#COVID19 Tunaambiwa na Serikali tuchukue tahadhari ya Corona lakini matukio mengi ya chama na Serikali hayana hiyo tahadhari

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nimemuona Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na mikutano ya hadhara kule Songwe na anakusanya watu wengi tu huku viongozi wakituambia hali ya corona ni mbaya. Je, kuendeleza hii mikutano haiwezi kuwa kitisho kikubwa cha kusambaza hiyo corona?

Ni kwanini CCM isiisitishe hii mikutano ili kuonesha mfano wa kuchukua tahadhari?

Mbali na hizo ziara za CCM kuna mbio za mwenge vyuo na shule ambavyo vyote hukusanya watu wengi na viko ndani ya uwezo kuvifunga ili kuwanusuru wananchi na hilo wimbi?
 
Kiongozi wa nchi hii mi simuelewi kabisa kuhusu hili,. Nimemtafakali sana ila nashindwa kabisa kumuelewa
 
Huyu ndiye msambazaji mkubwa wa maambukizi nchini.

6972ED78-89DC-4318-859A-6F0BAE8B44CC.jpeg

Nimemuona Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na mikutano ya hadhara kule Songwe na anakusanya watu wengi tu huku viongozi wakituambia hali ya corona ni mbaya. Je, kuendeleza hii mikutano haiwezi kuwa kitisho kikubwa cha kusambaza hiyo corona?...
 
Hapa tuna msiba babu yetu amefariki jana na covid. Kesho tunapandisha maiti[emoji26]
Jana aunt yangu amezikwa. Its scary aisee.
 
Macho kumchuzi mkono kuubwabwa pia alikua na ziara ya kikanda pia hilo msijisahaulishe,pamoja na vikao vya chama chake vilikua vikifanyika kwa watu kujazana ndani ya kumbi na sio nje.
 
pole sana kamama kama kweli hali ipo hivi basi kuna hatari kubwa mbelen kwa watanzania
Yes, aunt kafia korogwe tanga. Babu kafia muhimbili. Yaan it means iko kila mahali. Nahofia itatunaliza aisee. Babu siyo mzururaji aisee.
 
Nimemuona Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na mikutano ya hadhara kule Songwe na anakusanya watu wengi tu huku viongozi wakituambia hali ya corona ni mbaya. Je, kuendeleza hii mikutano haiwezi kuwa kitisho kikubwa cha kusambaza hiyo corona?

Ni kwanini CCM isiisitishe hii mikutano ili kuonesha mfano wa kuchukua tahadhari?

Mbali na hizo ziara za CCM kuna mbio za mwenge vyuo na shule ambavyo vyote hukusanya watu wengi na viko ndani ya uwezo kuvifunga ili kuwanusuru wananchi na hilo wimbi?
Mkuu.kwa sasa haiwezekani uache kuendelea na shughuli za kila siku kisa kuna corona....lazima tujifunze kuishi nao huu ugonjwa
 
Yes, aunt kafia korogwe tanga. Babu kafia muhimbili. Yaan it means iko kila mahali. Nahofia itatunaliza aisee. Babu siyo mzururaji aisee.
Sasa hapo cha kumaliza ni nini? mbona mie mwaka juzi kabla ya corona nimefiwa na watu wa karibu ndani ya wiki tu tunazika leo baada ya siku nne tunafiwa tena. Ingekuwa mwaka huu ingesemwa ni corona kwa jinsi vifo vilivyofuatana.
 
Ulisikia ni mashindano juu ya misiba ama? Na hapa hatuongelei misiba iliyopita maana naamini kaskazini maboma mengi sana tumepata misiba mwaka jana na mwaka huu. Huo mwaka juzi unaousemelea wewe ni upi wakati kwetu ni 2020 ndo imeanza onyesha madhara? Anyways, bye
 
Si mlikuwa mnalalamika hamuoni tofauti kati ya chama na serikali, sasa tumeamua kuwaonyesha utofauti, mbona hamridhiki ndugu zangu ?
 
Inasikitisha sana,ngoja tuanze kuokota miili mtaani ndio watie akili
Wewe endelea kuchapa kazi upate kipato cha kuendeleza maisha yako ya baadae, habari za Corona achana nazo. Tatizo mna macho lakini hamuoni, mnajifanya mnajua kumbe hamjui, achana na siasa ya dunia itakupotezea mda wa kukuza uchumi wako.
 
Ulisikia ni mashindano juu ya misiba ama? Na hapa hatuongelei misiba iliyopita maana naamini kaskazini maboma mengi sana tumepata misiba mwaka jana na mwaka huu. Huo mwaka juzi unaousemelea wewe ni upi wakati kwetu ni 2020 ndo imeanza onyesha madhara? Anyways, bye
Hujaelewa kabisa, hata hivyo wasalimie.
 
Nimemuona Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na mikutano ya hadhara kule Songwe na anakusanya watu wengi tu huku viongozi wakituambia hali ya corona ni mbaya. Je, kuendeleza hii mikutano haiwezi kuwa kitisho kikubwa cha kusambaza hiyo corona?

Ni kwanini CCM isiisitishe hii mikutano ili kuonesha mfano wa kuchukua tahadhari?

Mbali na hizo ziara za CCM kuna mbio za mwenge vyuo na shule ambavyo vyote hukusanya watu wengi na viko ndani ya uwezo kuvifunga ili kuwanusuru wananchi na hilo wimbi?
Uzuri wa corona uwe na bomu, bunduki inapita na wewe hakuna namna
 
Back
Top Bottom