Tumuombee sana Mzee Butiku wa taasisi ya Mwalimu Nyerere

Tumuombee sana Mzee Butiku wa taasisi ya Mwalimu Nyerere

Juzi kaitisha press conference kuelezea hali ya usalama inavyoendelea nchini baada ya mauaji ya Mzee MeD kiongozi wa CHADEMA.

Mimi kwangu kule nakuita kujilipua na uthubutu wa aina yake katikati ya mazingira tuliyo nayo sasa... Maana kusema KWELI na kwa UWAZI kwasasa ni kujitafutia majanga makubwa
Amezungumza mambo makubwa na lawama na mshangao wake kaelekeza moja kwa moja kwa wahusika bila kificho wala kupepesa macho.

Mambo yale yangezungumzwa na sisi tunaoitwa wapinzani sidhani hata kama ile press Conference ingeisha

Pamoja na kutambulika na kuheshimika kwake mzee Butiku.. Pamoja na ulinzi alionao lakini tumuombee sana.

Kwa namna watu walivyochanganyikiwa huko ndani, kitendo cha kuwakosoa kwa namna ya mzee Butiku ni kujipalia makaa ya moto mkali na kutangaza uadui

Video hizi hapa za yote aliyonena mzee Bujiku... Tumuombee sana.

Soma Pia:
Boss unakumbuka Bernard Membe? Mungu amlaze mahali pema peponi, wao kwa wao kukosoana hawaduriani kiviile. Hata MB mpina hawawezi kumgusa
 
Sioni sababu ya kuwa na hofu yoyote, Mzee Butiku ametumia haki yake kikatiba kutoa maoni yake, hajavunja sheria yoyote.

Akidhurika kwa vyovyote vile, wahusika watajulikana kirahisi sana hata kama huwa wanajiita wasiojulikana.

Kweli kabisa ingawa hii haki watu wabinafsi wanataka kuipokonya iwe yao tu.
Wengine wote tusithubutu kusema chochote
 
Back
Top Bottom