Tunaipokea treni ya mchongoko kwa shingo upande, ni kama ile ya zamani imechongwa kimchongo

Hebu fungueni karakana ya kuchonga pua
Yaani hii nchi ina lawama
Engineers wamejaa humu ila ila hata kukopi spana hamuwezi

China huo mchongoko wao inaenda mpaka 460km/h kwa majaribio na akiachia ni 501 km/h

Yaani unapanga kama tunaweza
 
Kwa hii huwezi kwenda hiyo speed ya 460!
Kwa hii ni dhahir Dar moro speed 50~60 hapo roho mkononi (masaa 3l
 
Kwa hii huwezi kwenda hiyo speed ya 460!
Kwa hii ni dhahir Dar moro speed 50~60 hapo roho mkononi (masaa 3l
Yaani huko speed gavana inawahusu
Wasiwaze kabisa kukimbia maana sisi speed ni kifo wao ni usafiri wa haraka
Mchina ni different species
 
" CHADEMA HAWANA JEMA HAWA JAMAA."
 
hata kama unamchukia sa100 hila hapa umeandika pumba.
 
Mtu mweusi achelewi kuweka kifuu li kuwe na mchongoko pale mbele
Kabisa, na yeye ni wa kuletewa rejects siku zote, ana chuma ya kutosha na viwanda vya chuma, plastic, umeme upo lakini hawafikirii kuanzisha kiwanda cha treni nchini kama ilivyo South Africa...anafikiria kuletewa tu na kupangiwa bei kubwa haswa yeye ni kupokea tu kana Mwanamke mchunaji
 
Mbona hii ni ya mchongoko ukaangalia Kwa makini hapo mbele Kuna part imetolewa ili iko kichwa kiweze kuvuta au kusukuma mabehewa na Kuna uwazi slots zinazoonyesha kwamba Kuna part imetolewa purposely
Bongo bahati mbaya
 
Mona picha ya hiyo treni inafichwa hata TBC wenye kiherehere hawaonyeshi
 
Mlitaka mchongoko mmeletewa
Mnataka nini tena????

Ova
 
Mbona hii ni ya mchongoko ukaangalia Kwa makini hapo mbele Kuna part imetolewa ili iko kichwa kiweze kuvuta au kusukuma mabehewa na Kuna uwazi slots zinazoonyesha kwamba Kuna part imetolewa purposely
Ni kweli, hapo mbele kwenye maungio kuna "structure" haijawekwa labda kwa makusudi kama ambavyo hata magurudumu hayajawekwa.

Tumeletewa kama tulivyoagiza ingawa naona baada ya kufika mbwembwe na umwagaji sifa umepungua ukilinganisha na ilivyonadiwa miaka miwili iliyopita.

Bado tuna kumbukumbu, speed 160 kwa saa.
 
Kila kitu watanzania ni kulalamika tuu..labda ndo maana tupo hivi hadi leo...
 
Usichanganye SRG, ambayo ni muundo wa reli yenyewe na mchongoko wa treni kwa mbele ili kuzuia air drag.
 
Usichanganye SRG, ambayo ni muundo wa reli yenyewe na mchongoko wa treni kwa mbele ili kuzuia air drag.
ukiweka kichwa mchongoko 100% kwenye standard gauge railway ni hatari zaidi πŸ’

mchongoko ambao unahisi na kufikiria ndio ungetakiwa kua, una aina ya reli na viwango vyake. Haya mambo hayafanywi kwa mapenzi, yanazingatia utaalamu πŸ’

hawajakosea kama ambavyo wengi pamoja nawe mnadhani..

imewekwa vile kitaalamu kuzuia speed isiyo kua yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…