Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Tunaitaka Tanganyika yetu! Wakati ni huu...

Baada ya miaka 50 je unaweza kufukua kaburi na kutoa kitu kilicho hai? Je kurudi kwa Tanganyika kutasaidia kupunguza ukali wa maisha yetu ya kila siku ? Je ufisadi utapungua na raslimali zigawanyewe sawa kwa wote? Je Afya, Elimu, Makazi zitaboreswa?

Kama haya yatatekelezwa na nikihakikishiwa basi na mimi nitachukua jembe kwenda kusaidia kulifukua kaburi ili Tanganyika atoke akiwa hai

Tambua pesa inayopelekwa Zanzibar ni Matirioni na matirioni hizo Fedha zikisalia Tanganyika Uchumi utakuwa kwa kasi huduma za jamii zitaimarishwa japo kuna ufisadi lakini si kigezo cha kuwazuia Watanganyika wasidai Nchi Yao
 
Wanabodi!!!

  1. Unawachukua wabunge 80 toka Visiwani (kwa miaka50!) wanakaa Dodoma wanajadili Barabara za Geita na Katavi. Unawalipa msharahakila mwezi na posho kwa kodi toka Tanganyika!
  2. Unammchukua Makamu wa Raisi, Mawaziri, Mabalozi na 20% ya wafanyakzi wa Wizara za Muungano toka visiwani.. kisha unawalipa mishahara na posho (kwa miaka 50!) kwa kodi za Watanganyika!
  3. Tunajuinga na Afrika Mashariki. Bara wanalipia pesa ya kodi gharama za Afrika Mashariki.. Wabunge ni 9 kama walivyo wabunge toka Rwanda (9), Kenya (9). Then!!!!! Tanyanyika inatoa Wabunge (6) Na Visiwan iwabunge (3). Then Bara kwa kodi zao unawalipia wabunge wa Visiwani katika Bungela Afrika Mashariki!!!
  4. Unawateua wabunge toka Visiwani kamati za Bunge Muungano kukagua barabara kule Ngara na Tandahimba unawalipa pesa ya kodi ya Tanganyika kwa miaka 50!
  5. Halafu unakaa unajivuna Muungano huu ni waKuigwa Bara la Afrika na Dunia yote na unajipiga2 kifua kuwa na fikra sahii za waasisi wa Taifa hili!
  6. Miaka 50! Wewe unakuwa rafiki au mshirika wangu!Siku zote tukionana mimi nakununulia tu soda au bia wewe.. wewe hata siku mojahaununui… na unaona ni poa tu! Kwa mika 50!
  7. Halafu watoto wetu wa shule kule Handeni naKondoa wanakaa Chini hawana madawati na tunalalamika na kuona ni sawa!
SAA INGINE NAONA KAMA TANGANYIKA AU TANZANIA BARA TUMEROGWA AND WE ACTUALLY DO NOT KNOW OUR PRIORITIES!
WATOTO NA WAJUKUU ZETU WATAULIZA SIKU MOJA NA HATUTAKUWA NAMAJIBU!

WATANGAYIKA TUAMKE TUACHE UNAFIKI HUU!

Tanganyika ni buzi la Zanzibar wanachunwa mpaka ngozi hawajitambui ! Watanganyika wamegeuzwa ndondocha na wazenji !
 
Sasa Nadhani wale Wazenji walalamishi Kama wanafika JF Habari wataipata angalau sasa watambue ni jinsi gani wamekuwa Zigo kwa Watanganyka ambao wanataabika kwa kuwalea wazenji huku familia zao wakilia huduma za jamii zipo taabani.
 
Mimi binafsi sivutiwi na jina la Tanganyika na kama katiba mpya itatambua uwepo wa serikali tatu mimi kwa maoni yangu ni bora sisi wa upande wa Tanzania bara tubaki na jina la Tanzania bara au litafutwe jina lingine.

Ukweli neno "Tanzania bara" does not sound well and it is not appeaing to the senses.

Haya ni mawazo yangu.

Je,wewe mwana JF mwenzangu una maoni gani?

Tunaweza kuanza kutoa maoni kupitia JF ingawa katiba mpya bado haijapatikana ila uwezekano wa serikali tatu ni mkubwa kwa kuangalia mazingira ya sasa na maoni ya walio wengi.

Hilo jina Tanzania asili yake ni Tanganyika si Zanzibar jina alipendekeza Nyerere hivyo Sidhani Kama kuna shida kuitwa majina yote mawili yaani Tanzania aka Tanganyika . Cha Msingi ni Hawa Watu Milion 44 kupelekeshwa na Watu Milion 1.5 tu kama Nyumbu , Zanzibar imewageuza Tanganyika Ndondocha .
 
Mimi pia sipendi Tanzania Bara. I am in love with Tanganyika. Hiyo ndiyo historia yetu. Tanganyika ndiyo ilipata uhuru 1961.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Tanganyika si Tanzania Bara wanaita hivyo wanapotosha jina ! Tambua huku panapoitwa bara si bara kihalisia kwani kuna Visiwa Vingi sana Baharini hadi Kwenye Maziwa Visiwa vimejaa watu . Tambua huku Panaitwa Tanzania tu si tz bara .hilo jina Tanganyika litumike pindu Uhuru ukirejeshwa Pia tunaweza kutumia majina yote mawili yaani Tanzania a.k.a Tanganyika ili Usajili wa jina pale UN usichukue mda kubadili jina.
 
Siku muujiza wa Tanganyika kujikomboa ukitokea Nina imani Tanganyika itabakia na jina lake la Tanzania ambalo ndilo limesajiliwa pale New York UN ili kuondokana na Usumbufu wa wageni na watalii kuja Nchini . Hivyo Zanzibar Ndio wataenda kujisajili Upya UN sisi tutasalia kuitwa Tanzania a.k.a Tanganyika Ukweli unabakia jina Tanzania asili yake ni Tanganyika Hilo jina aliotoa Nyerere na ujumbe wako toka Tanganyika.
 
Katika mambo ya kitaifa hatujaona mchango wa zanzibar katika kuyatekeleza.Mfano mdogo no garama za machakato wa katiba.

Tume ya Warioba imebeba sura ya 50:50 kwa bara na znz , lakini tunaambiwa tume hiyo imetumia zaidi ya bilioni 60. Tukiuliza znz imechangia kiasi gani hatupewi majibu. waziri wa fedha tanzania ni mmoja ana droo yake ni hazina, kwa znz wanayo wizara yao ya fedha na hazina yake.

Mchakato wa katiba hatuambiwa unagaramiwa na serikali ngapi au kujua bara wanachangia % fulani na znz %. tunachoelewa ni kuwa mchakato ule unagaramiwa na tanzania.

Ukubwa wa majimbo: jimbo la uchaguzi znz lina watu elfu 2 mpaka elfu 5. wakati jimbo la uchaguzi bara lina watu laki 4. Hawa wabunge wote wanaliwa sawa yaani kila mmoja zaidi ya milioni 11 kwa mwezi.Hapa kuna utata mkubwa sana kata pekee ya tanganyika inakuwa na watu mpaka elfu 20.

Hii ni kusema management ya watanganyika ni mbovu sana ukilinganisha na waznz.pesa inayokwenda znz ni kubwa kwa wingi wao,dar yenye watu zaidi ya mil 5 ina wabunge 7, angali Zanzibar yenye watu mil 1.2 ina wabunge 80. Jamani, hapo kuna usawa?

Uendeshaji wa wizara ya mambo ya nje.Balozi karibu zote za nchi yetu huendeshwa kwa msaada, maana nyingine mikopo , unaposikia serikali inashindwa kujiendesha mara nyingi husababishwa na mambo hayo.Sasa kama tunakopa kama tanzania alafu wenzetu wanaona kama wao sio wa tz ni hatari sana maana tunabebesha mzigo mkubwa wa kodi kwa watanganyika.

Ukubwa wa kodi bara: Ukubwa wa kodi Tanzania unasababishwa na mzigo iliyobeba.

Kupoteza utaifa na kuonekana kama mwizi znz. Kuna katabia kamejengeka kuita watanganyika wakoloni weusi, kiasi kwamba hata mtanganyika mshona viatu au muuza maji kule znz huonekana kama mwizi anaishi roho juu kama yuko ugenini hali hiyo sio nzuri, kama uzanzibar unaendelezwa ndani ya tanzania kwa nini na utanganyika usiendelezwe?.
 
Last edited by a moderator:
tukubali tukatae wazanzibar ni wabaguzi pia kwanini mzanzibar mahala popote pale anajitambulisha kama mzanzibar na sio mtanzania? kwa nini na sisi tusijitambulishe kama watanganyika?
 
Poa sana. Watanganyika wanaumizwa na ccm. CCM ikiondoka neema ya Tanganyika itarejea, Tulianza na Mungu Tutamaliza na Mungu!
 
Ongezea na hii,

-Tunataka sasa Serikali ya Tanganyika ili tulinde rasilimali zetu wenyewe, viongozi wa serikali ya JM ya sasa ndiyo vinara wa kupora na kuhujumu rasilimali za "Tanganyika" isiyo kuwa na serikali.

-Pesa zinazo patikana toka "Tanganyika" zinatumiwa vibaya na serikali ya JM. kwani hakuna Serikali ya Tanganyika itakayo hoji kama inavyoweza kuhoji serikali ya Zanzibar.

-Wakati maamuzi yanayo ihusu Tanganyika yanapofanyika, wazanzibar wanashiriki na kupewa nafasi sawa ya maamuzi.

-Tunataka Serikali ya Tanganyika ili tujitambue, tulitambue Taifa letu na kulilinda.
 
CCM watasema kwa nini uongeze mke?yaani point zao ni za mifano ya Gender tuu na kutishia vita wananchi na kusema eti sultan atarudi zanzibar.Binadamu lazima ukubali mabadiliko katika maisha
 
Hujisikia uchungu sana pale ninapomsikia mjumbe wa Kitanganyika anapoukana uraia wake kwa kuukataa mfumo wa serikali tatu.
 
Cccm wote wana fanana point za kijinga kweli eti kwanini tuongeze mke alafu vijana wengine sijuwi wamelogwa na nani bado hawaja amka kujuwa kuwa ccm ni ngenge la watu wanao la wezi hatari hawana huruma na aibu ata kidogo yani
Tutegemeye baraza la mawaziri lenye familia zao !
 
Ongezea na hii,

-Tunataka sasa Serikali ya Tanganyika ili tulinde rasilimali zetu wenyewe, viongozi wa serikali ya JM ya sasa ndiyo vinara wa kupora na kuhujumu rasilimali za "Tanganyika" isiyo kuwa na serikali.

-Pesa zinazo patikana toka "Tanganyika" zinatumiwa vibaya na serikali ya JM. kwani hakuna Serikali ya Tanganyika itakayo hoji kama inavyoweza kuhoji serikali ya Zanzibar.

-Wakati maamuzi yanayo ihusu Tanganyika yanapofanyika, wazanzibar wanashiriki na kupewa nafasi sawa ya maamuzi.

-Tunataka Serikali ya Tanganyika ili tujitambue, tulitambue Taifa letu na kulilinda.

ata mimi binafsi nahitaji kwanza nchi yangu Tanganyika itambulike kwanza ndio tudiscuss hizo issue nyingine za muungano.
 
Tanzania haijawahi kupata uhuru.nchi iliyopata uhuru ni Tanganyika.nasema tumechoka.kama noma na iwe tutaidai Tanganyika yetu kwa gharama yeyote.wazinzibar mtaendelea kuwa vimelea mpaka lini kama kupe.
 
Ethiopia haijawahi kutawaliwa hivyo haikuwahi kupata uhuru...Tanganyika ilitawaliwa na Mjerumani mpaka 1918 baada ya vita vya kwanza vya dunia tulikuwa huru ila chini ya udhamini wa Uingereza!! mwaka 1961 ilikuwa makabidhiano tu siyo uhuru!... Jaribu kujenga hoja yenye mashiko labda watakuelewa wenzio... Sisi Tuliozaliwa baada ya 1961 katika nchi inayoitwa Tanzania tunataka kero za muungano ziondoshwe hata hivyo issue kubwa kwetu ni maendeleo hata mkiwa na serikali 100 ...Tuambie baada ya wewe na vibabu na vibibi wenzio mkiipata Tanganyika Social GAP itapungua? Watoto wetu watapatiwa quality education? Social services kama maji safi na salama, afya, umeme, barabara, reli, zitaboreshwa? Mishahara ya watumishi itaboreshwa kulingana na gharama za maisha? wakulima, wafugaji na wafanyabiashara mtawanufaisha vipi chini ya Tanganyika yenu? Mikataba mibovu ya madini Mlioingia ninyi Wazee mtazi-review?... acha porojo njoo na mada yenye mashiko hapa tuijadili siyo majina...
 
Back
Top Bottom