Tunahitaji kukopa 80m kwa taasisi au mtu binafsi, Collateral zipo

Kokola

Senior Member
Joined
Sep 5, 2015
Posts
135
Reaction score
78
Wana JF tunahitaji kukopa 80m kwa ajili ya biashara iliyojitokeza. Tumejaribu benki lakini wametukatalia maana mwaka huu mapato yetu hayajaenda vizuri. Mali za dhamana (collateral) zipo. Kama yupo mtu binafsi au taasisi mbadala walio tayari kutupa kiwango hicho cha pesa tuweke mambo kisheria twende mbele. Hakuna wasi hapo kwani mali za dhamana zilizopo si za kuhamishika. Mwenye wazo au muhusika ani pm

Natanguliza shukurani
 

Okay kama collateral zipo, ni nani anakopa ? mtu binafsi, taasisi ? anafanya biashara gani ? uzoefu ? cashflow yake inamudu ?
 
Okay kama collateral zipo, ni nani anakopa ? mtu binafsi, taasisi ? anafanya biashara gani ? uzoefu ? cashflow yake inamudu ?

Soma vizuri uziwetu kama tungewa vizuri kwenye cashflow kwa mwaka huu usingetuona kutafuta mkopeshaji mbadala (sio benki). Jaribu kuelewa mada kabla hujaanza kuonyesha umahili wako.
 


kwa nini msiombe overdraft badala ya mkopo? maana ni rahisi kwa benki kumonitor movements za hiyo facility kuona kama biashara inaimprove au inakufa
 
Soma vizuri uziwetu kama tungewa vizuri kwenye cashflow kwa mwaka huu usingetuona kutafuta mkopeshaji mbadala (sio benki). Jaribu kuelewa mada kabla hujaanza kuonyesha umahili wako.

Mkuu kwa huu ukali kweli si mtu akishakukopa akija kudai pesa zake utamfukuza kwa bunduki ?

Sio wote wenye pesa au uwezo wa kukopesha wapo vizuri kwenye finance n.k. kwahio kama mtu amekosea au hajaelewa mueleweshe hata kama ni mara mia moja...

Beggars are not Choosers
 
 
 
hivi sheria inasemaje mtu binafsi kutoa mikopo?
 
Banki hawakubali collateral? Ni collateral ya aina gani?
 
Kwani wewe Unazijua collateral zipi zaidi ya real property ambazo unaweza kuchukulia mkopo kwa tz mkuu?
Kwa hiyo benki imekataa real estate? Mikopo hii haramu mtaani watu wanakubali magari/machine etc.
 

Thank you KeyserSoze.....
 
Last edited by a moderator:
Ndugu mleta uzi acha ukali. Huwezi kupata hiyo mkopo unaotaka kwa hiyo lugha yako mbovu. Niposoma uzi wako hapo juu nilitaa nikuelekeze/mwenye ningekuunganisha lkn jinsi unavyowajibu watu jukwaani dah!! sivyo. Kila la kheri.
 
 
Cash flow imeyumbishwa na kauri zako jirekebishe
 
Kama bank wamekataa kuwakopesha, huyo mtu binafsi atapata wapi guts za kuwakopesha kiasi chote cha pesa na mbaya zaidi biashara yenu haikufanya vizuri?
Milioni 80 ukopeshwe na mtu binafsi?
Kumbuka huyu mtu lazima akupe riba ambayo utajikuta unaiyumbisha biashara zako.
Bora muende bank muongee nao vizuri hata wakiwapa kwa installment huku wakiendelea kuminitor shughuli zenu.
Au uzeni hisa za 80M kwa watu binafsi waje kuwafundisha jinsi ya kusimamia biashara yenu.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…