Uchaguzi 2020 Tumkatae Magufuli, tumkubali Lissu

Uchaguzi 2020 Tumkatae Magufuli, tumkubali Lissu

Rais wetu kipenzi JPM ametuvusha kwenye vikwazo vikubwa kama kurekebisha mikataba ya madini,janga la Civid-19,na mengine meengi.
Embu tupe mfano japo mmoja tu Lissu akiwa mbunge alifanya nini kwenye jimbo lake angalau kiwe kigezo cha kumpa kura?
 
HICHO UNACHO JARIBU KUABARISHA WANAJUMUIYA YA JAMII FORUM NI BLACK PROPAGANDA TU. KWANZA TIANZE NAWEWE KUKUKATAA.

unapo zungumzia wafanyakazi kutoongezewa mshahara kwanza wanakushangaa sana
Swala la mshahara hili ni siri kati ya mwajiri na muajiriwa sasa wewe ulitaka wakutangazie ili iweje? Usikurupuke

Swala la kutekwa watu, ndg yangu kila nchi ina destination yake ndio maana tuna mfumo unao isimamia nchi
Swala la kutekwa alijaanza kipindi hiki cha awamu ya tano! Bali tangia awamu ya kwanza watu waliwekwa vizuizini wale walio ashilia kuaribu Destiny ya nchi, hili taifa limetoka mbali sana na limepitia magumu mengi pasipo kuwa na mifumo inayo monitor kila kitu leo tusingekuwa tuna bwabwaja humu Jamii forum.

Nikupe mfano tu, kipindi cha masih(yesu) yohana mbatizaji aliuwawa lakini taarifa ta yeye kukamatwa zilimfikia Yesu kwa uwezo wake Yesu alitarajiwa angefanya vyovyote kuokoa maisha Ya yohana lakini Yesu alikaa komya hatimae Yohana alikatwa kichwa. Wana thiolojia wanasema ilipaswa Destiny itimie,
Pia hata kwake yeye YESU pindi anateswa msalabani alilia kwa sauti kuu na uchungu mkuu lakini Mbingu zilikaa kimya Lakini uwezo wa kumuuokoa ulikuwepo hiyo ndio tunaita hatima (Destiny) lazima itimie

Ndio jinsi ilivyo katika ulinzi wa taifa lolote duniani kila taifa lina hatima yake hivyo lazima ilindwe kwa namna yoyote hile.

Umezungumzia ajira.
Itatuchukua karine watanzania kuona thamani ya natural resources tulizo nazo
Leo hii inchi aridhiyenye rutuba kila ukisafiri unapita mapori mengi tuna maziwa na bahari tuna maeneo mengi ya ufugaji hii nizawadi tulio zawadiwa toka enzi lakini leo hi tunataka tuishi kutokana na professional zetu badala ya kuyaishi maisha yetu
Tunalalama kuwa atuna ajira kweli?
Embu fikilia leo hi mfanyakazi aliyeko kwenye ajira anategemea kusitafu above 60 yrs sasa wewe unae maliza chuo leo hesabu miaka 60 ijayo ndio kutakuwa na nafasi endapo kifo kikiwa =0

Ukiwa wewe nikija unalalama ajira basi hata elimu uliyo nayo bado haijakusaidia kujitambua
Mimi nina masters tena ya Bsc in Chemistry lakini nilichagua kuwa mvuvi wasamaki karibu Gosiba (kisiwa ndani ya ziwa victoria) uone vijana wenzako tulivyo na ajira
Tunaishi ktk maisha sio kuishi ktk professional.

Hitimisho langu nyakati hizi za vizazi vyenye kukalili maisha na kwanamna nchi yetu ilipo fikia kwasasa MAGUFULI ni chaguo sahihi
Mtanyooka tu mnaishi kimamama hata bibulia inaesema asiyefanya kazi na asile
Wewe unajua kazi nikuajiriwa tu ofisini.
CHUMA MAGUFULI MITANO TENA.
 
1599206375250.png
 
Tunampigia kura Mgombea wa CCM anayetokana na Taasisi imara yenye kuheshimika Afrika na Dunia nzima,

Hatumpigii kura Mgombea wa Saccos inayotafuta fedha kukuza mtaji wake.
Kama unampigia dikteta ni wewe lkn wananchi wenye uelewa hatumtaki magufuli,nasema hatumtaki,kama kweli mnampenda dikteta iteni mikutano yenu bila wasanii tuone kama mtapata hata watu 11 kwenye mikutano yenu.
 


2015 aliahidi kuboresha haki za mfanya kazi na kutoza kodi zisizoumiza wafanya biashara. Hakuna lililotekelezeka.
 
Tundu Lissu tuvushe, wewe ndiyo tegemeo letu kutoka katika mikono ya mkoloni mweusi anaetawala ki mabavu CCM

Kwa ushidi atakaopata magufufuli tutakua tumepiga beberu Amsterdam na Smith na kibaraka wao, kwa mara ya pili tunachapa beberu,
Mara ya kwanza ni mwalimu JK Nyerere.
 
Anachonikera Magufuli ni kujiona yeye ni demi god ana akili kuliko mtu yeyote nchi hii kitu ambacho sio kweli.
Mimi naamini ana uwezo wa kawaida tu.
 
Ukifanya utafiti kidogo tu utajua Magufuli anakubalika na watu wengi, na ni idadi ndogo mno isiyomkubali.

Atashinda tena, na wale wanaosema atashindwa wanajua fika kuwa atashinda. Ukiukubali ukweli huo utakuwa mtu huru.
 
ungelizijua siasa zaidi ya unavozishabikia hapa sidhani kama ungefungua hilo bakauli lako dhidi ya magufuli, mabeberu wenyewe washachanganyikiwa dhidi yake hata huyo shoga wenu lisu anaujua ukweli, anajua kabisa hadi chanzo cha yeye kupgwa risasi ni kukosa uzalendo dhidi ya taifa, na naamini hua analijutia sana kosa lake japo nyie mazuzu hamuwezi elewa.


uku kuna watu wasiojulikana upande mwingine kuna watu wanataka kumpiga mawe! yaani sjui ataishi wap
 
Lisu atapigiwa kura na wahuni wenzie!

Sisi watanzania hatiwezi kumchagua mtu atuongozee nchi kwa matakwa ya beberu wake Amsterdam.
 
Ni dhahiri kwamba uongozi wa Magufuli umetuumiza sana watanzania wote wa rika zote na kada zote. Kwanza kuna watu wametekwa na kuuawa na serikali haijawahi eleza chochote na ushahidi wa hawa watu kuuawa wananchi tunao, Ben sanane ametekwa na kupotezwa mpaka Leo wazazi wake hawakuweza kupata hata mfupa ili wazike na kupumzisha nafsi zao, roho zao zipo juu juu, utekaji huu na uuaji wa namna hii hatujawahi kuushuhudia katika awamu zote zilizopita na wala huwezi msikia Magufuli akiongelea hilo la utekaji na uuaji, sasa tumchague tena Magufuli wa nini?

Azory Gwanda amefuatwa na waliojitambulisha ni Polisi na wamempoteza, tena anafuatwa mbele ya mkewe na mpaka sasa si familia yake ipate hata kidole angalau wazike na roho zao zitulie, huyu ni mwandishi wa habari amepotezwa na kuuawa lakini huwezi kuona hata Magufuli kuliongelea hivyo, sasa tumchague wa nini?

Kuna watu wengi sana wameuawa na kupotezwa, wengine wamepewa kesi za kubambikiwa na wanaozea gerezani, Mdude Chadema amebambikwa kesi ya dawa za kulevya ili anyamazishwe, Tito na mwenzake wamebambikwa kesi ya uhujumu uchumi na wanaozea gerezani, sasa tumchague Magufuli tena Kwa lipi?

Wafanyakazi miaka 5 hawajaongezwa mishahara, mbaya zaidi wananyanyaswa makazini, achaguliwe Magufuli Kwa lipi? Wafanyabiashara wamefilisiwa na wengine wamenyanyaswa na kuporwa Mali zao Kwa lazima na utawala wa Chuma wa Magufuli, sasa achaguliwe Kwa lipi?

Wahitimu wa kada mbalimbali nao pia wamekumbwa na uhaba wa ajira na wanaendelea kutaabika mtaani bila matumaini ya ajira, sasa achaguliwe tena Kwa lipi? Wananchi wa kawaida wanaishi katika umasikini uliopindukia baadhi ya familia zinapata mlo mmoja kwa siku na zingine zimekosa kabisa, achaguliwe Magufuli tena Kwa lipi?

Wananchi wa vyama vya upinzani wametukanwa na kutishiwa kuuliwa na vikundi vya CCMMara Kwa Mara UVCCM imekuwa ikihubiri machafuko na hakuna hata aliyewakaripia si polisi wala Magufuli, sasa tumchague wa nini tena. Maovu ni mengi sana yaliyofanywa na Magufuli katika utawala wake, tumchague tena wa nini?

Ni wakati sahihi wa kumuweka pembeni Magufuli na maovu yake yote yaliyo dhahiri na tuambatane na Lissu ambaye amepigwa risasi na utawala wa Magufuli, yawezekana hata Mipango ya kupigwa risasi Lissu ilipangwa na Magufuli na genge lake,tumkatae Magufuli na uovu wake.

Niliyosema yote ni kweli na hiki ni kipindi cha kampeni hivyo mtuache tuzungumze kikicho cha kweli. Ni mengi sana maovu ametutendea Magufuli kuliko mazuri,tunkataeni na tulinde kura zetu Kwa damu na jasho ili Magufuli asiibe kura zetu.

Swelana.
Wakandarasi tumeitwa wezi , wapigaji, tumenyinwa fursa ya kupata kazi, baada ya kuanzisha utaratibu wa kijima wa force account ,tumebaguliwa Sana project zote wanapewa jkt, tba,

walivyo na roho mbaya na chuki Wameagiza mashirika yote ya umma yaanzishe kitengo Cha ukandarasi na consultancy. Nhc, tannesco

alafu wanashinikiza board zote za usimamizi kwenye majenzi Crb, ERB, Aqrb,zikusanye mapato ya usajili na Ada za members ziende hazina,

Secta ya ujenzi imekufa Kifo kitakatifu,
makampuni hayakui, makampuni mapya hayaanzishwi Tena

Magufuli kaua makampuni ya wazawa yamebaki ya wachina na wahindi,

Ili wazawaa tuwe masikini ili tutawaliwe na wapuuzi
 
Magufuli na CCM ya Magufuli, na MaCCM yote yalishakataliwa Duniani na Mbinguni,
Tanganyika na Zanzibar.
 
Ccm Wana kauli mbiu yao toka 2016" wafanyakazi,wafanyakazi, wakulima waliokuwWanaishi Kama malaika waishi Kama mashetani"

Wamefanikiwa kuwafanya watz kuishi kama mashetani,

tumeona wafanyabiashara wakubwa wakuiuwawa, kufilisiwa, kutekwa, kuporwa fedha zao, na kufinguliwa mashtaka ya kubumba

Tuikatae ccm
 
Tunamchagua JPM na tunaichagua CCM acha porojo zako usitupangie cha kufanya
 
Kura yangu nampa lisu 2020 make 2015 nilibugi sana mpka sasa najiraum kuipigia kura ccm 2015 saizi sifanyi kosa tena ni yeye ndio nampa kura yangu
 
alafu nyie msozijua siasa sijui kwa nini mnaruhusiwa kupost haya mashudu yenu, hivi unayajua madhara ya mtu aliekosa uzalendo na kutumika na maadui dhidi ya taifa lake kwa maslahi yake?
je kama amekosa uzalendo kwa taifa lake ni ipi thamani yake?
amani na thamani ya taifa ni bora kuliko mtu yeyote anaekosa uzalendo dhidi ya taifa lake.

haya mambo bado ni mageni sana afrika kwa wenzetu ukitumika na maadui dhidi ya taifa lako kifuatacho ni kuuawa, bora hata hapa kwetu watu wanaonywa kwanza japo wanajitia ujuaji hadi yanawapata yakuwafika.
Prove
 
Back
Top Bottom