Tumpe Faraja Rais Samia kwa namna anavyofanya kazi bila kupumzika wala kukaa kwa ajili yetu Watanzania

Ningekua naomba Kazi ngumu kama anayofanya RAIS wetu na viongozi wengine wakuu hasa wa kisiasa, mtu angejaribu kuniibia Kura nisingehangaika Naye na wala nisingethubutu kuiba au kushawishi nipewe Kura nisizostahili...kwa sababu ningekuwa nasukumwa na dhamira ya kuwatumikia wananchi, but kama kuna shida Sana kwenye uongozi kama wanavyotuambia ni Kazi ngumu, why watu wa bleed ili mimi ni lead tena kwa kubleed!?
 
Nape ,makamba ,ridhiwani,Kenani,na wanaolamba asali wampe Mapenzi

Sisi wengine hapanaaa

Anayestahili Mapenzi ya kweli ya watanzania ni JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI Ndio mzalendo wa kweli.

Na aliyefanya kazi kubwa katika Taifa hili.

Swali kwako moja niambie mradi wenye maslahi kwa Taifa letu alilolianzisha Mama huyuu. Zaidi ya kuhudumia miradi ya Mzalendi wa kweli JPM
 
Umejaa ujinga. Nani kakueleza kukaa na tbc mgongoni mwako ndio utendaji kazi. Huko ni kutafuta fame tuu na kuonesha umma unafanya kazi.
Hapana Mambo afanyayo mh Rais yanaonekana wazi, Nenda katika Elimu, Afya, Maji, Miundombinu, umeme ,kilimo, kwote huko utakuta juhudi za mh Rais katika kumrahisishia mwananchi maisha yake
 
Nape ,makamba ,ridhiwani,Kenani,na wanaolamba asali wampe Mapenzi

Sisi wengine hapanaaa
Kila mtanzania ameguswa na utendaji wa mh Rais maana hakuna secta iliyobachwa nyuma, asipokugusa kwenye Elimu utaguswa katika Afya,maji,umeme, Miundombinu, kilimo n,k maana mama amefanya na anaendelea kufanya uwekezaji wa pesa za kutosha ili kutatua kero mbalimbali
 
Bila kuremba wala kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, Rais wetu Mama Samia anafanya kazi na inaonekana.
Sina mashaka wala wasiwasi tutaenda naye hadi 2030, Mungu azidi kumlinda.
 
Ni mama kwa watoto wake, kwa Mimi binafsi ni Rais na nitampima kwa nafasi hiyo na Wala siyo za uajuza Wala uchui.
Rais anapaswa kupimwa kwendana na outcomes anazo-generate. Apongezwe kwa kutopumzika kwani aliomba kazi ya kulala??
Watanzania tuache kujipendekeza pendekeza bila mambo ya msingi yasiyokuwa na kichwa Wala miguu.
 
Kama umelamba asali endelea kulamba tuu mkuuu.

Kipindi cha MZALENDO WA KWELI KILA MTU ALIULAMBA


MAFUTA BEI CHEE,ELIMU ,MIUNDO MBINU,KAZINI TUNAHESHIMIANA,KODI YA MISHAHARA ALISHUSHA HATA MTUMISHI WA SEKTA BINAFSI ALINUFAIKAA


EMBU NIWAOMBE MODERETA WAFUTE HUU UZI WAKOO
 
Bei ya mafuta unayoiona kwa Sasa inatokana na kupanda katika soko la Dunia, lililochangiwa kwa kiasi kikubwa na Vita
 
Ila jamaniii!
Kwahiyo sisi tumekaa tu yeye anatufanyia?
Mbona watanzania wasio viongozi ndio wanaoteseka zaidi kwa ajili ya nchi yao! Nani anawapa faraja?

Pamoja na mateso yao juani, machimboni, ofisini nk, wanaambulia ujira mdogo na wanalipa kodi.

Watanzania tufike mahali tuelewe kwamba maendeleo hayaletwi na rais bali ni kodi za watanzania. Tuachane na sifa zisizo na mantiki.
 
Maendeleo yataletwa na watanzania wote Ndio maana mh Rais anaendelea kutuasa Kuendelea kufanya kazi

Lakini Yale yanayopaswa kufanywa na serikali kwa kutumia Kodi zetu mh Rais na serikali yake anaendelea kufanya vyema Sana ili kumrahishia mwananchi kutimiza malengo yake

Mfano mkulima I'll afaidike na kilimo chake anahitaji apate Bei nzuri ya mazao yake yaani soko la uhakika, Bei nzuri ya pembejeo hasa mbolea, anahitaji kupunguziwa au kuondolewa kwa baadhi ya ushuru wakati wa kusafirisha mazao yake, hapo ndioo mh Rais wetu anapoweka mkono wake kwa kuhakikisha Anaondoka kero zote kwa mkulima

Anafanya kwa kutoa Ruzuku Kama alivyofanya kutoa billioni Mia hamsini ili kupunguza Bei ya mbolea,

Mh Rais wetu anafanya kazi kubwa Sana kututumikia watanzania
 
Pamoja na kumpa faraja, tafadhari wasaidizi wa Rais Samia,Tunaomba Rais wetu apumzike tunampenda..

Rais amesafiri San toka Mbeya tena kesho yuko ziarani na leo mwenyewe kasema akitoka Tanga anaenda DRC..

Alikuwa anawaambia Tarura wachape Kazi bila kuchoka maana na yeye hachoki anakomaa ila pamoja na kwamba anaweza kuwa anawaambia yuko fit ila ni vyema apate mapumziko..

Huku Mali wamempumzisha Waziri wao Mkuu 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220814-155939.png
    172.9 KB · Views: 3
amenogewa na posho za visafari, anajua mshahara wake hauguswi upo palepale kwanini asiwe busy kuzurula. Watumishi hao wengine unaowasemea wanaweza lala ofisini kama na wao utawapa posho hizo. Hata mimi navyopenda safari hivi, ajitokeze mtu wa kunipa posho kila safari..nitasafiri usiku na mchana usingizi utakuwa unaishia barabarani. Afanye kazi hakuna cha faraja hapa😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…