Tunaishukuru ZBC kwa kutuwezesha kuona michuano ya CHAN, wengine wameshindwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa ZBC, viongozi wa Zanzibar pamoja na Wananchi wake wote kwa wema wao wa kuamua kutuhurumia na kutumia TV yao ambayo hatuchangii hata senti 5 kipande kwenye uendeshaji wake kutuonyesha michuano hii ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon.

Bila wao hii michuano Wananchi makapuku wa Tanzania wangeisikia kwenye magazeti tu. Hii ni kwa sababu TV nyingi za Tanganyika kazi yao kubwa ni kutuonyesha madaraja, vivuko, mafuriko ya Jangwani na mambo ya akina Giggy money.

Masuala ya soka ambayo ndio yanayopendwa mitaani wao hawayataki.

Mungu wabariki watu wa Zanzibar.
 
Mmmh!

Nadhani hujui kitu kuhusu ZBC2.

Hilo ni jina tu, mmiliki wake halisi ni Azam Bakhresa, na huo ni mkakati wake wa kupata rights za kurusha matangazo ya mpira kwa mgongo wa nchi (Zanzibar) kwa cheap price or free. Ni mkakati wa kibiashara kukwepa cost na kodi.

Mengi alifanya sana hichi kitu kutumia ITV wakati huo ITV ikiwa ndio television pekee inayotamba Tanzania.
 
ILA ZBC HAIONEKANI BURE, LABDA KWAKO SIJUI UPO MKOA GANI LAKINI BILA KULIPIA KIFURUSHI CHOCHOTE KWENYE AZAM TV HAUWEZI KUIONA ZBC.
MIMI MWENYEWE BINAFSI SIJAWEZA KUIONA KWASABABU SIJALIPIA.
 
ILA ZBC HAIONEKANI BURE, LABDA KWAKO SIJUI UPO MKOA GANI LAKINI BILA KULIPIA KIFURUSHI CHOCHOTE KWENYE AZAM TV HAUWEZI KUIONA ZBC.
MIMI MWENYEWE BINAFSI SIJAWEZA KUIONA KWASABABU SIJALIPIA.
Hata hivyo wamejitahidi
 
Uko sawa..hata CAF champions league group stage jamaa wa ZBC 2 huwa wanapewa rights baadhi ya games
 
Wewe ndio hujui chochote... Tuambie zbc 2 imeanza mwaka gani ??

Zbc2 haina hata miaka 5.. Na ile ni azam pure kbsa.. Hata mechi za ligi mda mwingine wanaonyesha zbc2 (kama mechi zikiwa nying zikichezwa mda mmoja)

Sasa tafakari mwenyewe
 
Zbc2 ina milikiwa na Bakhressa.

Anatumia Zbc2 kuonyesha mechi ambazo hana haki kuonyesha, hivyo kuepuka mgongano wa kimaslahi na makampuni mengine ya kibiashara anatumia ile ZBC2 ambayo watu wanajua kuwa ni ya serikali kumbe ni ya kwake.


Disition zote za ile channel zipo chini yauwangalizi wake yeye ndio mean sponsor

Kwenye issue yakurusha matangazo mafano Kama ya hii michuano ya Chan, ananufaika kupitia mgongo wa channel ya Serkali Pay blll inakua ndogo.


Hi fixed wakina DStv wakisanuka wanauwezo wakumshitaki.

Kiuhalisia angalia hata graphics/rangi na ubora wa Zbc na ZBC2 ni vitu viwili tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…