Tumuweke kwenye maombi yetu Ismaël Koné, avunjika Mguu kwa Rafu Mbaya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kiungo wa Canada, Ismaël Koné, amepata jeraha kubwa la kuvunjika mguu kufuatia rafu mbaya aliyofanyiwa na mchezaji wa Qatar, Assim Madibo.

Baada ya tukio hilo, Madibo alionyeshwa kadi nyekundu huku Koné akitolewa uwanjani kwa machela, katika mchezo huo ambao Canada iliibuka na ushindi mabao 6-0 dhidi ya Qatar kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

1781848468236.png
 
allah amfanyie wepesi apone haraka aamin🙏
 
Siwezi kumuombea, Canada wana roho mbaya. Wamezuia wachezaji wa Ghana na Ivory Coast wasiingie kisa wana tuhuma mahakamani, hayo ni malipo ya Mungu. Kwanza Kone asili si Mkanada.
Comrade, wewe ni mdau wa michezo! Inakuwaje unakosa fair play kwenye jambo dogo kiasi hiki! Mchezaji kwenye asili ya Afrika kuchezea timu ya Bara/nchi nyingine siyo dhambi au kosa la jinai!

Lakini pia kitendo cha serikali ya Canada kuwapiga marufuku hao wachezaji uliowasema hapo juu, hakina uhusiano wowote ule na timu ya Taifa au wachezaji wa Canada.

Kubali tu kitendo alichokifanya huyo mchezaji wa Qatar siyo kitendo cha kiungwana. Na hivyo amestahili kuadhibiwa kwa kadi nyekundu. Kuhusu suala la kumuombea, hiyo ni hiari yako. Hakuna mtu wa kukulazimisha.
 
CANADA NA Marekani hawajafanya fair play, mtu anakuwa na hatia pale anapohukumiwa. Kitendo cha kuwazuia wachezaji kisa tuhuma ni kama wanawakomoa na kupunguza nguvu za timu husika. Malipo ni hapahapa.
 
Baada ya tukio hilo, Madibo alionyeshwa kadi nyekundu huku Koné akitolewa uwanjani kwa machela, katika mchezo huo ambao Canada iliibuka na ushindi mabao 6-0 dhidi ya Qatar kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Lakini ndio mpira wa miguu ulivyo
 
Back
Top Bottom