Mgogoro na kashfa ya sukari inayoendelea nchini iliyopelekea kufukuzwa bungeni kwa Mbunge Mpina tayari tumemsikia mpina, tumesikia maelezo ya bashe, tumesikia maelezo ya kamati ya bunge, tumesikia maelezo ya spika tulia na tumewasikia wazalishaji wa sukari.
Kama taifa tumeelewa nini Mpina ameonewa? Bashe yuko sahihi? Tulia yuko sahihi? Kamati iko sahihi? au wazalishaji wako sahihi?
Bashe yupo sahihi kwa asilimia zote.
Ni yeye peke yakje ndiye aliyefanya maamuzi ya kuliokowa jahazi kwa kuagiza sukari kwa haraka na kuweza kushusha bei ya sukari.
Wazee wa sukari walinishangza waliposema wamekosa meli ya kupakilia sukari kutoka Brazil.
Cha kushangaza ikiwa wao ni magwiji wa sukari kama waliuvyojitapa, vipi 'wauza vocha" waweze kupata meli na kuingiza sukari kwa haraka, wao washindwqe?
Walitudanganya sana katika maelezo yao. Watanzania tunachotaka ni sukari tena ya bei nafuu. Walikuwa wapi siku zoite mpaka sukari inafikia 10,000 kilo?
Maelezo ya Tulia, yalitulia, alituhakikishia bungeni kuwa Tanzania sukari ni bei ya juu kuliko nchi zinazotuzunguka kwa viwango vya kusimumuwa.
Wazee wa sukari na mpina hawakuliona hilo? Na ujanja wao wote wa sukari.
Heko kwa Bashe na heko kwa kuvunja monopoly yao, sasa au wazalishe au wasizalishe bohari za kuhifadhi chakula zitajaza sukari na wataagiza waonavyo wao sahihi ikibidi.
Binafsi nampongeza sana Bashe.
Mpina wa kuhurumiwa tu, kwa usongo wake wa kukosa uwaziri kuwa na fitina za kila siku bungeni kama vile mawaziri ndiyo walimkosesha hiyo kazi.