HOJA Tuna Kampeni ya Usafi Kitaifa, lakini unafahamu kama Dar yenyewe ina Dampo rasmi moja tu?

HOJA Tuna Kampeni ya Usafi Kitaifa, lakini unafahamu kama Dar yenyewe ina Dampo rasmi moja tu?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Club Mate

Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
29
Reaction score
125
Habari za wakati huu wakuu,
Siku hizi kila kona stori ni kuifanya Dar iwe safi tena. Tunaona wanasiasa na watendaji wakiwa mtaani na mifagio kwa mbwembwe nyingi, huku wakitangaza faini za hadi TZS Milioni 1 kwa mtu atakayetupa taka ovyo. Lakini wanafeli kujibu swali moja la msingi sana:

Hizo taka kimsingi zinatakiwa kupelekwa wapi?
Jiji la Dar es Salaam lenye takribani watu Milioni 8 lina jibu moja tu rasmi kwa swali hili. Moja tu! Dampo la Pugu Kinyamwezi. Kwa maana hiyo, kila dampo lingine unaloliona kwenye hili jiji letu "safi sana" halitambuliki rasmi, na yapo mengi mno.
Ili kuonyesha ukubwa wa hili tatizo, nilijipa kazi ya kufuatilia na kuweka kwenye ramani madampo yote yaliyo karibu na mto mmoja tu hapa Dar, Mto Mbezi (kama inavyoonekana kwenye ramani hapo chini). Kuanzia mdomoni mwa mto hadi kufika Barabara ya Morogoro, umbali wa kama kilomita 20 hivi, nimekuta madampo 19! Na mengi yapo pua na mdomo na makazi ya watu.

Dumps.jpg


Moja ya madampo hayo lipo ubavuni kabisa mwa shule ya msingi, Shule ya Msingi Matosa. Upepo ukivuma kuelekea upande wa shule, uwanja mzima wa shule unajaa uchafu. "Vipi kuhusu mamlaka husika?" unaweza kujiuliza... Ofisi za mamlaka husika (Serikali ya Mtaa wa Matosa) zipo upande wa pili tu wa uwanja wa hiyo shule! Na wanaonekana hawashtuki wala kujali kabisa kuhusu hili suala. Wingi wa haya madampo unaonyesha wazi kabisa kuwa wakandarasi wa kuzoa taka waliopewa zabuni kihalali na manispaa ndio wanaojaza haya madampo yasiyo rasmi.

photo_2026-10-13_14-09-42.jpg


Sasa tufanyeje, tuanze kuhesabu vipande vya taka kwenye madampo ya mitaani kwetu na kuziandikia faini manispaa zetu? Si wao ndio vinara wakuu wa kuchafua mazingira? Labda mamilioni ya faini yakianza kutoka mifukoni mwa maofisa wa manispaa yatasaidia kujenga madampo yaliyo rasmi na yenye viwango.

Taka zetu zinatakiwa kwenda wapi sasa?
Bila shaka siyo kwenye maeneo yasiyodhibitiwa, yasiyo na utaratibu, na yasiyofaa pembezoni mwa mito na katikati ya makazi ya watu. Kama tunaona huo ndio utatuzi, basi ni bora tukamwage hizo taka moja kwa moja baharini tu.
Hapana! Taka zetu zinatakiwa kwenda kwenye madampo yaliyotengenezwa na kuendeshwa kwa ajili ya kuchakata taka kwa namna ambayo inapunguza madhara kwa binadamu na mazingira. Hii inajumuisha recycling ya plastiki, chupa, na chuma, uchakataji sahihi wa vifaa vyenye sumu na hatari kama vifaa vya kielektroniki, kemikali, na betri na kama zikichakatwa vizuri, mitambo ya kuchomea taka inaweza hata kutumika kuzalisha umeme.

Kama kweli tunataka jiji safi, lazima tutatue haya matatizo ya kimfumo.
Ndiyo, tunahitaji kubadili tabia na watu wawe na uelewa zaidi wa wapi na namna gani ya kutupa taka zao, lakini juhudi hizi ni lazima ziende sambamba na uwekezaji kwenye miundombinu ya uchakataji taka. Tunahitaji kushughulikia mizizi ya tatizo, siyo hizi sarakasi na matamko ya mwezi mmoja halafu mambo yanarudi palepale kama zamani, sawa tu na lile vumbi ambalo wafagiaji wa barabara wanalisukumia pembezoni mwa lami, halafu kesho yake upepo unalirudisha tena barabarani.

Nawasilisha. Karibuni kwa mjadala!
 
Ila waafrika ni tuna umeme kidogo sana kwenye vichwa vyetu 🤣🤣🤣🤣🤣.. hao wanaoitwa viongozi kuanzia level za chini hawajali na haiwasumbui kuwa na uchafu wa kutosha katika maeneo wanayo yaongoza halafu ndo unategemea kwa akili hizi tuwe wabunifu na hatimaye tuweze kuanza kuwaza kurusha satelite angani?? 🤣🤣🤣
 
Sahihi kabisa, dampo kubwa na rasmi kuwa moja tena pembeni ya mji sio sahihi, hii inasababisha magari ya wakandarasi kutumia muda mwingi barabarani,.mbaya zaidi dampo lenyewe lina miundo mbinu duni hasa kipindi cha Masika..Pole ndugu yangu Kishere kwa kufanywa ngoma kila wakati

Labda niongezee hapa, taka ni MALI, tuihusishe kikamilifu sekta binafsi hasa investors toka nje, tena wapo hasa toka Korea Kusini, shida ni huu URASIMU wa viongozi wetu, wasiotaka kwenda na nyakati, wapeni wawekezaji sahihi tupate kodi, umeme na hata ajira,.. cha kushangaza sasa, nimewahi ongea na hao baadhi ya investors, wansema sisi tunazaliza malighafi ya taka kidogo ,ndio maana wanashindwa kuleta mitambo mikubwa, alitolea mfano taka za dampo la Muriet, akasema zile taka pale ni kidogo, anauwezo wa kuleta mtambo ambao ili ulete tija inabidi taka zote za mkoa wa Arusha, Manyara na Kilimanjaro ziletwe pale ili kuzalisha UMEME na hata mbolea ..kwa hiyo sisi bado tunazalisha taka kidogo shida tu hatuna viongozi na miundombinu sahihi

La pili , wakandarasi wanaopewa hizo tenda ni kweli wana SIFA?..wana magari,rasimali fedha,rasilimali watu? au mtu akiwa diwani or kiongozi wa chama chakavu, au chawa basi ndio tiketi ya kuzawadiwa tenda?

Tatu, jamii inaelimu ya kutosha kwamba TAKA ni MALI?..kuna haja gani ya kupeleka taka OZA dampo wakati unaweza kuzitumia hapo nyumbani kwa kuzalilisha mbolea, wana elimu ya kutenganisha taka hapo hapo nyumbani?..vifaa je, wanavyo?...wanafaidika vipi (incentives) na hao wanaokusanya taka OZO toka kwao(majumbani)
Halmashauri zetu zina miundo mbinu ya kutosha ya kutenganisha taka katika masoko na hata madampo yetu? , na hizi taka kupelekwa kuweza kutumiwa kwa shughuli zingine za kiuchumi mapema kupitia vituo rejeshi (wastes re-use n recycles centres)..
ELIMU YA KWAMBA TAKA NI MALI INAHITAJIKA SANA KWA JAMII , HALMASHAURI NA HATA WAWEKEZAJI HASA WA NDANI
 
Waste management Bongo land mtihani sana, NEMC safari za nje huwa mnaenda kujifunza nini.

🚮
 
Suala la takataka nishapiga kelele kwenye platform lakini hakuna kinachofanyika. Tunazalisha taka kiasi si kama wenzetu lakini tumeshindwa kabisa waste management. Sijui tungekuwa tunazalisha taka nyingi kama wenzetu hali ingekuwaje?

Si bure Mungu alisahau kutia akili kwa watu weusi. We are the worst of his creation.
 
Back
Top Bottom