Tuna mtoto wa miezi saba, mke wangu mjamzito. Ushauri pliiiz!

Tuna mtoto wa miezi saba, mke wangu mjamzito. Ushauri pliiiz!

Naomba MUNGU msipate mawazo ya kuitoa tu...maana ni dhambi kubwa sana....fuata ushauri wa wadau na mambo itakuwa poa tu........
 
Illovo

Kanisani wamegeuka madaktari, hospitali hakuna kilombero? Hawa wamama ndio maana wanapigwa miti hovyo na viongozi wa makanisa👿 matatizo ya ndani kwako unampeleka kanisani ili iweje?

Nirudi kwenye mada. Hili sio tatizo lingekua kwangu ningefurahi maana watoto watakua pamoja. Biashara ya kuzaa na kukaa mpaka mtoto aombe mdogo wake haipendezi. Mtoto anyonye tu hakuna madhara, doctor atawashauri lini aache kunyonya.
Mama ale vyakula vya kumpa nguvu, doctor pia anaweza kuwashauri. Hamna sababu ya ku panic.

Ilovo;
Ni kanisa gani tena hilo?? Jamani, sasa mtamwambia huyo Mungu awape sababu za kuwa wanawake au?? Umeenda kulia shida unaongezewa shida! Unajua hakuna shida kubwa kama kipigwa mti huku huutaki?? Poleni mliofikwa.
Back to the topic;
Hilo wazo la kukung'uta mapema unapata nafasi ya kupumzika mapemaaaa. Mama anabaki na shape yake ya usichana kabisa. Wangu is now 50 lakini akisimama na watoto wake, wao ndo wanapewa shkwamoo
 
mtoto aendelee kunyonya tu bla tatz mpka mama atakapo tmza miez 9 haina shaka
 
Mkuu,

Usiumize kichwa, acha stori za mtaani. Mimi ni shuhuda namba moja wa hiyo kitu, wakati mwanangu wa kwanza akiwa na miezi 6,waifu alishika ujauzito wa mwanetu wa pili. Tulichanganyikiwa kidogo lakini baaada ya kupata ushauri wa wataalam na kuufuata, leo hii tuna watoto wawili, yule wa kwanza wa kiume na huyu wa pili wa kike.

Mwanetu wa kwanza alinyonya kama kawaida hadi alipofikisha umri wa mwaka mmoja ndio tukamuachisha. Kitaalamu ni kwamba atleast huyo wa pili aachiwe ziwa miezi mitatu kabla. So,wanetu wapo na wana afya sana. Tatizo ni kwamba tu mimba imekuja pasipo matarajio hivyo mjiandae na malezi dabo dabo,lakini mengineyo yote shwari kabisa.

Malezi dabo sio kesi, fanya km mapacha.. Kamabmapacha wanaleleka poa haya hao sio kesi
 
pamoja na yote uliyoshauriwa pia usirudie tena hilo kosa
 
Wanaume mkiambiwa Condom kupanga uzazi HAMTAKI eti nitatumiaje condom kwa mke wangu, kwani ni kila siku??????

Hapo mlee mimba tu mtoto azaliwe.
 
Back
Top Bottom