Wizara ya Maji
Govt Institution
- Oct 2, 2024
- 34
- 20
Taasisi za Sekta ya Maji zimetakiwa kuwa na mifumo ya dharura itakayo saidia kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Nino kama ilivyo tabiriwa na Mamlaka ya Hali Hewa (TMA).
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Andrew Mathew (Mb) ametoa angalizo hilo akipokea taarifa ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mkoani Manyara, leo Oktoba 06, 2026.
Amesisitiza umuhimu wa kutumika kwa Vitengo vya Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma kufikisha taarifa mbalimbali na mrejesho wa wananchi ikiwemo suala la utunzaji na matumizi sahihi ya mifumo ya majitaka na miundombinu ya majisafi , pamoja na kutunza vyanzo vya maji.