Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,862
- 6,438
Wasalaam,
Katika wale wote tunaofuata Iman ya Mungu mmoja ama mafundisho yanayofanana na kutofautiana katika sehemu chache
Haswa katika dini kuu Uislam ,Ukristo na Uyahudi.
Katika pande zote hizo tunaamini jambo moja juu ya huyu mungu wetu ya kwamba yeye ndiye mjuzi wa yote yaliyotekea na yajayo.
Na kuna ule msemo maarufu sana wa wazee wetu wa zamani eti "MOLA NDIYE MPANGAJI"
Sidhani kama walikosea wanadamu wote asilimia 100% waaminio uwepo na muongozo wa huyu mungu wanaamini kuwa mola ndiye anayepanga mambo yote yanatokea katika dunia.
Wametutoka vigogo kadhaa msimu huu, Maalim Seif , Mzee Pombe Magufuli na kauli kama "YOTE NI MIPANGO YA MUNGU" zilishamiri sana katika vinywa vya wanaadamu vivyo hivyo hili ni jambo Endelevu na Desturi yetu kwamba likitokea jambo lolote liwe tata au la kawaida, kubwa au dogo basi Heshma ya Utendaji yote inabaki kwa Mungu huyu mungu mkuu
kwamba yeye ndiye mpangaji wa yote
Tunaamini
Kila Jambo hupangwa na Mungu mwenyewe.
Tukirejelea nyuma kidogo katika tukio moja , ambalo kidogo litanifanya niingie katika kundi la mapungufu kiuandishi baada ya kutumia kiambatanishi kimoja yaani kisa kutoka Upande mmoja wa dini ('Islam') hii ni kutokana na kukosa masimulizi ya kisa hiki katika upande wa dini zingine(ukristo) tofauti na Uislamu. Lakini hii haipangui lengo la Mada yetu kuu, inalenga pale pale katika kung'amua sintofahamu hii. katika pande zote. Si tunaamini Mungu ndiye mpangaji wa Yote.
Hii ni Hadithi ya mtume Muhammad (S.A.W) akielezea jinsi Nabii Musa yule aliyesumbuana na Farao kule Misri alivyokutana na Nabii Adam baba wa kizazi cha Wanaadamu Ulimwenguni.
Inasimuliwa
Nabii Muhammad (ﷺ) alisema,
"Adam na Musa walibishana wao kwa wao.
Musa akamwambia Adam.
" Ewe Adam! Wewe ni kipi kilikufanya ufukuzwe katika bustani ya Mwenyezi Mungu, kwanini ulivunja miadi ya mwenyezimungu (ukala tunda na mkeo ukafukuzwa peponi)"
Adam akamjibu
"Mwenyezimungu alikuwa ameiandika katika hatima yangu miaka kabla ya kuumbwa kwangu.
Mtume Muhammad anaelezea ya kuwa Adamu alimjibu Musa huku akimcheka ya kwamba kila kitu kilikuwa kimeshaandikwa kabla ya yeye kuumbwa.
Masimulizi haya yanaeleza namna Nabii Mussa alivyomuomba Mola wake amkutanishe na Nabii Adamu ili apate kumuuliza kilichomsibu ikafikia hatua ya yeye, kumuasi mola wake wake kwa kumfuata Ibilisi naye Adamu akajikuta yu Uchi kufuatia kula tunda.
Inaelezwa Mussa alipokutanishwa tu na Adamu alianza kumshushia lawama yakwamba kwanini alikula tunda mpaka akafukuzwa kule Eden akasababisha Wanaadamu waje kuishi mahali na sehemu zenye shida nyingi Duniani
Nabii adamu anamjibu nabii Musa ya kuwa "Hilo lilishaandikwa katika hatma za nabii Adam ya kwamba lazima litatokea.
Kama ni hivyo Kauli ya kusema Mola ni mpangaji wa yote haina Kipingamizi mara nyingi
Na hapa inatuonyesha yakwamba yote ilikuwa mipango ya Mungu ili mwanadamu apate kumcha/kumtii yeye, na wala asifate kwingineko.
SWALI.
Kwanini tunamlaumu Adamu na Shetani Ilhali ilikuwa ni mipango ya Mwenyezimungu?
i stand to be corrected
Na mwenyezimungu Mjuzi wa Yote
DaVinci XV