Tunaanza kutengeneza kizazi cha watoto au watanzania wasiojua vizuri kiswahili kama ilivyo kwa wahindi licha ya kuzaliwa na kukulia humu nchini

Kila kitu kina faida na hasara zake.Moja ya faida ya hizi shule za kisiasa ni watoto kujua lugha ya malaika angali wakiwa na umri mdogo na kuwa fluent tofauti na wale wanaosoma shule za St. Kayumba.

Hata hivyo, kuna kasoro naiona na ambayo baada ya muda, tutakuja kuiona huko mbele na hii si nyingine bali ni kuwa na kizazi cha watanzania wasioweza kujieleza vizuri kwa kiswahili bali kingereza huku lugha zetu za asili zikiendelea Kopotea kabisa.

Kwanini nasema hivi?

Mazingira wanayokulia watoto wetu wa leo ni tofauti sana na yale tuliokuia sisi.Siku hizi humu mijini kila mtu akijenga nyumba yake anajitahidi kuweka uzi wa ukuta na geti na matokeo yake watoto wetu hawachezi tena pamoja mitaani kama enzi zetu ambapo tukitoka shule, tunakutana mtaani tunacheza pamoja then kigiza kikianza kuingia tunarejea majumbani.

Nini kinatokea?

Watoto wetu hawa wa leo wakiwa katika hizi shule za kisiasa, ni kuongea kingereza mwanzo mwisho tangu wanapoanza shule tena siku hizi wakiwa na umri mdogo (wanamaliza darasa la saba wakiwa na miaka 12 mpaka 13) na wakirudi majumbani ni kufungiwa kwenye mageti mpaka kesho yake tena watapoenda shale.

Athari inajitokezaje?

Watoto hawa tangu wakiwa wadogo,wana-spend muda mwingi shuleni wakiongea kingerez na wakirudi nyumbani wanafungiwa kwenye magoti na hawapata nafasi ya kuchanganyikiwa na wenzao wa St.Kayumba walioko mtaani, hivyo hawakutani na watoto wenzao wanaozungumza kiswahili na matokeo yake wanakuwa wakijua kuongea zaidi kingereza kuliko kiswahili.

Mazingira haya wanaokulia na kulelewa yanafanana na mazingira wanayozaliwa na kukulia wahindi ambao licha ya kuzaliwa na kukulia humu nchini, wanakuwa hawawezi kuzungumza kiswahili fasaha kwani muda mwingi wanatumia lugha yao na kingereza wanachofundishwa.

Na katika hili, bora hata wahindi kwani mbali na watoto wao kufundishwa lugha ya kingereza, bado wanatumia zaidi kihindi katika mawasiliano yao huku sisi hata wazazi wakiendeleza matumizi ya lugha ya kingereza kwa watoto wao wawapo majumbani na kuona huku ndio kustaarabika.

Kujua kingereza ni muhimu kwasababu hiyo ni lugha ya kimataifa ambayo watoto wetu wataitumia kuombea ajira na kushindana na wenzao kimataifa na pia wataitumia kwa mambo mengine but not to this extent ya kuanza kusahau kabisa lugha yetu ya Taifa.

Tuchukue hatua na mojawapo iwe kuongea na kuandika lugha ya kiswahil kwa ufasaha kama ni added advantage kwenye usaili wa ajira za serikali huko mbeleni iwapo hali hii itafikia hatua mbaya.

Mnaweza msinielewa sasa hivi, ila miaka 15 mpaka 20 ijayo, hali hii itakuwa wazi kabisa, na mpaka sasa teyari kuna watoto ambao wako fluent zaidi katika kuongea kingereza kuliko kiswahili.

Usisahau hata mchicha ulianza kama mbuyu.

Tutakuja tena kulaumu wazungu kwa kuua lugha yetu kama ambavyo leo hii tunawalaumu kwa kuua utamaduni wetu.

Alietuloga alikuwa fundi!!
Leo kwa mara ya kwanz nime-like post yako.
Kumbe upo vizuri kichwani, lissu alitaka kukuharibu. Bora JPM alimfurumusha angeendelea kuharibu akili za vijana wengi kama nyie
 
Shule za kisiasa au kisasa umeharibu uzi mzima kwa kutokuwa makini kwenye spelling
[/QUOTE]
Simu hizi zinachangia sana kwani zina-type automatically kadri unavyo-type na uki-post bila kuona matokeo ndio hayo.
 
Hivyo wewe unajua Tanzania ni Dar es Salaam pekee? Comment yako inadhihirisha namna exposure yako ilivyo finyu..

Hata kwa hao wazungu wanazo hizo lahaja.

Maarifa sahihi huja kwa lugha sahihi. Napendekeza tufumue mtaala wetu uwe ni kiswahili mwanzo 'mwenga'
Wewe hujui English ! Jielimishe kwani dunia haiwezi kukusubiri wewe na Kiswahili chako hicho! Technologia inakwenda kwa kasi mno na English ndio " Kiswahili " cha Dunia hii.
 
Leo kwa mara ya kwanz nime-like post yako.
Kumbe upo vizuri kichwani, lissu alitaka kukuharibu. Bora JPM alimfurumusha angeendelea kuharibu akili za vijana wengi kama nyie
Tuweke siasa pembeni.
 
Hii sio ligi!
Sio ligi lakini kama hujui kitu kaa kimya kuliko kuleta upupu wako kwenye public domain.Wewe unadhani kutotamka maneno kwa ufasaha kwenye lugha basi hakuna shida! Ni shida kubwa sana.
Watanzania wengi hamjui Kiingereza wala Kiswahili ila mnatumia tu kichaka cha kukuza Kiswahili ili kuficha udhaifu wenu! Jifunzenu kutafuta maarifa zaidi ! Kujua lugha ya Kiingereza haikuzuii kujua au kujifunza pia Kiswahili fasaha!
 
Mkuu wanafunzi wa shule za serikali asilimia 90 wana maadili mabovu na mawazo potofu mimi ninajua ninachokiandika.
Na kama mtoto hajitambui lazima naye apotee.
Sasa ukitaka mwanao aharibike mchanganye na hao watoto wa mitaani then ulete mrejesho.

Achana na wao kutokujua kiswahili.
Asilimia 10 ya watanzania ndio wanatumia Kiswahili kama main language wengine 90% wanatumia kama second language na hawawezi kutumia vizuri hicho Kiswahili.
Pia Tanzania kuna lugha zaidi ya 100 unadhani kwanini Kiswahili hakijafutika tangu kipindi hicho?
Sasa English ni kitu gani kati ya hizo lugha 100?

Pia umesema wanafunzi wa shule ya msingi wanatumia Kiswahili.
Sasa kama kumbe wapo watu wanaotumia Kiswahili iweje kifutike?

Na kama unataka maisha yako yote ujifungie Tanzania basi ukos sahihi usijifunze lugha za mataifa mengine.
Na umesahau kwamba Tanzania kila kitu kwa asilimia nyingi ni English ndio inatumia hapo ondoa secondary school ambayo ukiondoa Kiswahili basi masomo yote ni English.

Pia Hakuna kitu kama hicho na hakijawahi tokea in centuries kwamba ukitumia na kujifunza lugha nyingi basi utasahau mother language.
Unaweza ukaniambia kwanini kuna watu wanaweza kutumia lugha zaidi ya 5 kiufasaha?
Na Kwanini wasisahau hizo lugha nyingine walizojifunza?

Au Leta ushahidi kuprove hoja yako.
 
Kila kitu kina faida na hasara zake.Moja ya faida ya hizi shule za kisasa ni watoto kujua lugha ya malaika angali wakiwa na umri mdogo na kuwa fluent tofauti na wale wanaosoma shule za St. Kayumba.

Hata hivyo, kuna kasoro naiona na ambayo baada ya muda, tutakuja kuiona huko mbele na hii si nyingine bali ni kuwa na kizazi cha watanzania wasioweza kujieleza vizuri kwa kiswahili bali kingereza huku lugha zetu za asili zikiendelea Kopotea kabisa.

Kwanini nasema hivi?

Mazingira wanayokulia watoto wetu wa leo ni tofauti sana na yale tuliokuia sisi.Siku hizi humu mijini kila mtu akijenga nyumba yake anajitahidi kuweka uzi wa ukuta na geti na matokeo yake watoto wetu hawachezi tena pamoja mitaani kama enzi zetu ambapo tukitoka shule, tunakutana mtaani tunacheza pamoja then kigiza kikianza kuingia tunarejea majumbani.

Nini kinatokea?

Watoto wetu hawa wa leo wakiwa katika hizi shule za kisiasa, ni kuongea kingereza mwanzo mwisho tangu wanapoanza shule tena siku hizi wakiwa na umri mdogo (wanamaliza darasa la saba wakiwa na miaka 12 mpaka 13) na wakirudi majumbani ni kufungiwa kwenye mageti mpaka kesho yake tena watapoenda shale.

Athari inajitokezaje?

Watoto hawa tangu wakiwa wadogo,wana-spend muda mwingi shuleni wakiongea kingerez na wakirudi nyumbani wanafungiwa kwenye magoti na hawapata nafasi ya kuchanganyikiwa na wenzao wa St.Kayumba walioko mtaani, hivyo hawakutani na watoto wenzao wanaozungumza kiswahili na matokeo yake wanakuwa wakijua kuongea zaidi kingereza kuliko kiswahili.

Mazingira haya wanaokulia na kulelewa yanafanana na mazingira wanayozaliwa na kukulia wahindi ambao licha ya kuzaliwa na kukulia humu nchini, wanakuwa hawawezi kuzungumza kiswahili fasaha kwani muda mwingi wanatumia lugha yao na kingereza wanachofundishwa.

Na katika hili, bora hata wahindi kwani mbali na watoto wao kufundishwa lugha ya kingereza, bado wanatumia zaidi kihindi katika mawasiliano yao huku sisi hata wazazi wakiendeleza matumizi ya lugha ya kingereza kwa watoto wao wawapo majumbani na kuona huku ndio kustaarabika.

Kujua kingereza ni muhimu kwasababu hiyo ni lugha ya kimataifa ambayo watoto wetu wataitumia kuombea ajira na kushindana na wenzao kimataifa na pia wataitumia kwa mambo mengine but not to this extent ya kuanza kusahau kabisa lugha yetu ya Taifa.

Tuchukue hatua na mojawapo iwe kuongea na kuandika lugha ya kiswahil kwa ufasaha kama ni added advantage kwenye usaili wa ajira za serikali huko mbeleni iwapo hali hii itafikia hatua mbaya.

Mnaweza msinielewa sasa hivi, ila miaka 15 mpaka 20 ijayo, hali hii itakuwa wazi kabisa, na mpaka sasa teyari kuna watoto ambao wako fluent zaidi katika kuongea kingereza kuliko kiswahili.

Usisahau hata mchicha ulianza kama mbuyu.

Tutakuja tena kulaumu wazungu kwa kuua lugha yetu kama ambavyo leo hii tunawalaumu kwa kuua utamaduni wetu.

Alietuloga alikuwa fundi!!
It's good and fine
 
Back
Top Bottom