moghasa
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 1,084
- 1,254
Nimeanza na hilo jina makusudi ili niwatoe watu katika fikra za siasa na tu-refresh kidogo.
Edward Said Tingatinga ni mchoraji maarufu aliyezaliwa katika kijji cha Namochelia huko Tunduma mnamo mwaka 1932. Mtu huyu alikuwa maarufu sana kwa michoro ijulikanayo kama "Tinga Tinga ", kazi ambazo huenda kwa jina lake maarufu la "Tingatinga!!
Sina maana ya kuelezea historia ya Tingatinga, ila napenda leo niwashirikishe kwa jinsi na namna ninavyoumia kuona hakuna harakati zozote za jamii yetu kutambua wala kujali kazi za "Tinga Tinga" . Sisi Waafrika muda mwingine nashawishika kwanini kuwa tuna shida fulani mahali fulani.
Moja ya wachoraji wakubwa waliowahi kutokea hapa duniani ni pamoja na "PICASSO" huyu akiwa ni Mhispania kama sikosei, Leonardo Da vinci, huyu ni Muitaliano aliyechora picha nyingi Vatican city!!
Michael Angelo, huyu pia akiwa mhandisi wa majengo na mchoraji aliengineer mojawapo ya majengo ya Vatican city na michoro pia!! Moja ya picha yake maarufu ni "Universal Judgement "
Watu hao yawezekana hawakuwa maarufu kwa kipindi cha uhai wao, lakini kulingana na juhudi za serikali zao " wataishi milele "
Shida yangu ipo kwetu sisi Watanzania, je, ni kwa namna gani tunamkumbuka Edward Said Tingatinga!?
Ni kwa jinsi gani tunahakikisha tunapata picha zake ambazo zilisombwa kwenda Ujerumani na Uingereza enzi za utawala wa mkoloni?
Anza wewe!!
Kwa kumweshimu Tingatinga nilianza kwa kununua moja ya greeting cards zenye moja ya michoro yake na kumpelekea Shem/wifi yenu!!
My take!!
Ufike wakati Waafrika tuheshimu amali zetu, na sio picha tu na akina "Tinga Tinga company " ila na utamaduni wetu kwa ujumla!!