Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Ndugu msomaji wa nakala hii fupi. Habari ya wakati huu. Naomba rejea kichwa cha nakala hii kama kinavyojieleza hapo juu.
Naomba kunukuu
"Tunahitaji mgombea binafsi wa ubunge ili wabunge wawe huru kutoa mawazo yao bungeni bila kuogopa chama".
Tangu nimeanza kufuatilia mambo ya siasa za dunia hii nimejifunza mengi ila bado naendelea kujifunza.
Katika kujifunza kwangu nimekuja kugundua kwamba wabunge walio wengi wanayo mengi ya kusema ila ni waoga, pengine wanaogopa na kuhofia kukatwa au kuwajibishwa na vyama vyao. Wengine wanaogopa kupokonywa ugali endapo kama wakishindwa kuzitumia akili za chama.
Siajabu hata mbunge Mnyika ataogopa kutoa hoja zake siku CHADEMA wakiwa ni chama tawala.
Hii ndio mantiki ya kuhitaji mgombea binafsi asiye na chama. Kama mtu anaweza kusimama mwenyewe na kugombea agombee tu.
Hili litampa uhuru wa kukosoa, kutoa mawazo, kujenga hoja bila kutumia akili za Chama.