Tumlaumu nani kifo cha CCM: Wazee wa chama, marais au ubinafsishaji mkubwa wa nchi kwa chama?

Tumlaumu nani kifo cha CCM: Wazee wa chama, marais au ubinafsishaji mkubwa wa nchi kwa chama?

Kansa sugu na uwepo wa vimelea vijulikanvyo kwa jina la kitaalamu "Poli Pole" ndo sababu kuu ya kifo cha marehemu Bwana mezameza
 
Nakisubiria kwa hamu kubwa sana hiki kifo, na mimi pia nitachinja ng'ombe tena lile duma zagamba.
 
Chama kimejikuta kina hisia kuwa kinaumiliki wa nchi. Kimejisahau kabisa.
 
Ningependa kujua nini maoni yakeo juu ya kifo cha hiki chama cha kisiasa hapa Tanzania. Unahisi nini kimepelekea kifo chake na je unahisi walikitegemea tayari na walishaanzisha vyama vya kukumbilia baada ya hiki KIFO au wataamua kubadilisha falsafa ya chama ili kujaribu kurudi kwa wananchi miaka hiyo ijayo.

Nini unawaza ni sababu kuu ya kifo cha CCM:
  1. Wazee wa chama hawakuwa wakifanya kazi zao maalumu bali walikuwa wakijijali wao, familia zao na mali zao walizochuma kipindi cha madaraka yao?
  2. Marais wenyewe, kama wengi tunavyoamini nchi ya Tanzania inaongozwa na raisi pekee mambo mengine ni maigizo tu. Lawama zote ziende kwake.?
  3. Ubinafsishaji mkubwa wa kila kitu kwenye nchi kwa chama: Bunge, Mahakama, Rasilimali, Uchaguzi na ndoto za watanzania (huwezi fanya lolote mpaka uwe na kadi ya chama au ujipendekeze kwa chama)
  4. Muda tu umefika, watu wanataka kuona sura mpya na namna wengine wanaweza kuwaongoza.
  5. Mengine...
Tuipemaua ccm yenyewe kwa kufariki dunia Tanzania
 
Back
Top Bottom