FestoKaguo
Senior Member
- Apr 1, 2022
- 128
- 202
Tumekuwa tukisikia habari au taarifa nyingi sana kuhusu cryptocurrency na blockchain. Neno Bitcoin limekuwa likitawala kwenye vinywa vya wengi, hususan vijana na wafuatiliaji wa teknolojia, lakini hadi sasa, bado ni watu wachache sana walioelewa kikamilifu maana na matumizi halisi ya teknolojia hii – hususan katika upande wa biashara. Kwa wafanyabiashara wadogo nchini Tanzania, hoja ya kutumia crypto kama njia ya kupokea au kutuma malipo si tu kwamba ni ya kisasa, bali pia inafungua mlango wa fursa mpya zisizopatikana katika mfumo wa kawaida wa kifedha.
Changamoto nyingi ambazo zimekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo nchini ni pamoja na ugumu wa kutuma au kupokea fedha kutoka nje ya nchi, gharama kubwa za huduma za benki, ucheleweshaji wa miamala, na masharti magumu kwa wale wasio na akaunti rasmi au miundombinu ya kifedha iliyo rasmi. Katika mazingira haya, teknolojia ya blockchain na matumizi ya cryptocurrency, hususan stablecoins kama USDT, yanatoa suluhisho mbadala linaloweza kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi tunavyoendesha biashara.
Tofauti na Bitcoin inayojulikana ambayo bei yake haiko stable inabadirika mara kwa mara, USDT ni mfano wa "stablecoin". Nikisema USDT kwa lugha nyingine namaanisha hii ni sarafu ya kidigitali au token ambayo imefungwa thamani yake na dola ya Marekani. Hii ina maana kuwa thamani ya dola moja ya USDT ina thamani sawa na dola moja ya kawaida ya Marekani, hivyo ukitumia USDT huwa inasaidia kupunguza hatari ya mabadiliko ya bei yanayoweza kuathiri biashara. Kwa mfanyabiashara wa kawaida, hii inamaanisha unaweza kupokea malipo ya bidhaa zako kutoka kwa mteja wa nje ya nchi au sehemu yoyote ile na kuwa na uhakika kuwa kiasi hicho hakitapungua wala kupanda kinyume na matarajio.
Lakini kwanini crypto ni muhimu hasa kwa biashara zetu za mitaani? Hebu tuchukue mfano wa mama anayeuza vitenge Instagram. Mteja wake kutoka Nairobi au Johannesburg anahitaji kutuma malipo. Kwa kutumia njia za kawaida kama Western Union au mabenki, itamlazimu kulipa ada kubwa, kusubiri siku kadhaa, na wakati mwingine kushughulika na masharti magumu ya benki. Lakini kwa kutumia USDT na kutumia crypto exchanges au wallets kama Trust Wallet, mteja anaweza kutuma malipo hayo ndani ya dakika chache kwa ada ndogo mno (mara nyingine chini ya shilingi 100), na mama anapokea malipo yake papo hapo bila msururu wa masharti, wala ucheleweshaji.
Kubwa zaidi, teknolojia hii haimhitaji mfanyabiashara kuwa na elimu ya hali ya juu labda eti awe amesomea IT au mambo ya Marketing au Banking. Kutumia crypto kunahitaji simu ya mkononi yenye uwezo wa ku-install app, internet, na uelewa wa msingi tu kuhusu jinsi ya kutuma na kupokea pesa. Kuna maelfu ya wafanyabiashara nchini Nigeria, Kenya na Ghana ambao tayari wanatumia njia hizi kuingia sokoni kimataifa. Hili linaweza kufanyika pia Tanzania tena kwa urahisi mkubwa.
Bila shaka kuna changamoto zinazotakiwa kutazamwa kwa makini. Miongoni mwa hizo ni uelewa mdogo kuhusu usalama wa mifumo ya digitali, udanganyifu (scams) unaofanyika kwa kivuli cha crypto, na upungufu wa mifumo ya ndani ya kisheria inayotambua au kudhibiti matumizi ya sarafu hizi. Lakini ukweli unabaki kuwa maendeleo hayawezi kusimama kwa sababu hatujajiandaa. Kinachohitajika ni elimu endelevu, ushauri wa kitaalamu, na hatua za busara za kuanza kutumia crypto katika mazingira yanayodhibitika.
Kwa sasa, kuna jamii kubwa ya vijana na wafanyabiashara wanaotumia njia rahisi kama Binance P2P kubadilisha crypto kuwa fedha taslimu, au kuziuza kwa mawakala wa ndani wanaoaminika. Mfumo huu unatoa uhuru mkubwa mfanyabiashara anaweza kupokea dola za kimataifa kwa crypto, kisha kuziuza kwa TZS na kupata pesa ya kulipa wasambazaji au gharama nyinginezo bila kutegemea benki.
Kwa wale wanaoona hili kama ndoto isiyotekelezeka, ni muhimu kutambua kuwa dunia ya biashara inabadilika kwa kasi. Kuingia kwenye mfumo wa kifedha wa blockchain ni sawa na kuwa sehemu ya mapinduzi ya nne ya viwanda. Ni wakati wetu sasa kuamka na kujiuliza: tutaendelea kuwa watazamaji wa mabadiliko haya, au tutakuwa sehemu ya wale wanaoyaongoza?
Kwa mtazamo wangu, crypto si tu fedha ya kidigitali bali ni fursa. Ni njia ya kuondokana na vizuizi vilivyowekwa na mifumo ya kifedha ya kale. Ni sauti kwa wale ambao hawakuwa na sauti katika dunia ya benki. Kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaotaka kuingia sokoni kimataifa, kukua kwa kasi, na kuepuka mzigo wa ada kubwa za miamala, crypto inapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa kipekee – si kwa woga, bali kwa maarifa.