Tunaelewa kwanini Mwigulu ana hasira na Magufuli hadi leo, na hadi sasa anatoa kauli hasi dhidi yake, na kumwaga maua kwa wingi!

Mwigulu ni mtu ambae atakuwa bega kwa bega na wewe mpaka pale chombo kinapoanza kuzama. Ikifika hatua akiona hapa hamna kuchomoka tena atakuwa mtu wa kwanza kuvaa life jacket na kuchukua boya kuruka kutafuta meli nyingine.

Mi hata sioni sababu ya kuangaika kumjadili huyo ropo-ropo kesho ‘bi-tozo’ akitoka Mwigulu akipewa nafasi na huyo raisi mwingine he will do the same thing, si yeye tu na mawaziri wote watakaoteuliwa ndio njia mpya ya ku-survive siasa za Tanzania. Kama uwezi kuonyesha mafanikio inabidi umpambe boss.

Shida ni kwamba awaelewi hizo kauli za kumponda Magufuli sio vote winners; bahati ni kwamba upinzani ni weak and not trusted yet na wapiga kura kwa hivyo wana hiyo luxury ya kuropoka vibaya dhidi ya Magufuli.
 
Zamani ilikuwa ngumu kupata taarifa, sasa hivi sababu ya mitandao tunapata taarifa nyingi sana ila za uongo.
Ni kama ilivyo kuwa kipindi cha marekani kumsaka Osama bin laden,walikuwa wanaweza kupata zaidi ya elfu moja kwa siku,lkn zoote ni taarifa fake na za uongo.
 
Wewe ni mjinga pia..unazunguka zunguka wakati jibu liko wazi..mwigulu hana uwezo kiuongozi! Hapo alipo na nafasi zote alizopitia..taja mambo mawili km alama ya uhodari kwa uongozi wake.

Nchi inakuwa na mtu kwenye nafasi nyeti amekaa kitapeli tapeli kabisa, sijui ni ulozi..maana hata bahati haziko za namna hii..
 
Alikuwa waziri lakini alikuwa na wakati mgumu sana. Nadhani kuna wakati Magufuli alimtema kabisa toka Baraza la Mawaziri.
Alivuliwa uwaziri akiwa safarini. Akasimamishwa maeneo ya Nzega na kinyang'anywa gari ya waziri akapanda basi kurudi kwao Singida.

Baada ya muda jiwe alipokea ushauri wa kumrudisha ndiyo akamrudisha kwa kumuapishia nyumbani kwake Chato.
 
Alivuliwa uwaziri akiwa safarini. Akasimamishwa maeneo ya Nzega na kinyang'anywa gari ya waziri akapanda basi kurudi kwao Singida...Baada ya muda jiwe alipokea ushauri wa kumrudisha ndiyo akamrudisha kwa kumuapishia nyumbani kwake Chato.
Umeona eeh! Hayo ndio mambo yanamfanya awe na hasira sana na Magufuli. Lakini inatosha sasa, uungwana ni matendo na maneno

Na kwa nilivyomfahamu Magufuli alivyojua kuwaweka watu wanapostahili, sijui alimwapishia sehemu gani huko Chato; sebuleni, kibalazani, jikoni? Kuna picha?
 
Sijaelewa hata unachosema hapa, na nani unamwambia mjinga. Umesoma thread kweli?
 
Achana naye
Aaah, kwangu mimi katika viongozi wa Tanzania, hata ukisema tufanye top 100 hawezi kuwamo! Mwigulu alipaswa kubaki UDSM kama lecturer, period. He has a good cramming mind, but not capable of pragmatic, constructive analytical thinking. That excludes him from being a good political leader.
 
Uongozi wa Magufuli ulikua ni uongozi bora na wenye tumaini, kama taifa ilipasa tujutie ule uongozi kuishia njiani.

Uongozi ule ukitiwa doa kwa kiasi fulani na tukio lile la lisu kupigwa risasi,lakini hakuna njia nyoofu moja kwa moja isio na kona mteremko wala mlima

Mwigulu alikua na nia ya kua rais wa Tanzania lakini dhamna aliyopewa aikiwa waziri wa mambo ndani na hii ya waziri wa fedha ni wazi inaonyesha hastahili kupata dhamana yenye mamlaka ya mwisho kama urais, halina haja ya kuliongelea hili kwa kina kwani kila mwenye ufahamu anajua ukweli huu.

Chuki yake dhidi ya hayati ni vile kwa aina ya uongozi wake ule alizima ndoto nyingi za watu dhaifu kuutaka urais, sio kwa mwigulu tu bali kwa wengi ambao wanandoto na tamanio la kuwania uras ccm au kwingineko, Magufuli alikua kikwazo kwao.
 
Chuki yake dhidi ya hayati ni vile kwa aina ya uongozi wake ule alizima ndoto nyingi za watu dhaifu kuutaka urais, sio kwa mwigulu tu bali kwa wengi ambao wanandoto na tamanio la kuwania uras ccm au kwingineko, Magufuli alikua kikwazo kwao.
Mtu yeyote ambae anamchukia mtu aliekufa ni kwamba ana tatizo la afya ya akili! Ni mtu hatari sana huyo katika jamii, maana akimchukia mtu alie hai atamuua akiwa na nafasi hiyo!
 
Magufuli alimfundisha kuwa ukisifia Rais na ukajibizana na wapinzani wa Rais basi unatoboa. Kwa hiyo anaendelea ku practice alichojifunza
 
Na wewe inatosha sasa ku invent mambo Ili uonekane unajua.
 
rais samia ni bora kiliko ibilisi mwendazake.

over
 
Ogopa sana Mtu aliye Shiba na Maneno yake. OGOPA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…