Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Mfano wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno bado unaishi.. Ni ule mfano wa kugawa madini ya thamani ya Almasi na kubadilishana na kipande cha chupa na kujiona mjanja sana
Post isiwe ndefu sana
Tunagawa maliasili zetu kwa wageni kwa bei ya kutupa
Tunagawa bandari zetu zote
Tunagawa miundombinu getu yote
Tunagawa madini getu yote
Tunagawa ardhi yetu
Tunagawa sehemu za bahari
mito na maziwa
Tunagawa vitalu na vyanzo vya gesi nknk
Hawa wote tunaowagaia wana tabasamu pana usoni lakini rohoni ni wanyama wa kutisha
Hivi vyote tunavyogawa kwa bei chee ni sawa na kugawa uhai wetu.. Achilia mbali uhuru.. Uhai una thamani kubwa.. Na uhai haushuki bei
Maliasili zote, vitalu vyote na kila nilichotaja hakuna kinachoshuka thamani hata siku MOJA na vyote vimebeba uhai endelevu
Sasa hawa tuliowagaia wanatupa nini!? Tunapewa
Vitu vitu visivyo na uhai tupu...! Misaada mfu.. Zawadi mfu.. Vitu ambavyo haviongezeki thamani bali vinashuka thamani tangu siku ya kwanza..
Tunadhani tunapendwa sana.. Tunadhani ni ukwasi.. Kumbe tunachekwa na kuzomewa kwa nyuma
Tunajaziwa machuma yaliyopakwa rangi na kutiwa nakshi mbalimbali
Tunabandikiwa picha zetu mpaka kwenye matambara.. Kila kitu, kila tukio, kila kusanyiko ni mapambio ya picha zetu na majina
Badala ya kuwa raha sasa ni karaha
Badala ya kuwa shangwe sasa ni chukizo
Badala ya kuwa pambo sasa ni uchafu
Mnyange anayejiamini huwa na mapambo machache.. Mnyange asiyejiamini hujipodoa mpaka anachukiza na kutisha...
Tumeuza uhai... Tukazawadiwa wafu..!
Mfano wa Mchonga bado unaishi...
Tanganyika...!