Naam,
Moshi mweupe unafuka, kuashiria ujio rasmi wa Tanganyika yetu iliyopotea.
Shukran nyingi na zakipekee zimfikie Jaji Warioba na wajumbe wake, ambapo moja ya jambo muhimu kabisa ni kuihuisha Tanganyika iliyopotea.
Ni furaha iliyoje kwangu mie kijana wa Kitanganyika? Hakuna fahari yoyote duniani kama utaifa, yaani nchi yako kamili na asili.
Nitakushukuru maradufu Muumba siku ambayo bendera ya taifa la Tanganyika ikipandishwa, nitawashukuru zaidi Watanganyika wenzangu walioipigania mpaka kuipata Tanganyika yetu tena. Bali nitaishukuru maradufu JF kwa kutupatia sisi wadau uhuru wa kupaza sauti za vilio vyetu na kuhifadhi kumbukumbu, ambapo hii leo yajionyesha.
RUDI Tanganyika RUDI.
Mpevu