Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Wadau,

Baada ya CCM kushindwa na nguvu ya mageuzi ya kudai uwepo wa KATIBA MPYA ya wananchi(tofauti na ile ya 1977 ambayo ilitengenezwa na wachache kwa niaba ya Watanzania) hatimaye mchakato wa kupata KATIBA mpya ukaanza.

Baada ya patashika nguo kuchanika hatimaye rasimu zikaanza kutengenezwa na mabaraza kupatikana. Mwisho wa yote wajumbe wakapatikana(kundi la 201 na wale wabunge wa bunge la JMT na BWZ).

Bunge Maalumu la Katiba likazinduliwa na Mh rais wa JMT na tukayasikia tuliyoyasikia na mijadala mizito yenye mashiko ikaanza Ndani ya Bunge na NJE ya Bunge.

suala la Muundo wa serikali likabeba kwa kiasi kikubwa hisia za watanzania wengi.Ikatokea hata wajuzi wa mambo kuhoji uhalali wa muungano ulioisshi miaka Hamsini.

Baada ya mvutano mkubwa yakatokea makundi mawili UKAWA na "INTARAHAMWE". Kundi la UKAWA likaona lina buruzwa na kuja kwa wananchi kutoa kilio chao na hao wengine wakabaki na kuendelea na vikao.

Katika vikao vya UKAWA hoja ya ujio wa TANGANYIKA ukaonekana kushika kasi.

Mie mleta hoja nawauliza wanabodi:
1: Tanganyika ikirudi je na chama chetu cha TANU ambacho kiliipigania Tanganyika huru na chenyewe KITARUDI?
2: Kama hakitarudi je, misingi yake itabebwa na chama gani kati ya hivi vilivyopo;CCM,CHADEMA, CUF,UMD,NCCR,ACT
TLP nk?
3: Kama kitarudi kipo tayari kuongoza nchi nje ya malengo na itikadi yake ya Ujamaa na Kujitegemea?

Naomba kufungua mjadala.

cc Mchambuzi Nguruvi3, Tumaini Makene, Ritz, Mwigulu Nchemba MSALANI, @Dr Kitila Mkumbo, kababu
 
Kaka sasa hivi ni TZ kwanza habari ya vyama baadaye. Shime tushirikiane kwa lengo la kujenga na tuache siasa za Uvyama ili tuijenge Nchi. Hivyo vyama siyo pepo bali ni moto kama vitatumika kunyonya maslahi ya wengi. Nadhani swali lako sintaweza kulijibu kwa kuwa mimi msimamo wangu ni Tz kwanza vyama baadaye.
 
Hivi Chama cha TANU kinarudishwaje jamani? Yaani watu badala ya kufikiria kusonga mbele tunafikiri kurudi nyuma!
 
Mkuu, maneno yako nimakali kuyasikia. Ila lazima Tanganyika yetu ipatikane.
 
Ni ile tunayoisherehekea tarehe 09/12 kila mwaka................
Ni kiini macho, hebu tazama maudhuiyote ya sherehe hizo na upime uzani wa kumbukumbu za Muungano, katu huwa haitajwi Tanganyika au ule uwanja wa Taifa/Uhuru upande mmoja uwe ni wananchi toka Zanzibar na mwingine uwe ni wananchi toka Tanganyika (iwe hadharani).
 
Tanganyika ni buzi la Zanzibar wanachunwa mpaka ngozi hawajitambui ! Watanganyika wamegeuzwa ndondocha na wazenji !
Haya maneno makali, ila Watanganyika tupo na ndio maana tunaililia.
 
Tambua pesa inayopelekwa Zanzibar ni Matirioni na matirioni hizo Fedha zikisalia Tanganyika Uchumi utakuwa kwa kasi huduma za jamii zitaimarishwa japo kuna ufisadi lakini si kigezo cha kuwazuia Watanganyika wasidai Nchi Yao
Nakuunga kwa ulilonena hapa.
 
Brilliant input, umenena vema sana mkuu.
 
Inadaiwa Muungano unang'ang'aniwa kwa sababu za kiusalama tu.
 
Well said comrade.
 
Hivi Chama cha TANU kinarudishwaje jamani? Yaani watu badala ya kufikiria kusonga mbele tunafikiri kurudi nyuma!
ukishindwa kukirudisha TANU itakuwa ngumu kuirudisha TANGANYIKA.
 
Unachotakiwa kujua kuwa Tanganyika ipo..ndo maana kuna mambo yasiyokuwa na muungani kama umewahi kushughulika na mambo ya viwanja utaona mhuri unaopigwa ni watanganyika, Tanganyika ipo kwny kivuli cha serikali ya muungano
 
hao viongozi watakao ngoja tanu wameshakufa ....
 
Wakuu, Kama mtu akiuliza Tanzania Ni zao la Muungano wa nchi mbili yani Zanzibar na Tanganyika, je Tanganyika iko wapi? Mbona haipo Kama Zanzibar? Mbona Muungano umekaa Kama vile Ni Muungano wa Tanzania na Zanzibar, huku Zanzibar ipo Kama state?

Zanzibar ina serikali yake,, ina Bunge lake, ina mahakamani yake, Mbona Tanganyika Haina mihimili hiyo muhimu na haijulikani iko wapi kikatiba?

Wakuu,, Tanyanyika ya watanganyika iko wap kikatiba?

Watanganyika wote tutoane tongotongo, huu ni Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar au Tanzania na Zanzibar??
 
Ccm wanajitahidi sana kupotosha. Muungano ni kati ya Tanganyika na Zanzibar! Na siyo Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…