Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 224
- 236
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa siri nyingi zimefichwa kwenye maandishi ndio maana tunavitu vingi tunavyo lakini tunashindwa kuvitumia na waliotangulia kuyafunua hayo maandishi ndio silaha yao wanayoitumia kututumia.
Tukiwa kwenye group moja la mitandao ya kijamii, Mchangiaji mmoja na mbobevu wa masuala ya Uchumi aliweza kueleza kuwa " black ni black, kokote alipo, a gifted human race, ignorant of their gifts and richness (Prof Mujwahuki). Hii hoja yake ilinifikirisha sana na kuona ni namna gani hatujajua kutumia vitu tulivyo navyo na kuweza kujivunia ambavyo vinatusaidia.
Leo hii Rais wetu Dr John P Magufuli anakuwa miongoni mwa viongozi bora ulimwenguni kote , wenye macho mmeona na wenye masikio mmesikia. Sasa hivi nchi nyingi huko ulimwenguni zinatamani zingekuwa na Rais wa kariba ya Dr John Magufuli. Tumeona baada ya kupata janga la corona hakupaniki kama mataifa mengine bali akatulia na kutoa maamuzi sahihi ambayo leo hii watanzania tunaishi kwa amani pasipo kuwa na hofu ila cha muhimu tunazidi kupata elimu ya tahadhari ya janga hili.
Baada ya Rais wetu kutoa tamko juu ya vifaa feki vilivyoletwa kwa ajili ya kupima Covid 19 tuliona hata nchi nyingine kama India , Spain na nchi nyingine walisemea hilo. Wakati Rais wetu anatuambia tukazanie maombi na kuungana waumini wa madhehebu yote kukemea hili janga watu walibeza lakini baadae tuliona na mataifa ya nje wanaanza kukazania kufanya maombi.
Haikuishia hapo ni huyu huyu Dr John Magufuli alikemea kutumia dawa za kupulizia kuzuia corona baada ya hapo tukaona na Shirika la Afya Duniani WHO nao wanakataza kutumia hizo dawa.
Prof Lumumba alivyokuja Tanzania akiwa Ikulu alisema " History is the fair judge" akimaanisha kuwa leo hii mambo ambayo kashayafanya Rais wetu yatathibitisha jinsi anavyosaidia kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati. Tumeona miundombinu inavyoboreshwa na sekta ya afya kuhakikisha kila wilaya wana vituo vya afya bora ambavyo vitasaidia watanzania wote.
Katika kupitia nukuu mbalimbali nikaona ya Baba yetu wa taifa Mwl Nyerere aliwahi kusema kuwa " Viongozi wazembe naona kuna watu wanadhani kiti cha Urais ni cha starehe sana huwezi kuwa Rais kama huna uchungu na watanzania najua taifa hili limeliwa sana lakini kuna awamu inakuja itakayoirudisha Tanzania kwenye heshima yake na dunia nzima itashangaa...nasema tena hiyo awamu ipo inakuja" Japo wengi watataka kuvuruga amani ya Tanzania lakini nawaambia haitawezekana ( Mwl Nyerere).
Kupitia kwa mwanafalsafa huyo tumeyashuhudia kupitia kwa mwamba , jemedari, chuma na tingatinga Rais wetu Dr John Magufuli.
Sasa hivi tunaelekea kwenye mchakato wa uchaguzi lakini tayari watanzania wenye mapenzi ya dhati na nchi yao hawana chaguo lingine zaidi yake kwa kiti cha Urais. Sasahivi uongozi wake uliotukuka ni wimbo wa watanzania wote pamoja na mataifa mengine. Mchakato mkubwa utakuwa upande wa wabunge na madiwani maana huko ndio wanahitajika watu sahihi watakaomsaidia kuijenga nchi yetu kwa ufanisi na ueledi wa hali ya juu.
Kupitia uongozi wa Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kafanya kiwe ni chama cha kila mtu. Leo hii tunaenda kwenye uchaguzi lakini watu wanachoamini mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi ilihali ni mtu mwenye maono na wananchi wanamuamini pasipo kuangalia kipato chake. Mlimwengu mimi nilipotia nia ya kugombea ubunge kwa mwaka 2015 watu walisema haiwezekani na mimi nikaamini hivyo haiwezekani. Leo hii kila mtu anasema huu ni muda sahihi wa kuchukua fomu na kugombea nafasi uitakayo. Na mimi pasipokupepesa macho nitachukua fomu muda utakapofika kutokana na namna Rais wetu alivyofanya chama kiwe cha haki na usawa kama katiba yake inavyojieleza.
Mlimwengu mimi pamoja na walimwengu wengine tunakuombea Rais Mungu azidi kukutia nguvu na uendelee na kazi nzuri unayoifanya. Watanzania tunakupenda na tuna imani na wewe. 2020 tunakuchagua tena.
20/05/2020
Mohamed Ismail
Email:mohammedismail613@gmail.com