Tunaipokea treni ya mchongoko kwa shingo upande, ni kama ile ya zamani imechongwa kimchongo

tatizo hamridhiki na chochote
 
Umenikumbusha zamani Tanga kulikuwa na basi likiitwa SHAKILA lilikuwa na umbo la mkate wa boflo
 
Kwa hii CCM usiamini kila kitu, watakuwa wamewaambia wachina waichoronge mbele ili kuridhisha watanzania, huku wakijua fika ndio tunachotaka kuona, ila specifics zinabaki pale pale, 80kph...

Nchi ngumu hii under CCM!!
Hatari sana

CCM ni wapigaji sana

Cc; Lucas Mwashambwa
 
Siwezi kuunganisha koment yangu ya zamani kwenye uzi huu lakini nilikomenti walipoleta vile vichwa vya kwanza nikawashauri TRC wasihangaike na maneno ya Watanzania, kwa kuwa baadhi yao wanapenda kufuata mkumbo.

Nikasema dawa ni TRC kurudi kiwandani na kumodify vile vichwa na kuwa mchongoko kwa sababu watu wengine wamekaririshwa vichwa mchongoko na siyo kuangalia ni kwa namna gani treni ina kasi

Kwahiyo, hapo dawa imepatikana, vichwa mchongoko ndiyo hivyo, kazi imeisha. Tuseme lingine sasa!

Yote kwa yote, kama ambavyo ni ngumu kwa Watanzania kununua magari zero kilomita ya miaka ya karibuni, nahisi ndivyo ilivyo kwa serikali za nchi zinazoendelea mfano Tanzania kushindwa kununua treni toleo jipya, zero kilomita. Ni gharama sana.

Mbona watu wananunua magari ya mitumba na yakifika bongo yanatembea tu na ndani ni mazuri, iweje tushangae treni ya mtumba?
 
Umepita mule mule komredi! Hongera
 
Kichwa kizima kimekaa kimchongo mchongo hivi. Ni kama kiliungwa ungwa na kupigwa rangi kisanii sanii.
 
Ni ngongongo iliyochangamka
Wewe utakuwa unaishi/umeishi maeneo yenye reli ya TAZARA bila shaka. Maana lile treni la mizigo huitwa kwa jina hili na wenyeji wanaoishi kando ya hiyo reli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…