Tuna watoto 4, wote kwa operesheni, mimba ya 5 (na mke alishafunga kizazi)

Tuna watoto 4, wote kwa operesheni, mimba ya 5 (na mke alishafunga kizazi)

Jaribu kutafuta daktari bingwa akushauri ukiamua kwa haraka kinaweza kula kwako.
 
Pole sana.muhimu ni kutafuta ushaur wa kitaalamu hospital nyingine kubwa.na iman utapata tu ufumbuzi. Muombe sana Mungu atakusaidia.mimi wazaz wangu walinipata kwa njia kama iyo.ujauzito wangu uligundukila ukiwa na miezi 7.mama alikuwa anahisi ni uvimbe tu coz alishafunga kizazi.alipata ushaur mzuri hadi ni kazaliwa.tafuta ushaur wa haraka kwa madaktari bingwa then fanya watakavyokushauri.pole mno.ila inauma na kuvuruga akili ukijua hukupagwa kuzaliwa.

Now this is very touching yokoshima....anayepanga kuzaliwa kwako ni Mungu pekee
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kama unapesa ingia bondeni hapo kwa madiba wataokoa vyote vi2
 
nakushauri onana na madaktari bingwa wa maswala ya uzazi watakusaidia lakini zaidi muombe mola amjaalie ajifungue salama nae Mungu atajibu maombi yako!
 
Ni tatizo la maisha,maana daily utakuwa unapambana kuonyesha Mungu alipanga niwepo.AMEN

Okay hiyo approach ni nzuri..nanin fact kila mmoja anajustify uwepo wake kwa namna moja au nyingine...so we move on....na sio tatizo kabisa
 
Habari wadau,
"mimi na mke wangu tuko kwenye ndoa mwaka wa 17 sasa na tumejaaliwa kupata watoto wanne wote wa kike. kutokana na uzazi wa mke wangu kujifungua kwa operesheni mara kwa mara madaktari hosp ya mwana nyamara walitushauri kuwa mke wangu afunge kizazi kwani mimba zaidi ya nne kwa operesheni itahatarisha uhai wake na mtoto pia endapo ataendelea kuzaa. kweli tulikaa na mke wangu japo tulitaka kuendelea kuzaa walau tupate mtoto wa kiume tukaona ni vizuri kufuata ushauri wa madaktari na kufanya kama walivyotushauri kwa kufunga kizazi.
mwezi na siku na kadhaa zilizopita mke wangu alijisikia vibaya atukutilia maanani sana japo dalili zilikuwa ni za ujauzito kwani tuna miaka minne toka alipojifungua na kufunga kizazi, lakini hali hiyo iliendelea mpaka tulipoenda hospitali na kugundulika ana ujauzito wa miezi 3 na manesi walisema tayari hiyo mimba ni kubwa na kutokana na mishono aliyoshonwa tayari ni tatizo na kwa kifupi haitawezekana kujifungua salama eidha mtoto afe mama apone au mama afe mtoto apone
nilipopata hizi habari nilishtuka na kuhuzunika sana.
nakuja mbele yenu wanajamvi mnipe ushauri mwenye uzoufu na masuala kama haya naamini kabisa inawezekana madaktari hawakufanya kazi yao ipasavyo katika kufunga kizazi lakini tayari tatizo limeshatokea, je tuuwe kiumbe au kilichopo tumboni au tufanyaje?"
ushauri tafadhari.
Pole sana Brother! Cha muhimu okoa mama ili uweze kulea hao watoto wanne pamoja naye vinginevyo utaishi maisha magumu baada ya hapo! Hakuna njia nyingine zaidi ya hii utakayoshauriwa na madaktari!
 
Watu 8 naomba useme kitu....
 
Last edited by a moderator:
Kaka imesema aisee Dr. Kamugisha aliokoa maisha yangu ilikua nife mimi na mtoto.

Kamuone Dr. Kamugisha atakusaidia. Yupo muhimbili
 
Habari wadau,

Mimi na mke wangu tuko kwenye ndoa mwaka wa 17 sasa na tumejaaliwa kupata watoto wanne wote wa kike.

Kutokana na uzazi wa mke wangu kujifungua kwa operesheni mara kwa mara madaktari hospitali ya mwananyamara walitushauri kuwa mke wangu afunge kizazi kwani mimba zaidi ya nne kwa operesheni itahatarisha uhai wake na mtoto pia endapo ataendelea kuzaa.

Kweli tulikaa na mke wangu japo tulitaka kuendelea kuzaa walau tupate mtoto wa kiume tukaona ni vizuri kufuata ushauri wa madaktari na kufanya kama walivyotushauri kwa kufunga kizazi.

Mwezi na siku na kadhaa zilizopita mke wangu alijisikia vibaya atukutilia maanani sana japo dalili zilikuwa ni za ujauzito kwani tuna miaka minne toka alipojifungua na kufunga kizazi.

Lakini hali hiyo iliendelea mpaka tulipoenda hospitali na kugundulika ana ujauzito wa miezi 3 namanesi walisema tayari hiyo mimba ni kubwa na kutokana na mishono aliyoshonwa tayari ni tatizo na kwa kifupi haitawezekana kujifungua salama eidha mtoto afe mama apone au mama afe mtoto apone
nilipopata hizi habari nilishtuka na kuhuzunika sana.

Nakuja mbele yenu wanajamvi mnipe ushauri mwenye uzoufu na masuala kama haya naamini kabisa inawezekana madaktari hawakufanya kazi yao ipasavyo katika kufunga kizazi lakini tayari tatizo limeshatokea, je tuuwe kiumbe au kilichopo tumboni au tufanyaje?"

Ushauri tafadhari.

Nakushauri umuone Daktari Bingwa wa magonjwa ya Akina mama unaweza kupata ushauri mzuri zaidi wa kitaalam. Pole sana mkuu.
 
pole sana mkuu kwa mtihani huo uliokupata...

sacrifice your child for the survival of your children..

kuna vitu vingine ni vigumu sana kuvielezea katika maisha..

Dogo sometime una akili!!
 
Pole sana mkuu kwa yaliyotokea hasa mkeo kupata mimba huku ukiamini walifunga.
......Mambo hayo hutokea ndugu wewe siyo peke yako kwamba madaktari wanafunga mirija halafu mama ana pata mimba,daktari ni binadamu anaweza kukosea kufunga mirija.

......Ni kweli wataalamu walivyokuambia kuwa mama na mtoto wako at risk,lakini hakuna gurantee ya kwamba lazima mama au mtoto afe.mimi risk ninayoona hapo ni kuwa kwa kuwa mfuko wa uzazi umeshashonwa mara nne ni kweli kuwa ukubwa wake umepungua,na hivyo kupunguza nafasi ya mtoto kukua vizuri,au kukua mpaka kufikia muda uliotarajiwa kwa hivyo mtoto atakayezaliwa (kwa operation) atakuwa mdogo sana,au atakuwa njiti(premature)yaani kuzaliwa kabla ya muda wake.

....Hatari kubwa ninayoiona kwa mama ni kuwa kama mimba ikikua mpaka kufikia muda wa kuzaa na uchungu kuanza uwezekano wa mfuko wa uzazi kupasuka ni mkubwa hapo hatari kubwa ni kutokwa damu nyingi inayo hatarisha maisha yake mama anaweza kufa kwa kupoteza damu nyingi,au kutolewa kizazi,na mtoto kufa sababu atakosa damu.

mambo ya kufanya ili kuokoa maisha yao.
......kwenda clinic mara kwa mara kuangalia ukuaji wa mtoto

.....Muda wa kujifungua ukikaribia uende uka book kwa daktari kufanyiwa upasuaji,(elective c/section) kumtoa mtoto ili kuepuka kufika hatua ya mwisho amabapo risk ndo inakuwa kubwa.

......sioni sababu ya kutoa mimba,maana mimba yenyewe itatoka tu kama mazingira hayafai,so kama mazingira ya mimba kukua ni mazuri itaendelea.

.....Muhimu ni kukaa karibu na hosp.zinazoweza kufanya upasuaji muda ukaribiapo.


swali langu kwa wale wanasema itolewe ...kwa nini itolewe? ikiwa atakuwa kwenye huduma nzuri za kihospitali...wapo watu mbona si wa kwanza yeye kupasuliwa mara tano.
 
Ndugu 1 hapo juu amesema kwanini amekuja humu kuomba ushauri mi nadhani hajakosea 7bu kati ye2 humu wapo maDr bingwa ikawa rahisi kupata msaada! Kwaupande wangu tatizo ninaloliona hapo hii familia inatafuta Mtt wa KIUME huenda hiyo MIMBA imeangaliwa ikawa na Mtt wa KIUME so itolewe? issue iko hapo Mama anaweza kuwa tayari itolewe lkn Baba atalidhika? ukichukulia ikitolewa Mama hatazaa tena? Naamini kuna watu wamebobea kwenye hiyo FANI sema sasa ishu ni MFUKO km unaruhusu cdhani km kunakinachoshindikana!
 
Lakini hali hiyo iliendelea mpaka tulipoenda hospitali na kugundulika ana ujauzito wa miezi 3 na manesi walisema tayari hiyo mimba ni kubwa na kutokana na mishono aliyoshonwa tayari ni tatizo na kwa kifupi haitawezekana kujifungua salama eidha mtoto afe mama apone au mama afe mtoto apone
nilipopata hizi habari nilishtuka na kuhuzunika sana.

mkuu pole sana kwa hali ilyokukuta.........

ukiachilia mbali sababu inayoweza kufanya mkeo kupata ujauzito ilihali madaktari walisema wamemfunga kizazi.......mimi nipo interesting na hapo juu......

hii taarifa uliyopewa inauhalisia gani?

usikute unatishwa bila sababu ya msingi.
 
Mathematically, unaweza okoa maisha ya mm ila ya mtoto hujui! So hesabu rahisi ni uwahi kuabort mtoto! Ingawa sio lengo na mungu hapend, ila mungu huwa haangalii machoni anajua ukweli kabla hujasema! So kwa kifupi anajua unavopata shida na hali iliyopo na atakusamehe kwa hilo! Omba mtihani huu uuvuke salama
 
besti na wewe umeamini hayo maelezo ya manesi? ya kuchagua kati ya mama au mtoto?

Yes hun. I am a CS and I know we wouldn't both have made it.

My son is the huge type. At 18 months ananifika kiunoni.... Pata picha.

Am not delving so much into the medical reasoning behind it am just brushing by.
 
Back
Top Bottom