Tunaandaa nyaraka za kusajili kampuni kwa Tshs Laki 1 (Memorandum na Articles of Association)

Tunaandaa nyaraka za kusajili kampuni kwa Tshs Laki 1 (Memorandum na Articles of Association)

mkuu sio utapeli,wapo wengi wanaitaji na hawajui pa kuanzia,tusiwe watu wa mtazamo chanya katika kila kitu,au unaona fahari wakenya wanapoishia tanzania na kuanzisha firms na kubeba kazi zetu zote? Si tupo tunakalia kuitana matapeli?badili mawazo ndio mwanzo wa maendeleo.
Tena hao Wakenya mtaji wao ni kuja na kilaptop tu mambo kwishney,baada ya miezi unamuona anatengeneza millions na kukuajiri kuwa mfanyakazi wake,hakika tusiwe watu wa kuwaza kuwa tunatapeliwa tu,nimeona hapa JF hata ukileta jambo la maana unaambiwa tapeli,tukubali ku take risk bila hivyo tutabaki tunaimba wimbo wa ah wewe tapeli,acheni uoga jaribuni kuthubutu
 
Mkuu mbona ukienda kwenye website ya Brela unapata template ya hizo MEMARTS! Hapo una download na kuzi edit kulingana na matakwa yako. Vile vile zipo fomu za kusajiri jina la biashara (business name), changes etc. katika web hiyo!
 
SALAMUU!.... LAKI MMOJA (100,000),AMBAYO .... MOROGORO,KWA ....WANAOITAJI HUDUMA ... MAITAJI

TUNAANDAA ...
Maitaji... laki mmoja .... salamuu... tunaandaa .... wanaoitaji.... duuh!

Robo ukurasa tu makosa chungu nzima, halafu ndio uniandikie mkataba wa partnership ya kampuni wewe kweli? Company Act inasema documents zote za incorporation lazima ziwe filed kwa lugha ya Malkia, sasa wewe mwenzangu na mie ngumbaru wa Kiswahili hata cha kwako hukijui, cha Malkia utaweza kukiandika kweli wewe? Tanzania hakuna wataalam!

 
Nafikiri tusimshambulie huyu mjasiliamali, huduma anayotoa ni kweli inahitajika na watu wengi wanasafa kushughulikia hili. Nafikiri ili uweze kupata wateja wa kutosha ni vyema uka ongeza scope ya huduma unazitoa. Usiishie kuandaa memorundun na article of association tu, bali mteja akija kwako unamwambia nipe a, b,c ,d jaza form hii wweka sahiishii hapa, njoo baada ya wiki 1 au 2 uchukue Registration, TIN, Business license, VAT na kila kitu.

Unatakiwa ujue procedure visuri na ujenge urafiki na wa wa BRELA na TRA ili uwe unapiga faster faster. Pia ni vyema ukawa na fom zote muhimu na maelekezo yaliyorahisishwa ambao mteja akija siku ya kwanza anaondoka na maelezo yote ya msingi na form anaenda kujaza. Akirudisha na kulipa fees, next time anakuja kuchukua mzigo wake.
 
@ndachuwa, kwani kitu kikiwa cheap inamaanisha low quality? Unajidanganya na kama una mawazo hayo kuna vitu vingine utakuwa unalanguliwa. Wafanyabiashara kwenye kuset price wanaangalia costs walizotumia. Wapo ambao huuza bei juu ila quality ndogo ili wapate super normal profit. Wapo ambao wametumia gharama kubwa hivyo bei zao lazima ziwe kubwa hata kama quality ni ile ile.
Pia inawezekana mtoa mada ameset low price ikiwa ni mojawapo ya strategies za kupenetrate kwenye market.
mkuu umeongea kitu sahihi kabisa,wengi hawajui medani ya biashara,kwanza sisi ni consultancy firm kwahiyo tunatoa huduma nyingi zaidi ya hii,na siri kubwa ya kuwa na biashara ya mafanikio ni kuaandaa au kutengeneza wateja wako tangu mwanzo,tunajua hata tukiwapa huduma hii ya usajili wa firms kwa bei nafuu sasa kesho watakua ndi wateja wetu wa judumu wa huduma zetu nyingine!kwani makampuni ya simu yanapotoa huduma za free sms manayake kwamba hayana quality? Wanajua ukifata free sms utanunua line yao na kesho utatumia tena huduma zao,tuamuka wadau wangu.
 
Nafikiri tusimshambulie huyu mjasiliamali, huduma anayotoa ni kweli inahitajika na watu wengi wanasafa kushughulikia hili. Nafikiri ili uweze kupata wateja wa kutosha ni vyema uka ongeza scope ya huduma unazitoa. Usiishie kuandaa memorundun na article of association tu, bali mteja akija kwako unamwambia nipe a, b,c ,d jaza form hii wweka sahiishii hapa, njoo baada ya wiki 1 au 2 uchukue Registration, TIN, Business license, VAT na kila kitu.

Unatakiwa ujue procedure visuri na ujenge urafiki na wa wa BRELA na TRA ili uwe unapiga faster faster. Pia ni vyema ukawa na fom zote muhimu na maelekezo yaliyorahisishwa ambao mteja akija siku ya kwanza anaondoka na maelezo yote ya msingi na form anaenda kujaza. Akirudisha na kulipa fees, next time anakuja kuchukua mzigo wake.

nashukuru sana sana mkuu kwa mawazo yako na ndio maana hapo is home of greter Thinkers,nimeyazingatia mawazo yako na yatafanyiwa kazi ki sahihi kabisa!
 
tena hao wakenya mtaji wao ni kuja na kilaptop tu mambo kwishney,baada ya miezi unamuona anatengeneza millions na kukuajiri kuwa mfanyakazi wake,hakika tusiwe watu wa kuwaza kuwa tunatapeliwa tu,nimeona hapa jf hata ukileta jambo la maana unaambiwa tapeli,tukubali ku take risk bila hivyo tutabaki tunaimba wimbo wa ah wewe tapeli,acheni uoga jaribuni kuthubutu
ni kweli kaka watu hawajui na inauma sana sisi tunakalia kuitana matapeli na wezi bila sababu za misingi,nitakupa mfano sisi wataalamu wa accounting wetu wanalalamika hakuna kazi na wamejaa mitaani,sasa wamekuja wakenya wanazunguka kwenye baa tu za dar wanatoa huduma ya kukukotoa mahesabu na stock ya bidhaa kwa siku na wanatoza tsh 10,000 kwa kira baa na kwa kiwango cha chini wanzungukia mpaka baa 50 kila siku kwani wanatumia softwares rahisi za accounting na wanamaliza kazi baada ya dakika chache tu,sasa chukua 10,000 x 50(bar)= 500,000 kwa siku!fikilia hilo kakaje kwa mwezi 500,000 x 30=15,000,000 million!...na huyu mtu hana staff zaidi ya wawili wanaomsaidia kufanya kazi hii,wana gari 1,laptop 3 hawana ofsi ya jengo zaidi ya kuzunguka na gari lao kwa wateja!leo tunakaa kulaumiana jamani lini tutaamuka? Na kuona opportunity zilizopo?tubadilike walai bila hivyo hata malaika ikiwa rais wa hii nchi maendeleo yatakua ni ndoto kama tukibaki na mawazo haya tulionayo sasa ya kuwaza hasi kwa kila wazo la mtu na kuona yeye anataka kufaidi sana.mungu isaidie tanzania.
 
maitaji... Laki mmoja .... Salamuu... Tunaandaa .... Wanaoitaji.... Duuh!

Robo ukurasa tu makosa chungu nzima, halafu ndio uniandikie mkataba wa partnership ya kampuni wewe kweli? Company act inasema documents zote za incorporation lazima ziwe filed kwa lugha ya malkia, sasa wewe mwenzangu na mie ngumbaru wa kiswahili hata cha kwako hukijui, cha malkia utaweza kukiandika kweli wewe?
Tanzania hakuna wataalam!

mkuu acha mawazo potofu,we unajuaje kama mimi ndio mtaalamu wa kuandaa hizo nyaraka? Hakuna mgawayo wa kazi katika kampuni?usihukumu kwa lugha yangu mimi sio mtaalamu wa kishwahili na lengo lilikua kufikisha ujumbe kwa wadau na sio mashindano ya kulemba lugha,kweli tanzania yetu naililia kama hawa ndio vijana wetu taifa la leo.
 
Not all people go for cheap services. ....

Because the price of anything reflect quality.

My advice to you is that you should advertise what you can do and leave fees for case to case negotiation. I am a selft practitioner too.

Company formation is not not a matter of editing someone MEMARTS and change name alone and proud yourself to be consultant, it requires searching or name clearance with BRELA, obtaining Lawyers signature, having MEMARTS signed by subscribers, presenting the same to BRELA, following with BRELA until Certificate of Incorporation is out.

Nime log business name search application pale BRELA tangu 17/02/2012 nemeambiwa niende tena leo mchana. Huyu consultant anajua hilo sijui?
 
mkuu,wasamee bure.ungesema wa umetoka ulaya au kenye wengekubali,wabongo tunaulimbukeni mpaka mtu atoke nje ya nchi
 
mkuu,wasamee bure.ungesema wa umetoka ulaya au kenye wengekubali,wabongo tunaulimbukeni mpaka mtu atoke nje ya nchi
ndugu yangu nashukuru sana na hakika inabidi kusameheana na ndio kuelimishana kwenyewe,ila kweli mimi inaniuma sana nchi yetu tunakua masikini kwa kuwaabudu watu wa nje,wanakuja hapa hawana elimu walai chochote cha kutuzidi muda mfupi wanaondoka na mamilioni sisi tunabaki kutoleana kejeli na dharau,kweli inabidi tuamuke na tupambane sote pamoja,hela zipo tanzania ni kaumuka tu na kupambana,na bila kusahau kuzani kwamba tunajua kilakitu kuliko watu wote.
 
...we unajuaje kama mimi ndio mtaalamu wa kuandaa hizo nyaraka?
Wewe sio mtaalam? Basi unatudanganya kuhusu uwezo wa kampuni yako maana wewe ndio uko hapa una defend kazi yenu, for all we know wewe ndio mtaalam wa hiyo kampuni, kama hii kampuni ikishitakiwa kwa utapeli, kwa mfano, wewe ndio utakuwa wa kwanza kutakiwa kujibu maswali na kusweka lupango maana we ndio the face of the company. Wewe sio mtaalam? Basi unaiharibia kampuni biashara kwa kuwabandikia wafanyakazi wenzio matangazo ambayo hayajaenda shule, inabidi uwe fired!

Unapata free advertisement halafu watu wakiku question unaruika kampuni yako eti wewe sio mtaalam wa hiyo kazi? Hii nchi yetu haina wataalam maskini, sijui kwa nini.


hatutumii template mmoja inakua customized kwa kadri ya maitaji ya mteja na standard format ya brela pia.....
 
wewe sio mtaalam? Basi unatudanganya kuhusu uwezo wa kampuni yako maana wewe ndio uko hapa una defend kazi yenu, for all we know wewe ndio mtaalam wa hiyo kampuni, kama hii kampuni ikishitakiwa kwa utapeli, kwa mfano, wewe ndio utakuwa wa kwanza kutakiwa kujibu maswali na kusweka lupango maana we ndio the face of the company. Wewe sio mtaalam? Basi unaiharibia kampuni biashara kwa kuwabandikia wafanyakazi wenzio matangazo ambayo hayajaenda shule, inabidi uwe fired!

Unapata free advertisement halafu watu wakiku question unaruika kampuni yako eti wewe sio mtaalam wa hiyo kazi? Hii nchi yetu haina wataalam maskini, sijui kwa nini.
safi mkuu kupanga ni kuchagua,subiri mtaalamu kutoka usa aje afungue firm tanzania atakusadia na atakua na hadhi ya wewe kumpa akaufanyie kazi yako,wakati sisi tunaendelea kusonga mbele.tanzania inasikitisha sana.
 
mi niko SINGIDA naendesha mafunzo ya ujasiriamali katika kubuni wazo endelevu la biashara napango wa biashara (business plan) . MCHAKATO WENU NI MZURI TUNAWEZA KUSHIRIKIANA?
 
Kwa Ulimwengu wa Fikra ni dhahir kuwa Mmekomaa,Tatizo ni kwamba wa Tz tu wamaskini,je mnashirikiana na Taasisi yeyote ya Fedha ilikuitumia Rasilimali watu yakutosha iliyopo Nchini ?Tofauti na Hivyo hamtonifaa mimi mwenye Nguvu bila Mtaji..!
 
wadau salamuu!

Tunatoa huduma kwa wajasiliamali wanaotaka kufungua limited company/firm kwa kuwaandalia nyaraka mbili muhimu za usajili nazo ni the memorandum of the company na articles of association.

Gharama ya huduma hii ni tsh laki mmoja (100,000),ambayo pia itaambatana na ushauri wa kitaalamu (consultancy) kuhusu hatua zote za kusajili kampuni:

Tunafanya kazi kwa njia ya mtandao kwa wale walioko nje ya mkoa wa morogoro,kwahiyo tunaweza kukuhudumia popote ulipo tanzania.

Kwa wanaoitaji huduma hii tupe maitaji yako kwa e-mail kulwa12@gmail.com

nb;tunaandaa nyaraka zote hizi kwa siku mmoja tu ya kazi na kwa ufanisi mkubwa.
vipi mkuu kama ni patneship .tunataka partnership deed?
 
WADAU SALAMUU!

TUNATOA HUDUMA KWA WAJASILIAMALI WANAOTAKA KUFUNGUA LIMITED COMPANY/FIRM KWA KUWAANDALIA NYARAKA MBILI MUHIMU ZA USAJILI NAZO NI The Memorandum of the company na Articles of Association.

GHARAMA YA HUDUMA HII NI TSH LAKI MMOJA (100,000),AMBAYO PIA ITAAMBATANA NA USHAURI WA KITAALAMU (CONSULTANCY) KUHUSU HATUA ZOTE ZA KUSAJILI KAMPUNI:

TUNAFANYA KAZI KWA NJIA YA MTANDAO KWA WALE WALIOKO NJE YA MKOA WA MOROGORO,KWAHIYO TUNAWEZA KUKUHUDUMIA POPOTE ULIPO TANZANIA.

KWA WANAOITAJI HUDUMA HII TUPE MAITAJI YAKO KWA E-MAIL kulwa12@gmail.com

NB;TUNAANDAA NYARAKA ZOTE HIZI KWA SIKU MMOJA TU YA KAZI NA KWA UFANISI MKUBWA.

This is too cheap to be true sophial pita hapa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom