Tunaingia Makaburini hatujatanguliza kheri yoyote

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Hakika binadamu ameshughulishwa Sana na wingi WA kutafuta Mali mpaka amesahau kesho itakuwaje,amesahau hakika hapa duniani yeye ni Msafiri na Mda wowote ataondoka.

Mwenyezi Mungu anatutaka tutafute dunia yetu na Akhera yetu pia,Kwa maana tupambane tupate ridhiki ya halali tupate Kula vya halali na kuvaa vya halali na kuwa na Maisha Bora kabisa.

Lakini

Wakati huo huo anatutaka tujiwekee hazina Bora ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari baada ya kuondoka hapa duniani,kwani mwisho wa siku tutaenda katika maisha mengine nje ya dunia hii.

Kuna ujumbe mmoja wa utani unasemwa na watu lakini umebeba ujumbe mkubwa Sana Kwa mtu mwenye kufikiri hatima yake unasema hivi;

Je kama sadaka ndio hela ya Matumizi yako huko Akhera unadhani ingekuwezesha kuishi kwa mda gani?

Ni utani lakini kuna ujumbe Fulani, ebu jitafakari wewe binafsi unafikir kwa sadaka yako uliyotoa ungetoboa miaka mingapi au miezi mingapi?

Hakika wengi wetu kama tungekufa Leo basi tungekuja kuwa ombamba huko mbinguni kwani naamini kabisa hizo sadaka tulizo toa ni hafifu mno kutuwezesha kufikisha miezi mitatu.

Tuwekeze katika maisha yajayo ambayo wengi wetu tunaamini yapo kwa mujibu wa imani zetu na Dini zetu.

Mwenyezi Mungu anasema hakika mwanadamu amekula hasara mpaka anaingia Makaburini hakuna kheri yoyote aliyoitanguliza ambayo itakuja kumfaa huko Akhera.

Kwahiyo ndugu zangu fanya utakavyo fanya na tafuta Maisha utakavyo lakini mwisho wa siku Sisi ni mavumbi na tutarudi mavumbini Tu kwahiyo hatuna budi kujitayarishia hazina ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari.

Walio tangulia wameshajua hatima Yao na laiti wangeweza kutupenyezea ujumbe basi wangetuambia:

Jamani Yale tulivyo ambiwa katika vitabu ni kweli na tumeyakuta huku msimdharau hata jambo moja!

Bahati mbaya wanashindwa kuwasiliana na Sisi na wanabakia kusema laiti walio bakia duniani wangejua hakika wangefanya Yale yanayo mpendeza Mwenyezi Mungu.

Kazi kwetu kufanya yale ambayo yatakuja kutufaa huko mbele ya safari.

Ni hayo Tu!

baby zu
Kazakh destroyer
adriz
Nurain
Akhi
 
"Kwahiyo ndugu zangu fanya utakavyo fanya na tafuta Maisha utakavyo lakini mwisho wa siku Sisi ni mavumbi na tutarudi mavumbini Tu kwahiyo hatuna budi kujitayarishia hazina ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari."
 
"Kwa hakika mmetujia sisi hali ya kuwa ni wapweke {mmoja mmoja} kama tulivyowaumba kwa mara ya kwanza na mmeviacha vile vyote tulivyokupeni nyuma ya migongo yenu, na wala hatuwaoni pamoja na nyinyi waombezi wenu ambao mlidai {huko duniani} kwamba wao ndio washirika kwenu, kwa hakika yamekatika mahusiano baina yenu na yamewapotea yale mliyokuwa mkiyadai."

Quran 6:94
637571088179342779.jpg
 
View attachment 2472257
Swadakta ujumbe uko wazi kabisa

Kubwa tuombe mwisho mwema

Amiin

Hlf mkuu hujareply pm yangu ingawa nimeona PM yako inasema this conversation cannot reply new messages, kama ina shida usijali mkuu.
 
Ni sadaka ya namna gani inahesabika huko akhera? Vipi ambao hatutoi sadaka/zaka huko misikitini ama makanisani lakini tunasaidia wenye uhitaji na kuishi vizuri mpaka na maadui zetu?
 
Sadaka iko katika namna nyingi Sana,hata kuongea na watu maneno mazuri ni sadaka.

Kupanda mti watu wakapata kivuli na matunda ni sadaka

Kuchimba kisima na watu wakanufaika na maji ni sadaka,tena hizi ni za kuendelea hata utakapo kuwa umekufa maadam watu wananufaika na maji, au ulimlipia mtu Ada akapata elimu ikamnufaisha hata kama umeondoka hapa duniani waendelea kuchuma.

Kwahiyo hata kusaidia watu wenye shida na uhitaji ni sadaka pia
 
Swadakta ujumbe uko wazi kabisa

Kubwa tuombe mwisho mwema

Amiin

Hlf mkuu hujareply pm yangu....ingawa nimeona pm yako inasema this conversation cannot reply new messages, kama ina shida usijali mkuu
Aaamyn, nimepambana sana kureply naona umenitilia bonge la kufuli mkuu, au ndo ushamba wa mambo ya PM sijui pa kugusa?.
 
Naona kuna shida ndio maana nimeona ule ujumbe, usijali ishu yenyewe sio sensitive Sana naweza pata jibu kwa member mwingine, Ila ishughulikie bhana unaweza siku ukapishana na gari la Mshahara hivi hivi hahaha
 
Hahahaha kama hapa nimeshahisi kabisa fursa inaweza kunipita by the way wewe ndo umefunga kwa upande wako ujue.
 
Sadaka iko katika namna nyingi Sana,hata kuongea na watu maneno mazuri ni sadaka.

Kupanda mti watu wakapata kivuli na matunda ni sadaka

Kuchimba kisima na watu wakanufaika na maji ni sadaka,tena hizi ni za kuendelea hata utakapo kuwa umekufa maadam watu wananufaika na maji, au ulimlipia mtu Ada akapata elimu ikamnufaisha hata kama umeondoka hapa duniani waendelea kuchuma.

Kwahiyo hata kusaidia watu wenye shida na uhitaji ni sadaka pia
Amin, umeinyoosha imeeleweka. Shukria
 
Hakika binadamu ameshughulishwa Sana na wingi WA kutafuta Mali mpaka amesahau kesho itakuwaje,amesahau hakika hapa duniani yeye ni Msafiri na Mda wowote ataondoka.

Mwenyezi Mungu anatutaka tutafute dunia yetu na Akhera yetu pia,Kwa maana tupambane tupate ridhiki ya halali tupate Kula vya halali na kuvaa vya halali na kuwa na Maisha Bora kabisa.

Lakini

Wakati huo huo anatutaka tujiwekee hazina Bora ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari baada ya kuondoka hapa duniani,kwani mwisho wa siku tutaenda katika maisha mengine nje ya dunia hii.

Kuna ujumbe mmoja wa utani unasemwa na watu lakini umebeba ujumbe mkubwa Sana Kwa mtu mwenye kufikiri hatima yake unasema hivi;

Je kama sadaka ndio hela ya Matumizi yako huko Akhera unadhani ingekuwezesha kuishi kwa mda gani?

Ni utani lakini kuna ujumbe Fulani, ebu jitafakari wewe binafsi unafikir kwa sadaka yako uliyotoa ungetoboa miaka mingapi au miezi mingapi?

Hakika wengi wetu kama tungekufa Leo basi tungekuja kuwa ombamba huko mbinguni kwani naamini kabisa hizo sadaka tulizo toa ni hafifu mno kutuwezesha kufikisha miezi mitatu.

Tuwekeze katika maisha yajayo ambayo wengi wetu tunaamini yapo kwa mujibu wa imani zetu na Dini zetu.

Mwenyezi Mungu anasema hakika mwanadamu amekula hasara mpaka anaingia Makaburini hakuna kheri yoyote aliyoitanguliza ambayo itakuja kumfaa huko Akhera.

Kwahiyo ndugu zangu fanya utakavyo fanya na tafuta Maisha utakavyo lakini mwisho wa siku Sisi ni mavumbi na tutarudi mavumbini Tu kwahiyo hatuna budi kujitayarishia hazina ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari.

Walio tangulia wameshajua hatima Yao na laiti wangeweza kutupenyezea ujumbe basi wangetuambia:

Jamani Yale tulivyo ambiwa katika vitabu ni kweli na tumeyakuta huku msimdharau hata jambo moja!

Bahati mbaya wanashindwa kuwasiliana na Sisi na wanabakia kusema laiti walio bakia duniani wangejua hakika wangefanya Yale yanayo mpendeza Mwenyezi Mungu.

Kazi kwetu kufanya yale ambayo yatakuja kutufaa huko mbele ya safari.

Ni hayo Tu!

baby zu
Kazakh destroyer
adriz
Nurain
Akhi
At-Takaathur (102:1)

أَلْهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُAlhakumu alttakathuru

Kumekushughulisheni kutafuta wingi,

At-Takaathur (102:2)

حَتَّىٰ زُرْتُمُ ٱلْمَقَابِرَHatta zurtumu almaqabira

Mpaka mje makaburini!
 
Back
Top Bottom