Tunaelewa kwanini Mwigulu ana hasira na Magufuli hadi leo, na hadi sasa anatoa kauli hasi dhidi yake, na kumwaga maua kwa wingi!

Tunaelewa kwanini Mwigulu ana hasira na Magufuli hadi leo, na hadi sasa anatoa kauli hasi dhidi yake, na kumwaga maua kwa wingi!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Tuongee peupe leo, uwazi na ukweli. Mtu yeyote makini atagundua kwamba karibu kila kauli anazotoa Mwigulu zinalenga kutaka kuonyesha Raisi Samia ni bora sana kuliko alivyokuwa Raisi Magufuli. Tunakiri kwamba kuna baadhi ya mambo Raisi Samia ni bora kuliko alivyokuwa Raisi Magufuli, lakini tuseme kweli, kuna mambo mengi tu Raisi Samia anafanya vibaya kuliko alivyofanya Raisi Magufuli. Lakini hiyo sio topic ya thread hii.

Nataka niwape vitu viwili vikubwa ambavyo vinamfanya Mwigulu hadi leo hii awe na maneno hasi sana kwa Magufuli, (including negative connotations against Magufuli) na kuwa na sifa nyingi sana kwa Raisi Samia. Kwanza ni kwamba Magufuli alimwona Mwiguli kama mshindani wake mkubwa ndani ya CCM, na siku zote Magufuli alitaka kuwaweka kando washindani wake. Magufuli alimwonyesha wazi Mwigulu kwamba hawakuwa marafiki, bali fahari wawili katika zizi moja. Magufuli hakutaka kabisa Mwigulu apate mwanya wa kuonekana ni kiongozi maarufu - ku shine.

Jambo la pili lililofanya labda niseme Magufuli amchukie Mwigulu, ni siku ya tukio la jaribio la kumuua Tundu Lissu. Mara tu baada ya tukio Magufuli alimpigia simu Mwigulu, kama waziri wa mambo ya ndani, atoe tamko kwamba serikali haihusiki na jaribio lile. Mwigulu akasita. Na mbaya zaidi, Mwigulu akaomba ushauri kwa vigogo fulani wa CCM (sintawataja) na wakamshauri asitoe hilo tamko. Hili lilimfanya Magufuli akasirike na amwone Mwigulu ana kiburi, hamheshimu, na hata anadiriki kutotii amri yake kama raisi. Magufuli akawachukia na wale waliomshauri Mwigulu asitoe tamko juu ya jaribio dhidi ya Lissu.

Kwa mnaokumbuka, Magufuli alisema katika moja ya hotuba zake kuna mawaziri wanadiriki kutotii maelekezo yake. Alikuwa akimsema Mwigulu. Na nakumbuka kuna wakati Magufuli alimwondoa kabisa Mwigulu katika Baraza la Mawaziri, kitu ambacho aliona kama kudhalilishwa (naambiwa alinyang'anywa gari ya uwaziri akiwa safarini, sijui kama ni kweli)

Basi kuanzia hapo Mwigulu alikuwa hana raha chini ya uongozi wa Magufuli. Alikuwa ignored, alipuuzwa mara zote, na Magufuli alimfanya Mwigulu awepo bila kuwapo, japo baadae alirudishiwa uwaziri, na inaonekana kwa shingo upande.

Kwa hiyo Magufuli alipokufa, kwa Mwigulu, lahaula! Sintasema mengi zaidi ya kusema heshima ya Mwigulu imerudishwa na Raisi Samia. Ndio maana kila Raisi Samia analotamka au kufanya, Mwigulu atasema tumpe maua yake!!!! Yaani kwa Raisi Samia Mwigulu amezama kweli kweli, line, hook and sinker. Humwambii kitu.

Lakini sasa anapita kiasi. Lazima tumwambie Mwiguli inatosha, awe na kiasi kwa kauli hasi dhidi ya Raisi Magufuli, na kiasi katika kumpa raisi Samia maua kwa kila tamko na tendo katika wajibu wake wa kuwa Raisi wa Tanzania. Raisi Samia anafanya tu kile kilicho wajibu wake, hahitaji mapambio ya Mwigulu kwa kila kitu. It is just too embarrassing kwa watu wenye akili kuona Mwigulu anavyofanya. Undignified kwa waziri mwenye wizara nyeti kama yake.

Nipeni maua yangu kwa kuliweka hili wazi!
 
Si alikuwa waziri wakati wa Magufuli? Si ndie aliepima papai kutwambia lina Covid? Binadam hana fadhila hasa ukiwa mwanasiasa. Akiondoka bi Samia atakuja na mapya kuuponda utawala wake
 
Si alikuwa waziri wakati wa Magufuli? Si ndie aliepima papai kutwambia lina Covid? Binadam hana fadhila hasa ukiwa mwanasiasa. Akiondoka bi Samia atakuja na mapya kuuponda utawala wake
Alikuwa waziri lakini alikuwa na wakati mgumu sana. Nadhani kuna wakati Magufuli alimtema kabisa toka Baraza la Mawaziri.
 
Si alikuwa waziri wakati wa Magufuli? Si ndie aliepima papai kutwambia lina Covid? Binadam hana fadhila hasa ukiwa mwanasiasa. Akiondoka bi Samia atakuja na mapya kuuponda utawala wake
Moyo wa mwanadamu umejaa uovu!
 
Mwigulu huyu huyu alie apishiwa CHATO?
Huyo huyo aliesema Raisi Samia amekuza sana uchumi kwa sababu magari yenye namba za E yako mengi mitaani! Katika siasa usiamini kila kitu unachoona au kusikia toka kwa wanasiasa, pamoja na kuambiwa mafuriko ya Rufiji yamesababishwa na wananchi wenyewe!
 
CCM ni ileile... Ooooooh... Ni ileile...
Watajijua wenyewe...
Na wavimbe wapasukee...
 
Back
Top Bottom