Tumpe Moyo Rais Samia Suluhu, hakuna aliyewahi kupendwa kwenye suala la kodi

Katika hili la kodi za miamala linaweza kuwaunganisha watanzania wakawa kitu kimoja.

Suala siyo Kodi, suala ni kiwango cha kodi kilichowekwa.

Huu ndiyo muda muafaka wa kuwaunganisha watanzania kupinga hii kitu, na wasiposikiliza ni kuwaondoa madarakani 2025.
 
Ingekuwa kodi isingekuwa shida sana. Lakini huu unyang'anyi serikali inataka kufanya dhidi ya wananchi wake.

Wanayo nafasi ya kusikiliza ushauri sasa ikiwa bado mapema na kubadilisha. Wanaweza pia kuamua kupuuza vilio vya watu. Wakiamua hilo la pili, watapata majibu yao muda si mrefu. Namuonea huruma sana Rais.....hili litamchafua mapema sana asipoingia front yeye mwenyewe kulipatia "suluhu"!

Mawazo yangu:
1. Waondoe huo unyanganyi, sio haki na haufai kwa taifa kiuchumi.
2. Waongeza ushuru kutoka wa sasa 10% na kua 15% (hii ni kwenye fee/ada inayochaji kampuni ya simu).
3. Wapunguze matumizi ya serikali. Punguza ukubwa wa serikali na bunge. Punguza pia mishahara/marupurupu ya wabunge. Punguzeni magari ya kifahari ya serikali. Siku hizi hata "wanajeshi" wanatembelea ma V8! Ajabu sana.
4. Msianzishe miradi mikubwa sasa hivi (kama inajitaji bajeti ya serikali). Malizeni kwanza iliyopo.
5. Imarisheni mbinu zinazokuza uchumi. Kodi ni matokeo ya uchumi imara na mkubwa. Wengeni mazingira rafiki ya kufanya biashara na uwekezaji na zaidi kurasimisha ardhi na shughuli za kiuchumi. Hizi tozo zitaharibu uchumi. Mtakusanya (soma kunyang'anya) leo kupitia hizo tozo lakini kesho hamtakuwa na pa kukusanya.
6. Jifunzeni kinachotokea na kuendelea kule Afrika Kusini na sababu zake. Sauti ya umma. Nchi yetu karibu asilimia 70 ni vijana. Hilo ni bomu kubwa tumekalia. Lakini ni fursa pia kama ikitumika vizuri. Lakini pia msisahau historia......kodi inaweza kuangusha serikali.

Etc.
 
We kodi za bongo sio za Dunia hii, mfano
Bidhaa moja unatwangwa kodi Mara mbili? hii ndo kodi wananchi hawapendi kulipa?

Nikitoa pesa KWA wakala Makato yale yana kodi ya serikali , ila bado serikali inaongeza Makato yake

Vocha vile vile,

Twafaaa, hakuna Cha kutiana moyo Wala nini,

Mafuta ukijaza Sheli tiyari Kuna kodi nzuri , na Makato mengine ya mamlaka, ila bado serikali inaongeza Makato yake, hizi ni kodi za sayari gani sijui
 
Mkuu Kuna kitu kinaitwa Constructive criticism.

Hiyo inaruhusiwa na ni muhimu sana.

Hata wakati wa Magufuli nilifanya hivyo na pia Sasa nafanya hivyo.
unaeleweka.
mimi dhana yangu ni consitency especially in the eyes of our rivals
 
Wacha wapitie wakati mgumu ili wapate hasira ya kumkimbiza mkoloni mweusi.
 
Y
Hii Sarafu ina Alama ya nani?Basi mpe Mungu yaliyo ya Mungu na kaisari yaliyo ya Kaisarivimeandikwa kwenyevvitabu vya dini.
 

Pitia uzi huu dadaangu hatuna chelewa bado:

Baraza jipya: Watu wale wale, wao Hawajiajiri?

Anasema bwana wa majeshi kwa kumtumaini yeye vitani, kijana mdogo David, alilishinda kitu la miraba 8, Goliath.
 
Pitia uzi huu dadaangu hatuna chelewa bado:

Baraza jipya: Watu wale wale, wao Hawajiajiri?

Anasema bwana wa majeshi kwa kumtumaini yeye vitani, kijana mdogo David, alilishinda kitu la miraba 8, Goliath.

Nakuelewa sana brazaj

Hata wakati wa mfalme Nebukadreza watu wake walipanga mengi juu ya kuwaangamiza vijana watatu waliomtumikia Mungu wa kweli; lakini vijana wale ndio waliokuja kuwa msaada kwa mfalme. Kwa kutafsiri ndoto zake na kupona kwenye vifo walivyopangiwa mfalme aliweza kujua ashike lipi ili afanikiwe.

Soma Daniel 2:1-49

Tusitumie nguvu
Tuombe katika uaminifu na tukishaomba tuwe na subira
 

Asante kwa kunielewa dadaangu. Hatuna nia mbaya. Yetu ni ya amani.

Hatutabeba silaha.

Umoja wetu unatosha sana kufanikisha maridhiano mema kwa njia za amani.
 
Asante kwa kunielewa dadaangu. Hatuna nia mbaya. Yetu ni ya amani.

Hatutabeba silaha.

Umoja wetu unatosha sana kufanikisha maridhiano mema kwa njia za amani.


AmiiiiinšŸ™
 
Mpe wewe moyo wako,ila mimi moyo wangu bado nauhitaji.

Hii mioyo mnayompa kila siku huenda ndio inamtia roho mbaya kwa kuuharibu moyo wake asili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…