Tumuache Samatta acheze mpira

Tumuache Samatta acheze mpira

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Watanzania wapenda michezo na wanaojua mpira na nidhamu kwenye michezo tuungane na Mbwana Samatta katika hili dhidi ya watanzania wenye lugha chafu na wasiojua mpira na wanaoshabikia tu mpira, wenye dhihaka dhidi ya timu yake na wachezaji wenzake katika timu.

IMG_20200203_101743.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nae aachane na mambo ya washabiki akijite katika kucheza mpira, hamna namna yoyote unaweza mzuia shabiki kuongea hata hiyo timu yake inakijua hilo.
Unadhani wao ndio wa kwanza kutolewa mapovu? tena ni bora haya mapovu ya kiswahili hawayaelewi vizuri
 
Samatta nae anajishtukia tu .
angeona akina Sterling wanavosemwa je ? Juzi Xhaka katishiwa kuvunja miguu tena na mashabiki wake mwenyewe . Yeye acheze mpira aachane na mambo ya mashabiki
 
Sio ishu ya kutishiwa, watanzania wanawachonganisha yeye na grealish, hio ni mbaya sana na hatujui grealish atalichukuliaje hili suala sababu yeye samatta hadi kusema hivyo pengine ameshaona tayari effect sababu yeye ndie anayekaa nao huko mazoezini
Samatta nae anajishtukia tu .
angeona akina Sterling wanavosemwa je ? Juzi Xhaka katishiwa kuvunja miguu tena na mashabiki wake mwenyewe . Yeye acheze mpira aachane na mambo ya mashabiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atuvumilie tu maana yeye ndiye mbongo wa kwanza kucheza EPL na Aston Villa ndio klabu ya kwanza ya EPL kusajili Mtz! Baadae tutazoea na mambo yatosonga kama kawaida! Kila la kheri Mbwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mmoja nimeona anawauliza Aston Villa yakuwa wiki moja yake Samata si imeshaisha wamlipe Mshahara wake wa wiki,Dah wabongo bwana hadi mshahara wa mtu wanauulizia
 
Back
Top Bottom