Tumlaumu Nyoka au Adam na Eva?

Aisee kweli sema ni zoezi zito
 
Kwanza nyoka hana kosa mungu wa biblia na qurani ndo mwenye makosa. Baada ya nyoka kutuona tukitembea uchi kama hayawani akatuonea huruma sana ndipo akampa eva maarifa kwani adamu kichwa yake alikuwa haweZi kupokea knowledge.

Baada ya kula tunda wakapata akili kuwa wako uchi ndipo wakajistiri tupu zao kwa majani. Swali langu. kama adamu kaubwa mfano wa mungu kwanini mungu alikuwa akifurahi adamu kutembea uchi bustanini? Wewe utafurahi kumuona kichaa akitembea uchi? Hata kama huna cha kumsaidia nafsi yako itaona hiki sio kitu kizuri na pengine utamwonea huruma kichaa huyo.

Kwanini mungu aliona ni sawa eva kutembea uchi bustanini. Alikuwa anawafanyanini wakiwa uchi hapo mpaka nyoka wa watu akawaonea huruma na kuwapa elimu ya maarifa ya kujitambua? Kumbuka walikuwa hawana akili ya kujua zuri na baya au mema na mabaya Chochote wakifanyiwa waliona ni sawa.

Na kwanini mungu alivyoona adam ana akili ndo akampa nguo. Swali kama yeye mungu wq bible nguo alikuwa nazo siku zote kwanini hakumpa adamu na eva bali aliamua kuwacha uchi hadi nyoka alipoona hii sio sawa?

Source kitabu cha mwanzo.
 
Bado nachunguza...kwa nini raia wengi kwenye mijadala kama hii wanapenda kukazia mawazo yao kwa mistari michache ya biblia tena iwe ni mpangani au Islamic!! Why?
 
Bado nachunguza...kwa nini raia wengi kwenye mijadala kama hii wanapenda kukazia mawazo yao kwa mistari michache ya biblia tena iwe ni mpangani au Islamic!! Why?
Bado sijakung'amua mkuu
 
Irudiweee [emoji23][emoji23] huenda Hawa akawa anajielewa this time!
Anyway hii mijadala inavuruga sana akili
 
Wote wanapaswa kulaumiwa.
 
Anayesema Masimulizi ya katika biblia au Quran hayana maana, ni mvivu wa kufikiri sawa sawa.
 
Katika uelewa wa leo, haingii akilini kwamba Nyoka anaweza kumzidi binadamu.

Ndio, binadamu ana cha kujifunza kutoka kwa nyoka ili kuwa bora zaidi.

Simulizi hilo la nyoka na Adamu na Hawa linataka kuangalia vitu vingi.

Aidha, sio sahihi kwamba Mungu anapanga kila kitu kinachofanyika hapa duniani isipokuwa kazi za kiakili.
 
Mjadala kama huu hauwezi kuwa na conclusion.
 
 
nasemaje wote swani tu
 
Wote wanapaswa kulaumiwa, nyoka kwa kukubali kutumiwa na lucifa, na Binadamu kwa kushindwa kufuata maelekezo ya muumba wake na kukubali kufuata maelekezo ya lucifa.
 
Lawama ni dhana dhaifu,katika hili fumbo kuna fundisho.Tunatakiwa tufumbue hili fumbo ili tukue (grow).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…