Tumuombe radhi ambao aliposema tumuombee, hatukujua anamaanisha nini

Tumuombe radhi ambao aliposema tumuombee, hatukujua anamaanisha nini

1.jpg




lissu-data.jpg


41028383_101.jpg


..tukio hili.
 
Radhi ya nini tena?
Wakati wajuba tulikuwa tunashusha maombi kama mvua. Sema Amina, basi ya radi⚡⚡
 
Hii kauli ya mwamba mpaka leo huwa inajirudia masikioni mwangu ni kama namuona alivyokuwa akihutubia na hakisisitiza hili jambo.

Kuna wakati nahisi huyu mwamba hakuwa mtu wa kawaida hasa nikiwaza jinsi alivyopambana na issue ya corona yaani Dunia nzima ilitandwa na hofu ila yeye hakuonesha kutetereka hata pale viongozi wa dini walipoingiwa na hofu yeye alisema tumuamini Mungu na nyumba za ibada hazitofungwa hakika huyu mwamba alikuwa na imani ya kweli isiyo na unafiki.

Hivi sasa dunia nzima inaishi na corona kama alivyokuwa akisisitiza yeye. Hapo ni kwamba huyu mwamba alikuwa na uwezo wa kuona mbele zaidi kabla ya wengine hiki ni kipaji ambacho binadamu wengi hawana.

Mwamba aliokoa maisha ya watanzania wengi sana wasife kwa njaa na na maradhi mengine kisa kufungiwa ndani kuogopa corona. Pia aliokoa maisha ya maelfu ya watu wa nchi jirani kwa kutokufunga mipaka na kuhakikisha huduma za kibinadamu zinawafikia.

Kwa haya machache yanatosha kabisa mwenyezi Mungu kumsamehe dhambi zake zambi maana hazina ya wema wake itamtetea na kwa jinsi watanzania wanavyomkumbuka kila siku na kumuombea inamuongezea hazina yake binguni.

Binadamu tutende wema na haki na kufanya mambo makubwa kwenye kila sehemu unapofanyia kazi ili leo na kesho ukiwa haupo basi wema wako huishi kwa watu. Wema au ubaya wako utakufuta.
 
Back
Top Bottom