Tumjadili huyu Mstaafu hapa wakuu tuone ana akili timamu au sio mzima

Alipopata pesa alitakiwa awashirikishe wanae kwanza au angeacha kugawa ovyo angemalizia ujenzi kisha angetoa sadaka kidogo
Hao wakipata hela huwa hawashikiki na huezi kumweleza kitu mkaelewana hadi pesa iishe ndo akili inatulia.

Akiwa ni mwalimu basi uo mcheche wake ongezea *2. ukimshika kichwani utasikia acha mguu wangu
 
Alipopata pesa alitakiwa awashirikishe wanae kwanza au angeacha kugawa ovyo angemalizia ujenzi kisha angetoa sadaka kidogo
Pesa yangu mwenyewe niwashirikishe watoto wangu ili iweje? Walinisaidia nini kuipata katka utumishi wangu?
 
Another one from mstaafu.
 
Mpwayungu Village huyu mstaafu alikuwa mwalimu au?
 
Huyu mama jirani mtaa wa pili (Arusha) yeye na mume wake walikuwa walimu. Na wote walistasfu kwa wakati mmoja na hata kwenye kupokea mafao yao walichukuwa kwa wakati.

Mama alipopokea kiinua mgongo yeye moja kwa moja akapeleka kupanda mbegu kwa wanaomuita nabii mkuu, mume wake ni mzaliwa wa Arushana alikuwa ana shamba la urithi na alikuwa amejenga nyumba ya familia.

Kwa kuwa anajua yeye na mke wake wana akamwuliza mke wake ana malengo gani na hiyo pesa! kumbe mke keshapeleka shambani na kupanda mbegu.. Mke amejiuma uma wee mwishoni akasema ukweli kuwa amependa mbegu kwa nabii mkuu pesa yote 63+ million. Baada ya tafakuri mume wake akamfukuza kwani alitegemea hiyo pesa kama wangezichanga zingewasaidia kwenye mambo mbalimbali.

Mume kwa yale mafao yake amefanikiwa kujenga vyumba kadhaa vya kupanga (biashara na makazi). Ameboresha nyumba ya familia na kuwekeza kwenye ufugaji wango'mbe na ukulima.

Naamini moja ya wahanga wakubwa wa kutapeliwa na hizi imani tulizoletewa na wageni ni wanawake na walimu hususani jinsia ya kike ... Mwanafunzi anaweza buruta mkia miaka yote hakuna anachoelewa darasani hadi walimu wamemchoka, cha ajabu yule yuke kilaza kwenye kutafuta anaweza jikuta anaangukia kuwa nabii, mtume, au mchungaji na akaja kuwatapeli walimu wanaofundisha madaktari na marubani.

Dunia haina usawa, kila mmoja ale kulingana na urefu wa kamba yame.🙅‍♂️
 
Watoto ni kwa ajili ya kupata ushauri siyo kugawana nao pesa yake.
Amekosa ushauri amepotea njia anarudi kuwa mzigo kwa watoto wake.
 
Mambo ni mengi sana.

Moyo unaficha mambo mengi.
 

Maisha ya mtanzania magumu sana. Tunashika hela nyingi kwa mkupuo tukishafika uzeeni. Hapo ukishazishika unataka kutimiza ndoto zako zote ambazo hazikutimia kipindi unahangaika. Ujenge nyumba, ununue gari, usaidie ndugu, utoe sadaka, uanzishe biashara…etc kufumba na kufumbua hakuna kinachobakia.
 
Haya mambo ya wastaafu magumu sana. ile ela ni kama imelaaniwa hivi. Kuna mstaafu alipata ela zake na za mumewe aliyekuwa amefariki muda mchache baada ya kustaafu, yule mama leo hii ukimwuuliza leo hii kapeleka wapi au kafanyia nini ile ela yote unakuta hakuna majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…