Tunadekezwa, tunajua sote madhara ya deko

Tunadekezwa, tunajua sote madhara ya deko

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,521
Reaction score
4,381
Kuna Mmarekani Mmoja anaitwa Steve Harvey aliwahi kusema kuwa Success is the very uncomfortable process to attempt alimaanisha kuwa mafanikio yanahitaji hofu, yanahitaji pressure yanahitaji kukosa raha yanahitaji kila Aina ya internal and external forces.

Binadamu yeyote anayejaribu kushusha hasira za Mapambano ya kuutesa mwili na roho huyu amekosea. Ni hatari sana tena sana kwa Rais wa nchi yeye kujipambanua madhaifu yake mbele ya umma kiongozi popote pale usizoeleke lazima uwe mkali, mfariji kuwalinda wema dhidi ya makatili.

Tunadekezwa
 
Mbona shetani mnywa damu akumfariji lissu alipopigwa risasi kadhaa?
 
Eti anadai atakua anawalea, ila jaman watanzania safari hii tumepata kichekesho
 
Nani kakwambia sio mkali? Yeye hataki kuogopwa kwa hofu na wala hajajishusha. Wanaodhani amejishusha na wafanye.
 
Mtaimba nyimbo zote safari hii.Mlianza na lizombe,kiduo,msusumio,maswezi,chagulaga,mbina,sensemamalunde,njuga na mtamalizia na igembe nsabho![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mbona kama ni wewe mwenyewe ndiye unayeimba hizo nyimbo hapa JF [emoji848][emoji1787]
 
Unajua tulishazoeshwa kwamba ukimbishia Simba wa Burigi umekwisha.

Watu walishazoea kusikia flani yupo Mahabusu na anatakiwa kufanya plea bargain ya million 100 achiwe.

Kutekwa na kupotezwa watu hapo sizungumzii.

Utakuta huyu mtoa mada alikuwa kikosi kazi. Sasa hivi hana kazi anakuja kujaza serva za JF.

Kikosi kazi walikuwa wanauwezo hata wa kupata million moja kwa siku na kuipeleka nyumbani.

Wengi wao wanategemea mshahara tuu sasa hivi. Lazima wapige kelele
 
Kuna Mmarekani Mmoja anaitwa Steve Harvey aliwahi kusema kuwa Success is the very uncomfortable process to attempt alimaanisha kuwa mafanikio yanahitaji hofu, yanahitaji pressure yanahitaji kukosa raha yanahitaji kila Aina ya internal and external forces.

Binadamu yeyote anayejaribu kushusha hasira za Mapambano ya kuutesa mwili na roho huyu amekosea. Ni hatari sana tena sana kwa Rais wa nchi yeye kujipambanua madhaifu yake mbele ya umma kiongozi popote pale usizoeleke lazima uwe mkali, mfariji kuwalinda wema dhidi ya makatili.

Tunadekezwa

Ni kawaida ya wapambe wa mtawala kutamani kuwatangazia “ubatizo wa moto” watawaliwa hata pasipostahili.

Utawala wa kistaarabu unaweka mazingira yenye vivutio (incentives) kuhamasisha ubunifu, ujasiriamali na maendeleo kwa ujumla. Muulize Steve Harvey aliyewekeza kwenye soga/uchekeshaji akuambie siri ya maendeleo nchini kwake. Kuchekesha tu kajituma na kuwa milionea (US$).

Silicon Valley na NASA, kwa mfano, wanavutia na kukaribisha best brains toka pande zote za dunia kuja kupambana na changamoto za kiteknolojia. Bidhaa kali zinazalishwa bila foka foka, vitisho, utekaji, mateso wala mauaji.

Ndio maana tuna mashaka CCM imebakia na mbinu ya kutawala kikomunisti tu staili ya Stalin/Putin. That’s obsolete.
 
Back
Top Bottom