Tumsaidie Steven Mdoe aka Dj Steve B anaumwa sana

Tumsaidie Steven Mdoe aka Dj Steve B anaumwa sana

Nimesikiliza interview yake Global tv ikanisikitisha sana. Mahojiano yale yanafikirisha sana na ili kutoleta sintofahamu au kutokuelewana bora kuyaacha ili wadau wamsaidie apate matibabu.

Ila tujifunze kuwa siku yatakapokuja kukupata ya kukupata, ni familia yako ndio itayoangaika na wewe. Uzima na nafasi yako ndio kitu kinachofanya uheshimiwe na vikitoweka wote wanaojifanya kukupenda hutowaona.

Fikiria DJ Steve B akiwa active pale Clouds alikuwa anafuatwa na wangapi awasaidie? Alikuwa na marafiki including wasanii wakubwa wangapi? Simu ngapi zilikuwa zikiita kila dakika? Imagine yule ni icon wa XXL kipindi kikubwa mno cha vijana Tanzania, Kuna wakati ndio alikuwa DJ tegemeo na kichwa pekee pale Clouds baada ya Boniluv kuacha lakini sasa yupo peke yake akihangaika na ndugu zake!

Tuwe karibu na familia zetu na hasa muumba wetu. Sometimes tunaishi kama tutaishi milele, mtu hata hukumbuki hata lini mara ya mwisho kukanyaga Kanisani/msikitini! Hata ule utii na nia ya kushirikiana na Kanisa au waamini wenzako huna time zaidi ya kukimbizana na dunia!

Kama Mungu anakuhitaji na wewe mkaidi anaweza kutumia hata njia ngumu sana kukurudisha kwake kama alivyomfanyia Yona. Una siku saba za wiki tenga siku moja ya kuhudhuria ibada, kila siku omba/mshukuru Mungu hata kwa dakika chache, itakujenga na kukuokoa na mengi.

Tujitahidi kumsaidia ndugu yetu Steve B kwa kila hali ili arejee afya yake. Nimeona huruma sana. Kristo kupitia mateso na madonda yake pale msalabani amponye ndugu yetu.
This is Deep[emoji22][emoji22]
 
Ugonjwa mbaya sana huo kibaya zaidi huwa unawafilisi kwanza halafu mgonjwa anafariki!...so sad!
Nimeona kwenye acc yake ya instagram ,may 14 alikuwa anauza gari aina ya NOAH nahisi ni ya kwake.

Alafu naona wadau wapo kimya,wanaohangaika ni madj peke yao,wadau wengine wa bongo fleva wamekaa kimya.
Screenshot_20190820-211734.png
 
Kaamua kuokoka naona....

Get well Steve b

Ova
Swala la Steve B linasikitisha sana. Akifikia hatua mbaya ndio utaona "wadau" wanakurupuka. Tanzania tumejaa unafiki sana na mbaya zaidi hata kupitia matukio kama haya hatujifunzi!

Hii ndio askofu Kakobe anaita kiburi cha uzima! DJ Steve B anaumwa na msaada kwake ni sasa! Post hii chini ya Mchomvu speak a lot ..kweli? Hata wadau wa karibu?

Screenshot_20190821-212846_Instagram.jpeg
 
Wengine hata kurepost tu ombi lake la msaada! Walau nimeona DJ John Dilinga na Venture wamejilipua kuchangisha ...
Kama hawa wasanii wa bongo fleva wapo kimya wanasubiri afe,kesho wakamtungie nyimbo za kumkumbuka .
 
dah so saaaad, binafsi nikiwa msanii miaka ya nyuma jamaa alinigusa direct kabisa. nakumbuka ilivyokuwa shida kumuona iwe club au hata clouds pale lkn alitupigania sana na hata tukafika mbali, ila Mungu ananjia nyingi sana kutufanya binadamu kuwa si kitu kwake. Get well soon brother
 
Jina lako la kisanii ni nani?
 
Swala la Steve B linasikitisha sana. Akifikia hatua mbaya ndio utaona "wadau" wanakurupuka. Tanzania tumejaa unafiki sana na mbaya zaidi hata kupitia matukio kama haya hatujifunzi!

Hii ndio askofu Kakobe anaita kiburi cha uzima! DJ Steve B anaumwa na msaada kwake ni sasa! Post hii chini ya Mchomvu speak a lot ..kweli? Hata wadau wa karibu?

View attachment 1187066
Kweli kabisa! Nmeona ayo TV akielezea mwanzo mwisho nn kina msibu na namna gani ya kumpatia msaada
Kwa Kweli kaekezea vizuri
Huu ndy wakati wa kumsaidia

Ova
 
hivi wagonjwa figo hawatibiwagi na NHIF
Gharama za matibabu ya figo NHIF hawawezi kutoa,sababu ni kubwa, gharama za kusafisha figo ni zaidi ya laki tano kwa wiki.
Kila wiki unatakiwa usafishe mpaka hali itapotengemaa.
 
Back
Top Bottom