANO YA AMANI YASIOKUA NA KIKOMO

kiongonzi mwenye uchungu na nchi yake lazima kutii bila shurti hisia za watu wake na Kama hawezi basi sio kiongonzi sahii,Sasa tz tuna kata ngapi na mtawezaje yazuia,ngoja tuone ,NARUDIA NAUNGA MAANDAMANO MKONO ,Kama kulia hacha tulie wote labda tutaheshimiana vizuri
Asiyesikia la mkuu..... Mguu mmoja utaokotwa mwenge mwingine ubungo, shauri yako. Mwisho mita kumi tu.
 
Nchi nzima idadi ya polisi na wanajeshi sidhani kama inafika laki moja, Chadema peke yake ina wanachama wanazidi milioni 7, Utawazuaiaje?

Wanajeshi wanaweza kuzuia maeneo maalum katika nyakati maalum. Hawana uwezo wa kuzuia watu wa nchi nzima!

Na display yoyote ya nguvu kupita kiasi kwa raia itakuwa ni muendelezo wa kukusanya ushahidi wa kuwafikisha watu ICC

Pia raia wakishakuwa wengi wanao uwezo wa kuzuia au kuchelewesha polisi wasiwaharibie mipango yao, kwa mfano maaskari huwa wanategemea usafiri wa magari yao, nimeona kwenye nchi nyingine raia wanawachelewesha kwa kuziba hizo barabara kwa mawe mazito, au kuchoma matairi.

Kiufupi ni hekima kuwaacha wananchi waandamane, hasa wakishakuwa wengi la sivyo ni uwendawazimu kutumia bunduki dhidi ya maelfu ya raia, maana at the end of day, kuua raia wanaodai haki zao za kiraia siyo heshima kwa jeshi makini. Jeshi haliwezi kujisifu uhodari kwa kuua raia wa nchi husika ili kulinda genge la watu wachache wanaotaka madaraka kwa kuiba chaguzi!
Punguani utawajua tu, chama cha saccos mpo 7M kutoka wapi?. Mbona hamkumpa Mbeligiji hizo kura mkamwacha aiue Chadema kwa kura 1,933,271 tu?.
 
Zitto kama ana vidhibiti vya kuchezewa rafu anaweza kwenda mahakamani.

Kabla hujaandamana jiulize;

1. Je, lengo lako ni kupindua serikali iliyoko madarakani? Kama ndio, je uko tayari kupambana na vyombo vilivyowekwa kisheria kuilinda serikali isipinduliwe? Je, uko tayari kukabiliana na kesi ya uhaini?

2. Nini unategemea kitatokea baada ya hayo maandamano? Kama ni uchaguzi mpya, je nani ataitisha huo uchaguzi na kwa mujibu wa sheria ipi? Kama ni tume mpya, je nani ataiunda na kwa kutumia sheria gani?

3. Je, una uhakika watu wote wanaokuja kuandamana wana lengo lilelile unalofikiria wewe kichwani? Hakuna mtu anayetaka kutumia maandamano hayo kufanya uhalifu? Iwapo watakuwepo wahalifu, je uko tayari kuwa sehemu ya watakaochukuliwa hatua ya uhalifu?
Mkuu mtu yeyote atakaesoma hili bandiko lako na akashindwa kukuelewa Basi jua huyo ana mapungufu makubwa Sana ya akili.

Niwakumbushe tu Watanzania wenzangu ikitokea Umewekwa kwenye tenga la polisi Zitto Wala lissu hawatakujua wewe Kama wewe zaidi ya kuendelea kulialia kuwa vijana wetu wamekamatwa.

Walikuwepo kina Mdude Leo hatupo nao Tena uraiani na familia zao zinaendela kuumia huku aliokuwa anawapambania wapo kuhamasisha raia wengine wakamatwe Kama yeye na familia zao ziendelee kusota kuwarejeshea uraini Kama inavyo sota familia yake.

N.B: Don't believe politicians.
 
Punguani utawajua tu, chama cha saccos mpo 7M kutoka wapi?. Mbona hamkumpa Mbeligiji hizo kura mkamwacha aiue Chadema kwa kura 1,933,271 tu?.

Sasa wewe unaleta figure zilizopikwa na TISS kwa kushirikiana na NEC kuwa ndo uhalisia?.

Cheki wizi wa mchana huu

Theme: mijizi haina makazi salama, duniani wala mbinguni.

Wewe ni mmoja wa hiyo mijamaa?

Kama jibu ni "ndiyo", basi hiyo ndiyo habari yenyewe!
Hahaha mijizi haiishi duniani, ni kama njaa ukishiba hujakaa Sawa hii.
 
Kama unatoka kwenda kwenye maandamano ya amani unajidanganya. Ukweli ni unaenda vitani, umejiandaa? Wenzako wamejiandaa na silaa zote za kivita.

Waliojiandaa kwa silaha kwenda vitani dhidi ya waandamanaji walio katika haki yao ya msingi ya kuonyesha mawazo na hisia zao tu, hawana jina zaidi ya kuwa kumbe si wezi tu bali ni majambazi.

Wacha tuone watatukamata, kutupiga au watatuuwa wangapi?

Acha tuone pia kiongozi wao hatufai kwa kiwango kipi.

Dunia itakuwapo pia kuona.

Wajue pia kuwa nao hawatabaki salama.
 
Msitegemee huyo dictator uchwara atarudisha mtandao na huku mnataka kuandamana, tunzeni VPN Zenu vizuri. Na 2025 Anagombea tena tusipomfunga brake now.

Wala si kuwa 2025 anagombea tena.

2025 anakwiba tena!
 
Hatimaye uchaguzi mkuu wa 2020 umekamilika na kutuletea matokeo ya kushangaza. Sio siri kuwa uchaguzi haukuwa huru, haukuwa wa haki wala haukuwa wa wazi. Ushahidi wa uhalifu uliofanywa dhidi ya demokrasia ulikuwa mwingi na kila mahali. Hakika, watu wengi wameumizwa kwa yaliyofanyika.

Baada ya kutangazwa matokeo, viongozi wa vyama vya upinzani, hususan Chadema na ACT, walijitokeza hadharani kutangaza kutoyatambua matokeo. Hili ni jambo sahihi kwani hamna namna unaweza kuukubali uchafuzi ule uliobatizwa jina la uchaguzi.

Shida ipo katika hatua zilizotangazwa za kupambana na udhalimu na ujambazi uliofanyika dhidi ya demokrasia.

Vyama vya upinzani vimetangaza maandamano yaisyo na ukomo yatakayoanza kesho Jumatatu Novemba 2.

Tujiulize maswali mawili: Kwanza: je maandamano ni muhimu? Pili: Je maandamano yanawezekana na yataleta tija inayotegemewa katika muktadha wa Tanzania?

Nikianza na swali la kwanza, hakika maandamano ni muhimu, tena ni muhimu sana. Maandamao ni moja ya njia muhimu za kujieleza katika siasa za kidemokrasia, haki ambayo inatajwa hata kwenye katiba ya nchi (rejea uhuru wa kujieleza na kutoa maoni).

Kwa hiyo, katika hali ya kawaida, ilikuwa ni muhimu kuandamana kuelezea kutoridhishwa na uchafuzi wa uchaguzi uliofanyika.

Hata hivyo, kuhusu swali la pili, kwamba, je maandamano yanawezekana na je yataleta tija? Jibu, bila shaka, ni hapana. Nina hoja tatu za msingi za kuamini maandamano hayataleta tija.

Hoja ya kwanza ni ukatili wa vyombo vya dola utakaopelekea watu wengi kuumizwa, iwapo watajitokeza. Uzoefu wa Zanzibar na maandamano yaliyowahi kuitishwa huko nyuma dhidi ya utawala wa awamu ya tano, yakiwemo yale ya UKUTA na yale ya Mange Kimambi, unaonesha kuwa hii ni serikali ya kikatili isiyojali kabisa utu na haki za binadamu.

Katika utawala wa serikali ya awamu hii, uhai wa binadamu hauna thamani hata kidogo. Watakuua na hawatajali. Kwa nini viongozi wa upinzani muwapeleke watu kwenye kifo hali mnaelewa kiwango cha ukatili wa serikali hii?

Tuseme, watu wameandamana na baadhi kadhaa wamekamatwa na kuwekwa ndani. Je, vyama hivi vilivyoitisha maandamano vina uwezo wa kwenda kuwatoa ndani kwa kuwawekea dhamana au itakuwa kila mtu na lwake? Naelewa kiuhakika kabisa kuwa wengi kati ya watakaojitokeza (kama kweli watajitokeza) ni vijana wadogo, maskini ambao huenda familia zao hazina mbele wala nyuma na zinawategemea katika kutafuta riziki. Je mmewafikiria hao wategemezi?

Ukweli ni kuwa, kuna idadi kubwa ya Watanzania wasioridhishwa na ukandamizaji wa demokrasia., lakini changamoto za kimaisha wanazokabiliana nazo ni kubwa mno kuwafanya wajali. Hivyo, ni wazi kuwa, watakaojitokeza kwa maandamano ni watu wachache sana, jambo ambalo litarahisha kazi ya vyombo vya dola ya kuwashughulikia.

Na baada ya kushughulikiwa kikatili, naamini vijana hao hawatarudia tena kuandamana. Jambo hili likitokea litaipa serikali dhalimu ya CCM ushindi wa kisaikolojia. Watasema na kutangaza duniani kote, ‘Aagh ni wakorofi wachache tu waliokuwa wakileta ukorofi.’

Ndugu viongozi wa upinzani kutoka vyama vya ACT na Chadema, jaribuni kuwalelewa watu mnaowaongoza, na tafadhalini msiwapitishe katika njia wasiyoimudu kwani wafuasi huenda wakaamua kuacha hata kuunga mkono mapambano ya kidemokrasia. Kuwafanya watu waandamane hivi sasa ni sawa na kukamua jipu lisiloiva.

Nini kifanyike? Mambo mawili ni muhimu sana. Kwanza, vyama viendelee kupaza sauti za kupinga uchafuzi wa demokrasia uliofanyika kwa kutumia vyombo mbalimbali ili kunyanyua uelewa miongoni mwa wananchi na hivyo kupata uungwaji mkono. Hoja isiwe chama kipi ni mahiri zaidi katika kuleta maendeleo bali ulinzi wa demokrasia yetu.

Pili, viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine wajaribu kushawishi jamii ya kimataifa kwanza kutotambua uchaguzi na matokeo yake na kisha kuibana serikali ya Magufuli irudie uchaguzi baada ya kufanya mabadiliko ya kisheria yanayokandamiza demokrasia.

Kwa kumalizia, ni vyema kwa vyama vya upinzani kujitathmini. Baada ya kufanyiwa dhulma walizofanyiwa, Je nini wanaweza kufanya ili vyama hivi viendelee kuheshimika na kukubalika mbele za wananchi?
Hiyo paragraph ya mwisho umeandika UJINGA yaani unataka kusema hivi vyama haviheshimiki? Kudai Haki hakuna njia moja hiyo ya maandamano ni mojawapo....wamekwambia wataandamana bila kikomo unadhani siku zote watakuwa barabarani?
 
Maandamano yasiyo na ukomo uwezo huo watanzania hawana, kwanza watakula wapi, nani atawaletea chakula? Vinginevyo itawezekana kama kuna mtu anagharamia maandamano hayo
Unadhani watu wote wanauhakika wakula kila siku?
 
Back
Top Bottom