Tunajifunza nini kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini Malawi?

Tunajifunza nini kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu nchini Malawi?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Siku ya Jumanne ya terehe 23/06/2020 Wananchi nchini Malawi, walipiga kura katika uchaguzi wa marudio, baada ya yale ya awali yaliyompa ushindi Rais aliyeko madarakani, Peter Mutharika, kutenguliwa na Mahakama ya kikatiba nchini humo.

Tukumbuke kuwa Peter Mutharika alitangazwa na Tume ya Taifa nchini humo kuwa alipata ushindi mwembamba, katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo, mwezi Mei mwaka 2019, kwa kumshinda mpinzani wake mkubwa, Lazarus Chakwera, wa muungano wa upinzani, wa kupata ushindi wa asilimia 38.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, Jane Mansah, kuliibuka maandamano ya wananchi wa nchi nzima, wakidai kuwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, ilifanya udanganyifu kwa kumtangaza Rais aliyeko madarakani, Peter Mutharika, kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi huo.

Hata hivyo Muungano wa Upinzani nchini humo ulifungua kesi katika mahakama ya kikatiba kupinga ushindi huo uliotangazwa wa Peter Mutharika.

Hatimaye mwezi Februari ya mwaka huu, mahakama hiyo ya kikatiba, ilifanya uamuzi wa kihistoria, kwa kutengua matokeo hayo ya uchaguzi na kuamuru kuwa uchaguzi huo urudiwe, tena kwa kutumia sheria mpya ya uchaguzi huo kwa mgombea wa kiti cha Urais, ni lazima apate ushindi wa zaidi ya asilimia 50, kinyume na sheria ya hapo kabla ambayo ilikuwa ikimtaka mgombea wa kiti cha Rais, atangazwe mshindi, kwa ushindi wowote, hata ule wa (simple majority) ambayo ni chini ya asilimia 50 ya wapiga kura nchini huko.

Hata hivyo kwa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa na vyombo vya habari vya serikali ya Malawi, ni kuwa hadi hivi sasa mgombea wa upinzani, Mchungaji Lazarus Chakwera, anaongoza kwa kupata kura asilimia 59 ya kura zote zilizohesabiwa hadi hivi sasa, akifuatiwa kwa mbali sana na Peter Mutharika, ambaye ndiye Rais aliyoko madarakani hadi hivi sasa, ameambulia kura asilimia 38 pekee!

Kama Taifa la Tanzania tunajifunza nini kwa matokeo hayo ya uchaguzi mkuu wa Malawi?

1. Ni lazima kiwepo kipengele kwenye Katiba ya nchi, ambapo matokeo ya Urais yanaweza kupingwa mahakamani

2. Kuwepo hapa nchini kwa mahakama ya kikatiba, ambayo itaweza kusikiliza kesi za kupinga matokeo ya Urais kwenye uchaguzi mkuu, iwapo yatajitokeza

3. Ni lazima tuwe na Tume huru ya uchaguzi wa Taifa na ionekane katika muundo wake kuwa ni huru kweli kweli

4. Kuwepo na Muungano ya vyama vya upinzani usiokuwa na masharti magumu kama yalivyo nchini kwetu

Ninaamini yakifanyika marekebisho hayo muhimu katika Katiba ya nchi yetu na katika mifumo ya chaguzi zetu, ndipo tutakapojidai kweli tuna demokrasia iliyokomaa nchini mwetu na itatuepushia nchi yetu isiingie kwenye machafuko yanayoweza kuhatarisha maisha ya wananchi wetu.

Mungu ibariki Tanzania
 
Kwamba Tume yao ya Uchaguzi ni Huru kweli katika maana halisi ya kuwa huru.
 
Mifumo yao ipo huru.Huwezi kuta inaingiliana au kumilikiwa na mtawala, tofauti na sie, mfumo wetu wa uongozi aliouasisis Nyerere copy na paste toka kwa dikteta Mao wa China ndio unatutesa,maana umeundwa kwenye misingi ya mtu mmoja kuwa juu kuliko katiba na hakuna kipengele kinachomdhibiti ukishakuwa na mfumo kama huu tegemea kuongozwa Kama familia ya mtu binafsi ndio unaowafanya hata polisi kutenda hata wasiyoyataka kutii maagizo au kufutwa kazi, tofauti na Malawi mifumo yao ipo huru hakuna aliye mkuu kuliko katiba.
 
Nilichojifunza hapo hakuna wakuishinda nguvu ya umma.

Na mihimili mingine ya nchi (mahakama) lazima iwe huru, isiingiliwe na serikali, hapo ndipo haki itatendeka.
Ni kweli kabisa, wenzetu Malawi wametuzidi sana kidemokrasia, kwa kuwa mhimili wao wa mahakama upo huru kabisa, unaoweza hata kutengua ushindi wa Rais aliyeko madarakani!

Wakati mahakama zetu za hapa nchini, Jiwe anatamba kuwa mhimili wake ndiyo uliojichinbia zaidi chini na yeye ndiyo aliouweka mfukoni mhimili wa mahakama!
 
Kuna wadau wa kusoma hii thread wanaona ukweli mtupu ila watapita kama vile awajaisoma ...Ahsante sana mleta mada.
 
Hawana Jecha hao 😁 😀
FB_IMG_1592719242994.jpg
 
Cc: Paschal Mayalla & Co.
Na kwa kuwa uchaguzi huo umeendeshwa kwa Uhuru na haki na kila mshiriki wa uchaguzi ameridhika, hakuna tena maandamano ya kupinga matokeo.......

Hata wafuasi wake Rais aliyeko madarakani, Peter Mutharika wameridhika na kuyakubali matokeo hayo ya kushindwa kwenye sanduku la kura

Huo ndiyo ukomavu wa kisiasa ambao sisi kama nchi tunapaswa tuwaige hao majirani zetu wa Malawi
 
Uko sahihi mtoa mada, lazima tume ya uchaguzi iwe huru na mihimili yote ya nchi (Bunge, Serikali, Mahakama) iwe huru.
 
Back
Top Bottom