Uchaguzi 2020 Tumrudishe Magufuli Chato

Uchaguzi 2020 Tumrudishe Magufuli Chato

Atohitaji Tena kura zetu atatumaliza atatushughulikia kweli kweli atofanya chochote kuhusu alivyohaidi maana hatoitaji kura zetu tena.

Kama kwa 5 yrs amewaumiza watu vipi kwa mnango huu alioupata kipindi hiki cha kampeni unategemea nn juu ya visasi kwa watz, maana atatukomesha haswaa kwa ukatili na unyama wa Hali juu akijisifu si mlidhani sirudi.

Hatari ni kubwa Sana wengi watakimbia nchi akirudi huyu
Kweli mwananchi mwenzangu, sasa inabidi tusimamie haki kwa nguvu zetu zote.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
Ndugu asante sana kwa elimu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwa Tume ipi? Hii inayoengua na kupiga red card wagombea wa vyama vingine isipokuwa cha CCM!! Kwa polisi wanaomtamkia HADHARANI mwenyekiti wa chama cha mageuzi chenye nguvu zaidi ya vyote, kuwa hatoshinda!!!
Wananchi tusimame kidete kusimamia haki zetu za msingi

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Asante Magu tutakukumbuka kwa mazuri na mabaya uliyotutendea kikubwa tu jiandae kukubali matokeo ni hayo tu kwa leo.
 
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli imekuwa ya machungu na kilio kwa Watanzania wengi. Maisha ya mwananchi wa nchi iliyowekwa kwenye kundi la uchumi wa kati yamezidi kuwa ya umasikini na ufukara mkubwa.

Serikali ya awamu ya tano imeshindwa kabisa kuboresha hali ya kiuchumi ya mtanzania pamoja na usalama na haki ya kuishi ya mtanzania. Serikali hii inamapungufu mengi sana lakini ningependa nizungumzie mambo haya mawili yaliyonihamasisha kwenda kumpigia kura Tundu Lissu hiyo tarehe 28.

Jambo la kwanza: Utawala wa sheria na uhuru wa watu
Eneo hili limejawala na giza nene. Viongozi wa serikali ya awamu ya tano wameshindwa kabisa kutawala kwa kufuata sheria zilizopo kwenye Katiba ya nchi yetu.

Miaka hii mitano ya Magufuli tumeona watanzania wakiiishi katika sayari mbili ndani ya nchi moja. Wapinzani ndani ya nchi hii wamegeuzwa kuwa watumwa na watanzania wenzao wanaoiongoza nchi.

Viongozi wa upinzani kila siku wamekuwa wakiwekwa sero na kupishana kwa kesi zisizokuwa na madai ya msingi wowote ule ndani yake. Achilia mbali viongozi wa upinzania watanzania wa kawaida ambao ni wapinzania serikali ya Magufuli imewachukulia kama adui na kuwatesa sana.

Ndani ya miaka mitano ya uongozi wa Magufuli amezuia vyama vyote vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa akidai kitu ambacho ni haki yao Kikatiba na kudai kwamba ni muda wa kazi na wamuache afanye kazi.

Kwenye awamu hii ya tano taifa liliingiliwa na watu wasiojulikana. Watu hawa ambao hawajulikani mpka sasa wamewatesa na kuwaumiza watanzania wengi wa vyama vya upinzani. Watu wasiojulikana mwaka 2017 walimpiga risasa Mh. Tundu Lissu akiwa maeneo ya Bungeni Dodoma.

Tukio lile lililokuwa na nia ya kuondoa uhai wa Lissu lakini mpka sasa jamii ya watanzania haijajua lilifanya na nani na kwa lengo gani. Ukiachilia mbali kiongozi wa upinzani kupigwa risasi bado kuna watanzania wengi wa kawaida wasiokuwa na madaraka lakini wamepotea na kutekwa na watu wasiojulikana.

Matukio ya utekaji ambayo sio desturi ya watanzania yametawala sana katika awamu hii ya tano. Visa ni vingi na wengi wetu tunavifahamu lakini jambo la muhimu na la kusisitiza ni kwamba matukio yote haya yametokea ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano ya Magufuli.

Awamu hii ya kwanza ya utawala wa Magufuli imeleata hofu na woga mwingi ndani ya mioyo ya watanzania. Watanzania tunaogopa, tunaishi ndani ya nchi yetu kama wakimbizi tukikosa uhakika na usalama wa maisha yetu wa kila siku.

Ndani ya miaka hii ya tano ya Magufuli mtanzania anaiogopa serikali zaidi hata kuliko ya katiba. Hii inatokana na wenye madaraka kuongoza kwa amri kutoka kwa Mtukufu na sio sheria za nchi zilizopo kwenye Katiba yetu.

Jambo la pili: Ajira na Maslahi ya watumishi wa serikali
Miaka hii mitano ya Magufuli ni miaka michungu sana kwa watumishi wote wa serikali. Watumishi wa umma kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hawajaongezewa mishahara ndani ya miaka mitano.

Serikali hii imeona ni vyema kuwekeza na maandeleo ya vitu kama barabara kuliko kuangalia maslahi ya watumishi wake wa serikali.
Ajira mpya kwa vijana wetu bado ni jipu kubwa. Awamu ya tano imeshindwa kabisa kutengeneza sera ambazo zingeweza kufanya vijana wetu kuajiriwa au kujiajiri.

Magufuli kwenye kampeni zake za mwaka 2015 alihubiri sana Tanzania ya viwanda lakini ameshindwa kabisa katika eneo hilo. Ukweli ni kwamba watanzania tuna njaa na wengi tunakufa kwa utapiamlo kwa kukosa chakula.

Magufuli kashindwa kabisa kugusa maisha ya Watanzania kwa miaka yake mitano aliyokaa madarakani. Jumatano ni muda wa kumfungashia virago vyake atoke ikulu aende akapumnzike kwa amani huko kwao chato.

Watanzania wenzangu tunahitaji kiongozi mwenye uchungu na watanzani na atakayeongoza kwa kufuata katiba kitu ambacho Magufuli kashindwa kukifanya katika kipindi cha miaka mitano.

Itoshe kusema kwamba uhuru wetu upo mikononi mwetu Twendeni tukampigie Kura Tundu Lissu. Lissu ndiye tumaini yetu pekee na taifa letu linamuhitaji sana. Tusifanye makosa tumpe kura za kutosha aweze kuingia Ikulu na Magufuli arudi kwao Chato.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Magufuli ni janga la taifa! Hafai kabisa
 
Back
Top Bottom