Ni dhahiri kwamba uongozi wa Magufuli umetuumiza sana watanzania wote wa rika zote na kada zote. Kwanza kuna watu wametekwa na kuuawa na serikali haijawahi eleza chochote na ushahidi wa hawa watu kuuawa wananchi tunao, Ben sanane ametekwa na kupotezwa mpaka Leo wazazi wake hawakuweza kupata hata mfupa ili wazike na kupumzisha nafsi zao, roho zao zipo juu juu, utekaji huu na uuaji wa namna hii hatujawahi kuushuhudia katika awamu zote zilizopita na wala huwezi msikia Magufuli akiongelea hilo la utekaji na uuaji, sasa tumchague tena Magufuli wa nini?
Azory Gwanda amefuatwa na waliojitambulisha ni Polisi na wamempoteza, tena anafuatwa mbele ya mkewe na mpaka sasa si familia yake ipate hata kidole angalau wazike na roho zao zitulie, huyu ni mwandishi wa habari amepotezwa na kuuawa lakini huwezi kuona hata Magufuli kuliongelea hivyo, sasa tumchague wa nini?
Kuna watu wengi sana wameuawa na kupotezwa, wengine wamepewa kesi za kubambikiwa na wanaozea gerezani, Mdude Chadema amebambikwa kesi ya dawa za kulevya ili anyamazishwe, Tito na mwenzake wamebambikwa kesi ya uhujumu uchumi na wanaozea gerezani, sasa tumchague Magufuli tena Kwa lipi?
Wafanyakazi miaka 5 hawajaongezwa mishahara, mbaya zaidi wananyanyaswa makazini, achaguliwe Magufuli Kwa lipi? Wafanyabiashara wamefilisiwa na wengine wamenyanyaswa na kuporwa Mali zao Kwa lazima na utawala wa Chuma wa Magufuli, sasa achaguliwe Kwa lipi?
Wahitimu wa kada mbalimbali nao pia wamekumbwa na uhaba wa ajira na wanaendelea kutaabika mtaani bila matumaini ya ajira, sasa achaguliwe tena Kwa lipi? Wananchi wa kawaida wanaishi katika umasikini uliopindukia baadhi ya familia zinapata mlo mmoja kwa siku na zingine zimekosa kabisa, achaguliwe Magufuli tena Kwa lipi?
Wananchi wa vyama vya upinzani wametukanwa na kutishiwa kuuliwa na vikundi vya CCMMara Kwa Mara UVCCM imekuwa ikihubiri machafuko na hakuna hata aliyewakaripia si polisi wala Magufuli, sasa tumchague wa nini tena. Maovu ni mengi sana yaliyofanywa na Magufuli katika utawala wake, tumchague tena wa nini?
Ni wakati sahihi wa kumuweka pembeni Magufuli na maovu yake yote yaliyo dhahiri na tuambatane na Lissu ambaye amepigwa risasi na utawala wa Magufuli, yawezekana hata Mipango ya kupigwa risasi Lissu ilipangwa na Magufuli na genge lake,tumkatae Magufuli na uovu wake.
Niliyosema yote ni kweli na hiki ni kipindi cha kampeni hivyo mtuache tuzungumze kikicho cha kweli. Ni mengi sana maovu ametutendea Magufuli kuliko mazuri,tunkataeni na tulinde kura zetu Kwa damu na jasho ili Magufuli asiibe kura zetu.
Swelana.