Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Wizkid

Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Wizkid

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Tangu kutangazwa kwa majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo mwaka huu, Wizkid hakuwahi kusema chochote. Alikuwa kimya tu utadhani hakuna kinachoendelea licha ya kuwepo kwenye vipengele vingi.

Hakuwa na muda wa kusema ‘thanks for the nomation.’ Hakuwa na hata muda wa kusema ‘jama eeh, mwenzenu nimetajwa kwenye MTV MAMA hebu nipigieni kura.’ He didn’t give a damn! Si ajabu lakini kwasababu ni kawaida yake bwa’mdogo huyu. Yeye tuzo huziona kitu cha kawaida, mpe sawa, mnyime, fresh tu!

Ehh! Jumamosi kaibuka na tuzo nne, kawa ‘man of the night.’ Unadhani ni kura ndizo zimempa ushindi wa tuzo zote hizo? Napata tabu kuamini. Msanii mmoja mkubwa sana ameniambia, namnukuu: Sometimes KURA zinapotosha. Watu wamepiga kazi nzuri ila kura zinapick wengine.”

Anachomanisha kuwa, msimamo wa Wizkid kutojishughulisha na kusema lolote kuhusu tuzo, kunaweza kukawa kulimfanya asipate kura nyingi kihivyo, lakini ukweli ni kwamba, hakuna msanii Afrika aliyefanya makubwa kumzidi Wizkid mwaka huu.

Alishirikishwa kwenye wimbo ‘One Dance’ wa Drake ambao umeweka rekodi kibao ikiwemo ya kusikilizwa mara bilioni 1 kwenye mtandao wa Spotify na kuwa wa kwanza kuwahi kuvutia namba hizo. Wizkid amefanya kazi na Chris Brown, Trey Songz, French Montana na wasanii wengine wakubwa. Ndio msanii anayefanyia kazi Afrika anayefahamika zaidi kwa sasa Marekani. Hata kama hakuonesha kuzitilia maanani tuzo hizo, ilikuwa ngumu kumkwepa.

Fundisho hapa ni kwamba, wingi wa kura unaweza usiwe na maana yoyote katika kumpata mshindi. Haiko sawa kwa namna yake ndio maana Eddy Kenzo amelalamika. Kwamba kama waandaji wanasisitiza watu wapige kura, lakini waliopigiwa kura nyingi hawapewi ushindi, ya nini kuwaambia watu wapige kura? Ni sawa na kampuni kutangaza ajira na kuwafanyia usaili baadhi ya waombaji huku ikiwa na watu wengine itakaowapa kazi.

Hatuna ulazima wa kujilaumu au kuumia sana au kuushusha muziki wetu. Wasanii waliotuwakilisha wamefanya kazi kubwa na ngumu kuipeperusha bendera ya Tanzania. Tusiwabeze, tuwape moyo na kuwaunga mkono bila kuchoka. Katika kipindi wanachohitaji zaidi support yetu, basi ni hiki.

1477424081148.jpg
 
Usisahau kuwa mwaka jana wizkid alishndwa kwa davido tuzo hizo hizo za MTV MAMA
Usisahau mwaka huu mwez wa 7 wizkid alishndwa kuchukiwa tuzo ya BET, tena akapata Black Coffee sjui au black belt wa south afrika kama sjakosea.
Wizkid asipo pata tuzo kwake ni poa, akipata pia kwake ni poa, ila amefocus na kazi zaidi, pia tujifunze kuwa hakuna mtu ambaye huchukia kila tuzo tena kila mwaka au huchukua tuzo milele tuzo ni kama pesa hutoka kwa huyu na kwenda kwa mwingine, hivo lazima wasanii wa bongo na wote walio kosa maisha yaendelee wafanye kazi, majungu waziachie timu zao hiyo kaz itafanywa.
Tujifunze kwa wizkid fanya kazi, zamu yako kesho itafika.
*Zamu ya nani leo!!?, zamu ya wizkid
 
Ila sasa na msanii ukiona unaisha mwaka mzima hujapata hata tuzo za vichochoroni ni shda nyingine hiyo. Hapo jitafakari lazma mziki wako una shida. Maana duniani ziko tuzo nyingi sana kwa kweli, haiwezekani upige kazi ifanye poa halafu ukose hata moja ya kizushi.
 
Mkuu unakumbuka kwenye ile clip aliyohojiwa Kenya Sallam Sk alisema yeye hakuzima mic bali alivyosikia sikia "eti Alikiba na Wizkid walikuwa na ubishani nani apande stejini wa kwanza" kwamba Alikiba ni mkali kuliko wizkid

Ni kweli huo uzushi hapo juu hizo tetesi zipo au Sallam sk alikuwa anatudanganya[emoji115]
(Najua unamkataba na WCB mkuu[emoji1] )
 
Hahahaha
Eeh bhana, naskia Sallam hata kwenye ile suti ya Ali Kiba oversize wakat ina shonwa alikuwa nyuma ya fundi karibu na cherehan aka chomoa uzi ndio maana ikakosewa vipimo.
Mimi simchukii Kiba kabsaaa ni shabiki tu wa domo zaid kuliko yeye, lakini hata Kiba akitoa mziki wake, hata hapa naskiliza wimbo wa usiniseme.
Basi hivi juzi juzi, kulikuwa na shughuli
Mtaa wa pili tena si mbali, kulikiw na pilau nawali, basi na mi nikajiunga.....[emoji444] [emoji444] [emoji444] [emoji444]
 
Ila sasa na msanii ukiona unaisha mwaka mzima hujapata hata tuzo za vichochoroni ni shda nyingine hiyo. Hapo jitafakari lazma mziki wako una shida. Maana duniani ziko tuzo nyingi sana kwa kweli, haiwezekani upige kazi ifanye poa halafu ukose hata moja ya kizushi.

Bado tuu Una uteams damuni mwako?
 
hahahaaaa Aisee uteam utakuua ndugu yangu, punguza chuki kuwa free soul
 
Watu wanadhani kukosa tuzo dhambi
Wizkid alikosa sana, kama BET hadi leo hawaelewan naye kwa sabab ya mambo hayo
Ila wizkid alishachukua bet 2012 kama skosei ila aliwamind sababu ya kutoa tuzo backstage... Inshort wizkid hana uhaba wa tuzo hata kidogo tuzo ambazo alikua hajapata ni MTV na sasa kapata.... Sku zote ukifanya bidii mafanikio yanakufuata tuuu
 
Ila sasa na msanii ukiona unaisha mwaka mzima hujapata hata tuzo za vichochoroni ni shda nyingine hiyo. Hapo jitafakari lazma mziki wako una shida. Maana duniani ziko tuzo nyingi sana kwa kweli, haiwezekani upige kazi ifanye poa halafu ukose hata moja ya kizushi.
ha haaaa haaaaa ulipuliza comment ya juu, naona ukaona haitoshi uje ung'ate tena...lol
Umenifurahisha kweli mkuu
 
Ila wizkid alishachukua bet 2012 kama skosei ila aliwamind sababu ya kutoa tuzo backstage... Inshort wizkid hana uhaba wa tuzo hata kidogo tuzo ambazo alikua hajapata ni MTV na sasa kapata.... Sku zote ukifanya bidii mafanikio yanakufuata tuuu
Upo sahihi ila naamini hata mwaka huu alistahili apate BET ila walimpa Black beauty cjui
2013/2015 pia alipaswa apewee yeye vile vile
 
ha haaaa haaaaa ulipuliza comment ya juu, naona ukaona haitoshi uje ung'ate tena...lol
Umenifurahisha kweli mkuu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ebu Acha kunigombanisha na wananchi
Uchochezi huo sasa
 
Niliwahi kusema kua Star Boy ununda wake ipo siku utamsaidia naona yanatokea jamaa aliwahi kusema kua thamani ya muziki wake haipo kwenye hizi awards ila route za kwenda bank kuweka sarafu hapa tukisema Wizkidayo ni mkubwa Africa kwani aliyoyafanya inabidi wadogo zetu waige utaambulia kutukanwa kisa tuna nyimbo zetu na viewers mil 5 Yotube
 
Back
Top Bottom