Tumuenzi Edward Saidi Tingatinga

Tumuenzi Edward Saidi Tingatinga

moghasa

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
1,084
Reaction score
1,254
Nimeanza na hilo jina makusudi ili niwatoe watu katika fikra za siasa na tu-refresh kidogo.

Edward Said Tingatinga ni mchoraji maarufu aliyezaliwa katika kijji cha Namochelia huko Tunduma mnamo mwaka 1932. Mtu huyu alikuwa maarufu sana kwa michoro ijulikanayo kama "Tinga Tinga ", kazi ambazo huenda kwa jina lake maarufu la "Tingatinga!!

Sina maana ya kuelezea historia ya Tingatinga, ila napenda leo niwashirikishe kwa jinsi na namna ninavyoumia kuona hakuna harakati zozote za jamii yetu kutambua wala kujali kazi za "Tinga Tinga" . Sisi Waafrika muda mwingine nashawishika kwanini kuwa tuna shida fulani mahali fulani.

Moja ya wachoraji wakubwa waliowahi kutokea hapa duniani ni pamoja na "PICASSO" huyu akiwa ni Mhispania kama sikosei, Leonardo Da vinci, huyu ni Muitaliano aliyechora picha nyingi Vatican city!!

Michael Angelo, huyu pia akiwa mhandisi wa majengo na mchoraji aliengineer mojawapo ya majengo ya Vatican city na michoro pia!! Moja ya picha yake maarufu ni "Universal Judgement "

Watu hao yawezekana hawakuwa maarufu kwa kipindi cha uhai wao, lakini kulingana na juhudi za serikali zao " wataishi milele "

Shida yangu ipo kwetu sisi Watanzania, je, ni kwa namna gani tunamkumbuka Edward Said Tingatinga!?

Ni kwa jinsi gani tunahakikisha tunapata picha zake ambazo zilisombwa kwenda Ujerumani na Uingereza enzi za utawala wa mkoloni?

Anza wewe!!

Kwa kumweshimu Tingatinga nilianza kwa kununua moja ya greeting cards zenye moja ya michoro yake na kumpelekea Shem/wifi yenu!!

My take!!
Ufike wakati Waafrika tuheshimu amali zetu, na sio picha tu na akina "Tinga Tinga company " ila na utamaduni wetu kwa ujumla!!
 
Huyu Tingatinga wengi wa umri wetu hawamjui...hata mimi nilimjua kipindi nipo shuleni nakumbuka Headmaster alitumegea ka historia kafupi...
 
Wakati mimi nawaza wamama wajawazito watawezaje kujifungua ktk mazingira bora na salama,elimu bora,huduma za maji safi na salama kumbe kuna wengine wanawaza vibonzo,
Tingatinga yeye ni msanifu wa uchoraji na inawezekana ameshafaidika sana kutokana na kazi za mikono yake.
 
Watazoa tanzanite yoote hata kumbukumbu ya gram moja itakosekana ktk jumba la makumbusho miaka 50 ijayo,faida ya kuwepo iyo hapa haitaonekana cha msingi yangeboreshwa maisha kwa wa tz ndio wangenunua picha,vinyago na kwenda mbugani watu hawana uhakika wa kesho unamwambia umempunguzia gharama za kutalii hata ingekua bure kama life kwa maisha ya wengi ni ya kubahatisha hawata enda kutalii.
 
Wakati mimi nawaza wamama wajawazito watawezaje kujifungua ktk mazingira bora na salama,elimu bora,huduma za maji safi na salama kumbe kuna wengine wanawaza vibonzo,
Tingatinga yeye ni msanifu wa uchoraji na inawezekana ameshafaidika sana kutokana na kazi za mikono yake.

mkuu!! Makamee kumbuka uchoraji wa Tingatinga umeasisiwa hapa kwetu! tukiwekeza na kufungua makumbusho ni moja ya eneo kubwa la uwekezaji! picha za kisanifu za kuchorwa kwa mikono niajira tosha kwa vijana wengi tusio na ajira! pia humfanya mbunifu kukumbukwa milele!!
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa mkuu umesema kweli, leo hii pia tunaona kazi hiyo ikiendelezwa na vijana wengine kule oysterbay kama sikosei. Kumbe muasisi wake ndo huyu said, je bado yupo?. Mi pia napenda kujifunza kazi hizi za mikono, je naweza jifunzia wapi mkuu??
 
Mleta mada sijajua kama ni kusudi lako kupotosha ukweli au ni bahati mbaya.

Edward Tingatinga alizaliwa kijiji cha Nakapanya wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma. Umetaja kijiji cha Namochelia kuwa ndipo alipozaliwa, si kweli.

Ukweli ni kwamba Namochelia ni eneo ambalo lilikuwa likikaliwa na watu kabla ya mpango wa vijiji vya ujamaa kuanzishwa na Mzee au Chifu wa eneo hilo kwa wakati huo akijulikana kwa jina Namochelia.

Ijapokuwa wenyeji wa wilaya ya Tunduru ni wa kabila la Wayao sehemu kubwa ya Nakapanya na vitongoji vyake inakaliwa na Wamakuwa ambao hupatikana kwa wingi katika wilaya jirani ya Masasi mkoani Mtwara.

Ni hayo tu. Nawapisha wenzangu... Bhaaa bwana wewe somo!
 
Mwendabure kwa namna moja au nyingine uko sahihi, na mimi pia niko sahihi, Namochelia kililkuwa kijiji halisi na halari kabla ya vijiji vya ujamaa! baadae kikaunganishwa na vitongiji vingine na kuwa kijiji cha Nakapanya! ni sawa na kusema Anne Makinda kazaliwa mkoa wa Iringa!! mwingine akasema sio mkoa wa Iringa ni mkoa wa Njombe!! ni hayo tu!!
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa mkuu umesema kweli, leo hii pia tunaona kazi hiyo ikiendelezwa na vijana wengine kule oysterbay kama sikosei. Kumbe muasisi wake ndo huyu said, je bado yupo?. Mi pia napenda kujifunza kazi hizi za mikono, je naweza jifunzia wapi mkuu??

mkuu kimbisi mbisi huyu jamaa alishafariki mwaka 1972 aliuwawa na maaskari wetu watukufu! ila hati miliki ya kazi zake iko chini ya mwanae wa kike!! kwa habari zaidi hapo Oysterbay watakupa updates mhimu!!
 
Last edited by a moderator:
mkuu kimbisi mbisi huyu jamaa alishafariki mwaka 1972 aliuwawa na maaskari wetu watukufu! ila hati miliki ya kazi zake iko chini ya mwanae wa kike!! kwa habari zaidi hapo Oysterbay watakupa updates mhimu!!

Ahsante mkuu, kumbe kafa zamani ase, maana hii michoro ina umaarufu hata hivyo.
 
Last edited by a moderator:
moja ya hoja za Obama kuifahamu vizur Tanzania ni baada ya tune ya maneno "Tinga Tinga " na michoro yake ilipokuwa ikitumiwa katika moja ya ads za CNN, baada ya kupenda aina ile ya uchoraji ndipo akagundua ilikuwa Tanzania!!!
 
Back
Top Bottom