Tumshauri kijana mwenzetu Adam Mchomvu achague A au B au C

Adamu ni mtangazaji mzuri wa kariba yake....anapenda sana utani na masikhara......komedian na mropokaji

Sio kweli kama yupo underrated pala CMG
Adamu alimkuta B12 XXl so ilikua ni sahihi tu kuendelea kua chini ya B12

Akapewa kipindi chake cha Bongo Fleva alikiongoza hadi pale yeye mwenyewe alipoomba apewe kipindi maalamu cha Hip Hop kwakuwa aliona kama Hip Hop haipati platform kama wabana pua
Ndio akapewa So So Fresh na Bongo Fleva akapewa Kennedy
Ndio maana kule So So Fresh ni mwendo wa Hip Hop mwanzo mwisho

Kwa muktadha huu Adamu anakipindi chake kama anchor kama walivyo Kennedy na Bongo Fleva, Mumy Baby na Top twenty
Na kutokuwa anchor wa kipindi hakukufanyi wewe kuwa underrated. Marehemu Kibonde, Kipanya, Gadner, Mussa nk ni watangazaji wakubwa lakini hawana vipindi vyao wanaongoza
Kumbuka bwana mdogo George Bantu ndio anchor wa jahazi na alikua naongoza wakongwe kibonde na gadner

Kuhusu Adamu kuacha muziki sioni mantiki yake
Yeye mwenye anasema anafanya Hip Hop kama hobby yake na sio kazi yake

Kuhusu Fiesta Adamu ana play party kubwa sana, licha ya kuwa Mc kwenye matamasha, Adamu ndio chief judge wa super nyota wa Fiesta mikoa yote inapofanyika fiesta

Kwa kupitia uzoefu CMG wanaweza wasiwe ndio Media house wanalipa vizuri Tz lakini ukweli ndio Media hause yenye fursa nyingi sana wa watangazaji wake kuliko media yeyote
Wengi waliondoka lakini mwisho wasiku walirudi wenyewe mjengoni
 
Ni muhimu kuheshimu mtu anayepewa muda mchache na analipwa. Tambua kabisa hizo dk30 Mchomvu asipokuwepo huwa kipindi kinapwaya hata alipokuwepo B12

Mchomvu anavitu vyake na style yake ya utangazaji. Bilashaka ana watu anaowavutia

Kipindi kupewa Kennedy hiyo ilionekana tangu mwanzo maana yeye ndo alikuwa co-host wa B12

Pale wenye kazi ya kufanya ni wale madada. Mami bebi na Meena Ally. Wale bado wanakelele nyingi huenda mbeleni huko watakuwa watu wazuri lakini ni mpaka wamalize assignment

Meena mara mia angebaki zake Amplifayani kule japo aliharibu haribu ili alikuwa ameanza kuzoea. Mamii akitulia, akawa anaweka pozi kwenye maongezi yake atafanikiwa

Mchomvu akijifunza akakubali kutumia masikhara yake vizuri na akawa anayaelekeza in positive way halafu yakawa na kipimo, ni mtangazaji mzuri sana sema kuna wakati anapitiliza kama kina Gardener tu na jahazi lao, maneno maneno yanayoelekea "matusi matusi" yamekuwa mengi kitu ambacho sio kizuri sana. Ni lazima kumsoma kwanza mtu anayehojiana nae kujiridhisha kama anaweza kuvumilia masikhara au yatamuondolea mood
 
Umeongea kweli kabisa, ukisikiliza kile kipindi cha ijumaa kuanzia saa 4;30 usiku haya unayosema yote yanafanyika hapo.
Jamaa yupo talented lakini bange nyingi..hawezi pewa kipindi aongoze yeye,kwanza atajipigia hiphop tupu
 
Kumwambia kuwa yeye ni bora zaidi ya wengine wote uliwataja hapo ni kumdanganya. Taasisi inajua watu wake zaidi ya sisi tunaosikia sauti zao tu.
 
Unamdanganya mwenzio eeeh..yaani akitoka tu hapo na R.I.P inamhusu

Nani aliwahi kutoka clouds halafu akaenda kutamba kwenye hizo redio zenu uchwara
 
Ni kweli Mkuu. Lakini kutoa ushauri mzuri hivi ni rahisi kuliko wewe mwenyewe ndiye ungekua Adam Mchomvu na utekeleze hiki hiki ulicho shauri.
..
Kutakuwa na sababu ya wao kufanya hivyo, maana huenda jamaa bila kumfunga kithibiti mwendo atapitiliza maana Adam ni kama kichaa flani japo ule ukichaa wake hata mimi naupendaga uwa yuko really.
. .
Kweli, mfano kipindi cha soso fresh kimeshakuwa kipindi cha hiphop full kupiga mangoma ya hihop
. .
Adam ni msela sana so akipewa kipindi akiongoze ni wazi kitakufa ndani ya miezi michache tu.
Unamkubali adam kwa sababu anakuwepo mtu kumfunga mdomo hali ikiwa tete.
 
Napigia mstari. Na-support ulichoandika hapo juu! Big Up!
 
Kweli kabisa... I think Adam knows what he is doing..
And he is happy about it!

So watu wasiforce sanaa Afanye wanavyotaka wao!
 
Aliyeshauri kale ka meena kaende xxl ni nani? Kale kanafaa taarabu na gea j2 tu ni kanapiga kelele tu..bora mamybaby kuliko uyo meena
 
Mi Nadhan muarusha huyu og apewe ara za roho tu anaweza leta radha ya mapenz kihiphop
 
Adam ni Arachuga og, ni zile damu za Hiphop ambazo hata ufanyaje huwezi kuzibadili. Tatizo ni bado hajapata wa kujua jinsi ya kumtumia huko kwenye Hiphop. Yule alipaswa apewe uwanda mpana kuwakilisha hiphop pale CMG
Aibu naona hip hop gani ya nikki wa pili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…