Nimesikiliza interview yake Global tv ikanisikitisha sana. Mahojiano yale yanafikirisha sana na ili kutoleta sintofahamu au kutokuelewana bora kuyaacha ili wadau wamsaidie apate matibabu.
Ila tujifunze kuwa siku yatakapokuja kukupata ya kukupata, ni familia yako ndio itayoangaika na wewe. Uzima na nafasi yako ndio kitu kinachofanya uheshimiwe na vikitoweka wote wanaojifanya kukupenda hutowaona.
Fikiria DJ Steve B akiwa active pale Clouds alikuwa anafuatwa na wangapi awasaidie? Alikuwa na marafiki including wasanii wakubwa wangapi? Simu ngapi zilikuwa zikiita kila dakika? Imagine yule ni icon wa XXL kipindi kikubwa mno cha vijana Tanzania, Kuna wakati ndio alikuwa DJ tegemeo na kichwa pekee pale Clouds baada ya Boniluv kuacha lakini sasa yupo peke yake akihangaika na ndugu zake!
Tuwe karibu na familia zetu na hasa muumba wetu. Sometimes tunaishi kama tutaishi milele, mtu hata hukumbuki hata lini mara ya mwisho kukanyaga Kanisani/msikitini! Hata ule utii na nia ya kushirikiana na Kanisa au waamini wenzako huna time zaidi ya kukimbizana na dunia!
Kama Mungu anakuhitaji na wewe mkaidi anaweza kutumia hata njia ngumu sana kukurudisha kwake kama alivyomfanyia Yona. Una siku saba za wiki tenga siku moja ya kuhudhuria ibada, kila siku omba/mshukuru Mungu hata kwa dakika chache, itakujenga na kukuokoa na mengi.
Tujitahidi kumsaidia ndugu yetu Steve B kwa kila hali ili arejee afya yake. Nimeona huruma sana. Kristo kupitia mateso na madonda yake pale msalabani amponye ndugu yetu.